Kwanini Marais wengi duniani wakiwa na Hafla na Wanajeshi Ulinzi wao na wa eneo husika huimarishwa zaidi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,875
Hii nimekuwa nikiiona sana nchi za Marekani, Urusi, China, Korea Kaskazini, India, Afrika Kusini, Uganda na Rwanda ( ila kwa Tanzania bado sijaiona na nadhani pia haipo kwani Marais wetu wote huwa wanakubalika na wanaaminika sana na Wanajeshi wetu ) na imekuwa ikiniacha na Maswali mengi mno. Naomba wale ' Wajuvi ' wa haya mambo muweze Kunisaidia Kunielewesha tafadhali.

Nawasilisha.
 
Naona umetupa kaa la moto kwenye banda la bata, ingawa wana njaa lkn wanaogopa kulitafuna. Vijana wanachungulia uzi na kupita kimya kimya. Si kwamb hawataki kuchangia ila.....
 
Niko hapa ubalozi wa Burundi pembeni ya lango la magharibi la ngome nachekacheka kuelekea ubalozi wa Cuba

huyo ndio popoma mkuu wa mapopoma kipenzi cha wengi jf na Adui wa wengi vilevile Kama kawa Kama dawa uzi utabamba
 
Mkuu unaonekana Wewe ni Mhudhuriaji mzuri na Mwaminifu sana kwa Waganga wa Kienyeji kwani hilo neno lako la ' Tawire ' nasikia ndiyo huwa si tu kwamba linatumika huko bali ndiyo Salamu yao tukuka.
Kwa hiyo mkuu kuna ubaya gani kutumia neno hilo kama ambavyo watumiaji wengine wanavyotoa maneno na kuyatumia ktk matumizi mengine ya kila siku! Lakini hapo umeelewa sidhani kama unaweza ukawa mzungu kwa kutumia lugha ama kuongea kizungu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nimekuwa nikiiona sana nchi za Marekani, Urusi, China, Korea Kaskazini, India, Afrika Kusini, Uganda na Rwanda ( ila kwa Tanzania bado sijaiona na nadhani pia haipo kwani Marais wetu wote huwa wanakubalika na wanaaminika sana na Wanajeshi wetu ) na imekuwa ikiniacha na Maswali mengi mno. Naomba wale ' Wajuvi ' wa haya mambo muweze Kunisaidia Kunielewesha tafadhali.

Nawasilisha.
Kea sababu ulimpenda.
 
Back
Top Bottom