Kwanini Marais wengine huogopa kwenda kuongea na wasomi wa UDSM-Mlimani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Marais wengine huogopa kwenda kuongea na wasomi wa UDSM-Mlimani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtego wa Noti, Nov 28, 2010.

 1. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Ndugu wana JF,

  Wakati uhai wa Mwalimu Nyerere, alikuwa akienda pale UDSM kukutana na wanazuoni na kufanya nao mijadala mbalimbali ya namna ya kuendeleza nchi na dunia kwa ujumla. Hivi karibuni nimeshuhudia Marais wengi waliokuja baada ya yeye kama vile Mzee Ruksa, Mkapa na JeiKei wakikwepa sana kutia maguu yao katika viunga vya UDSM, mlimani na kukimbilia katika vyuo vichanga kama UDOM.

  Je, hii inadhihirisha kuwa wanaogopa kukutana uso kwa uso na wasomi waliobobea pale Mlimani? Au kuna kingine zaidi?

  Naomba majibu wanaJF...
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Wasome wepi hao hawa wa aina ya Kitila mkumbo au aina ya Rweikaza mukandala na akina Bana??

  Kinyume na unavyoweza kusema au kuwaza, niko hapa mlimani kwa miaka 10 sasa!

  Hakuna agenda, pressure , misukumo na hali zozote tete (tension) zinazoweza kumyima usingizi rais wa sasa 9na hao waliopita) na awaze kwenda UDSM! hao wasomi wa caliber za enzi zile za Nyerere hawapo kwa sasa!

  Usije ukafikiri eti kuna vichwa sana na hao akina JK wanaogopa kuja, NO! kila professor anawaza maisha yake, kila mwanafunzia anawaza apate wapi desa na kushinda kwenye viunga vya bodi ya mikopo!

  Huwezi ukasema mtu kama Mkapa alikuwa anawaogopa! labda haumjui Mkapa!!! hakukuwa na msukumo wa wao kwenda mlimani, ila Mwinyi alikimalizia kile kizazi cha wale wasomi waliokuwa wanawaza maslahi ya taifa

  Nenda mlimani leo hii,nenda utawala, utacheka sana, hakuna sehemu vitu vinafanyika baghala shaghala kama mlimani!

  WANACHUO HAWA (KUANZIA WALIMU NA WANAFUNZI) wamejidharaulisha wao na kudharauliwa HAWANA ILE SAUTI YA MAMLAKA YA KUOGOPWA NA SERIKALI haipo! ndio wanachuo hawa wakimaliza wakishapata hatchbacks za mikopo na kupanga sinza, they dont care even to vote!

  Kuna mengi yamesababishwa na hayo
   
 3. a

  awtu Member

  #3
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Only those with intellectual confidence can face the likes of Shivji, Mvungi & Semboja!
   
 4. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  NOw I understand... Inawezekana serikali ndio inawafanya wanachuo wawe busy kufikiri mikopo yao ili wakose muda wa kujadili matatizo ya Kitaifa. I agree with u 100%, lakini naona kama bado kuna vichwa makini kama akina Shivji, Lwaitama na wengine wachache ambao bado ni misumari ya hatari kwa kujenga hoja ukiondoa hao akina Mkandala na Bana ambao tayari wako kwenye mifuko ya CCM na ni mawakala wa CCM hapo Mlimani
   
 5. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Waberayo:

  Wasomi wa Tanzania ni pathetic. Hiyo enzi ya Nyerere wanafunzi wa chuo kikuu walikuwa kwenye maisha ya hoteli ya kitalii wakati wananchi wa kawaida walikuwa na maisha duni. Na wengi ndio wanaoongoza nchi sasa. Sasa kama kuna kitu walijifunza kwenye kuongea kwao na Nyerere, mimi sikioni.
   
 6. F

  Ferds JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hivi wewe bado unahesabu UDSM ni chuo, matatizo matupu yamejaa hapo kilimani, watu mabonzo na maconservatives wamejaa hapo nani aje, wanafunzi wanawaza kuingia bungeni na harakati za kisiasa masaa 24 , yaani kimebaki jina elimu ikovyuo vingine sio hapo, halafu enzi za nyerer angeenda waoi coz chuo kilikuwa hicho tu kimoja sasa unavingapi acha mawazo mgando wewe
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  There are many reasons why UDOM was built.
   
 8. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kwani pale kuna wasomi siku hizi? au ni mamuluki wa ccm tu? kwani si ndio hao wasomi waliotoa REDET/synovate? au nimesahau...
   
 9. M

  Matarese JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  UDSM sasa hivi hamna kitu, kila mtu anafikiria kumfisadi mwenzake. Hata Wahadhiri wenyewe kwa wenyewe wanabaguana, wengine wanastahili kupewa nyumba wengine hawastahili, kwa ufupi ni ubinafsi na unafiki umejaa UDSM!
   
 10. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Msipotoshe hakuna chuo chenye uhuru kama UDSM hasa hasa vya umma,hata waadhiri
  wanaweza tofautiana(boycott) na management na baadae wakaelewana.lakini nenda UDOM
  uone wanafunzi wakitofautiana na mgt usiku usiku unafuatwa uanaondolewa Chuoni hadi kwenu and non back.but udsm wanafunzi waweza fukuzwa na baadae rudishwa.

  waadhiri UDOM walitofautiana na mgt wakatimuliwa wakaambiwa hii sio UDSM,means no
  democracy.udsm bado kuna vichwa ambavyo vinasumbua kama Lwaitama na havipatikani
  anywhere na kama vinapatikana bado vinauoga au vinatishiwa na mgt zao.
  udsm still a centre of democracy in tcu na ya kuigwa,JK anatambua hilo


  'IF YUO HAVE NO CRITCS YOU'LL LIKELY HAVE NO SUCCESS'....Malcolm X
   
 11. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  UDSM NI CHUO CHA SISIEM.redet/synovate
   
 12. mdukuzi

  mdukuzi JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 5,372
  Likes Received: 4,220
  Trophy Points: 280
  enzi za mwinyi alitaka kuja kuongea na wana UDSM wakati wa mgomo akaambiwa kama anataka kuja aongee English akaogopa akamtuma warioba
   
 13. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2014
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Jk alikuja akazomewa na wanafunzi..mpaka leo hajatia maguu tena.
   
 14. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2014
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Watakuwa wanaongea na msomi wetu namba moja, mh. Mwigulu Nchemba. Huyu anatosha kuwasemea na kuwajibia hao wasomi wote unaowafikiria.
   
 15. K

  Kihega JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2014
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 1,338
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Pap...pap... pap... pap... pap... pap... pap!
   
Loading...