Uchaguzi 2020 Kwanini Marais wanaoangalia maslahi ya nchi zao hawatakiwi na Marekani?

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,076
2,000
Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani na kuamua Tanzania iwe nchi inayojitegemea katika masuala yake za kiuchumi pamoja na kuleta mageuzi makubwa katika mikataba ya madini na uwindaji wanyama imekuwa kero kubwa kwa hawa wa Marekani.

Namkumbuka baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani kundi la maseneta waliwasili na kujaribu kuonana na Rais Magufuli lakini hawakufanikiwa.

Tumeona huko Venazuela na Bolivia jinsi serikali za nchi hizo zillizopata misukosuko baada ya kuvunja mikataba na makampuni za kinyonyaji za Marekani.

Watanzania tuache ushabiki wa kisiasa ni Rais Magufuli pekee ambaye atatuvusha watanzania kuelekea taifa lenye uchumi imara. Hawa wa Marekani wanapenda kukumbatia viongozi mafisadi.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,903
2,000
..Mabeberu wanapenda nchi zenye amani na viongozi walarushwa ili wazinyonye vizuri.

..Tanzania na Magufuli wanavyo vigezo nilivyovitaja hapo juu.

..Amani ikikosekana hapa Tanzania, makampuni ya madini kama Barrick hayataweza kuchimba madini.

..Pia kukiwa hakuna kiongozi fisadi kama Jiwe, Tanzania haitanunua midege tusiyoihitaji toka kwa mabeberu.

..Kwa hiyo Mabeberu kama Marekani wanapenda Tanzania iwe na amani, na zaidi iwe na kiongozi fisadi anayewapelekea mapesa ya bure kama Jiwe na miradi yake ya ununuzi wa midege[dreamliners] tusiyoihitaji.

cc Chige
 
wingatereza

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
1,294
2,000
Haiwezekani uminye uhuru na demokrasia watu wakuangalie tu.

Unafosi tulia na gambo wawe wabunge, ndo wananchi wanavyotaka? Nec na polisi wanavuruga uchaguzi halafu wananchi wakae kimya kisa nini

Sauti za wananchi zimefika ulaya ila kwa sasa bado sana 2025 ujinga huu ukiendelea tutalambishwa vikwazo hapo kipindupindu kitarudi na dawa hakuna
 
MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,535
2,000
Madikteta uchwara wa Afrika hupenda sana kutumia kisingizio cha kuangalia maslahi ya nchi na uzalendo kuwatendea udhalimu wananchi wao. Nchi ambazo zimeendelea ikiwa ni pamoja na Marekani ni watetezi wakubwa wa haki za binadamu, demokrasia na utawala unaozingatia haki na sheria. Sasa wewe dikteta ukifikiri bado tunaishi enzi za old stone age (na madikteta wengi hufikiri hivyo) utakuta dunia nzima inakusuta.

Kuna ubaya gani wa kulinda maslahi ya nchi yako (yaani ukawa mzalendo kweli kweli) na wakati huo huo ukawatendea haki (haki za msingi za kibinadamu) wananchi wako na ukazingatia utawala wa sheria ambao ni silaha muhimu kulinda maslahi hayo ya nchi? Ukiona mtu hafanyi haya, huyo ni dikiteta na ni halali yake kupingwa kadri iwezekanavyo ndani na nje ya nchi.
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,963
2,000
Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani na kuamua Tanzania iwe nchi inayojitegemea katika masuala yake za kiuchumi pamoja na kuleta mageuzi makubwa katika mikataba ya madini na uwindaji wanyama imekuwa kero kubwa kwa hawa wa Marekani.

Namkumbuka baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani kundi la maseneta waliwasili na kujaribu kuonana na Rais Magufuli lakini hawakufanikiwa.

Tumeona huko Venazuela na Bolivia jinsi serikali za nchi hizo zillizopata misukosuko baada ya kuvunja mikataba na makampuni za kinyonyaji za Marekani.

Watanzania tuache ushabiki wa kisiasa ni Rais Magufuli pekee ambaye atatuvusha watanzania kuelekea taifa lenye uchumi imara. Hawa wa Marekani wanapenda kukumbatia viongozi mafisadi.
Tatizo bado hujajua kuwa marais hao ni watu walioshiriki pia kuziibia nchi zao mpaka wakawa mabilionea. Wanatumia sheria kuwakandamiza watu wao wenyewe kisha kutafuta namna ya kubaki kwenye madaraka.

Hivi unajua kuwa Kwa sasa madini hayana bei kubwa kabisa. Tanzanite imeshuka bei sana.
Ni kwa nini kila kitu Tanzania hakina bei. Mazao yakivuka kwenda nchi jirani yanapanda bei lakini ndani hayana soko.
Tatizo ni mikakati mibaya inayolenga siasa badala ya uchumi.

Hivi kwani kujenga ukuta uhusiano gani na kuwateka watu au kumuacha Musiba ahamasishe mauaji nchini!!

Wazungu wanachokipigania ni kufuata sheria zilizowekwa kwa haki. Vinginevyo nchi itakua na wafanyabiashara Wachache sana wanaojipendekeza na walioficha Mali za watawala. Uchumi wa nchi sio lazima uwe wa kuwaumiza watu.
Kama Kenya kuna soko la Tanzanite kuliko Tanzania waruhusu watu wauze alimradi walipe kodi.
Mtu akipata pesa atazileta nchini, ataajiri watu ,atajenga,atanunua vifaa vya ujenzi ,ataongeza mzunguko wa pesa. Kuliko kuwaachia Wanajeshi wapore watu madini na kuyauza wao wakati hawana mgodi. Dhulma tupu.
Nchi haiwezi kuitwa nchi yenye mabalozi wakati inaendeshwa kijambazi. Dunia ina mambo mengi yanayopaswa kuwa na uhalali ndio maana hata ubaponunua ndege ina viwango vyake vya kimataifa ,wazungu wangekua wana Roho za akina Polepole, Musiba Bashiru na Kheri basi wangetuuzia ndege zisizo na kiwango kinachoweza kuhimili anga. Hata silaha na vyombo vya ulinzi wangetuuzia vinavyoweza kujilipua ili tuangamie lakini wanafuata kanuni za biashara za kimataifa na mikataba yake.
Sasa iweje wakae kimya sisi tunapoendesha mambo yetu kienyeji bila kufuata sheria za kimataifa ?
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
10,542

Mkuu hata sheria na taratibu tulizojiwekekea tunazivunja hasa pale mnufaika anapokuwa mwenye mamlaka.
Sasa hivi kuvunja sheria kwa kumnufaisha Magufuli/serekali/ CCM siyo kosa.
 
RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
957
1,000
Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani na kuamua Tanzania iwe nchi inayojitegemea katika masuala yake za kiuchumi pamoja na kuleta mageuzi makubwa katika mikataba ya madini na uwindaji wanyama imekuwa kero kubwa kwa hawa wa Marekani.

Namkumbuka baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani kundi la maseneta waliwasili na kujaribu kuonana na Rais Magufuli lakini hawakufanikiwa.

Tumeona huko Venazuela na Bolivia jinsi serikali za nchi hizo zillizopata misukosuko baada ya kuvunja mikataba na makampuni za kinyonyaji za Marekani.

Watanzania tuache ushabiki wa kisiasa ni Rais Magufuli pekee ambaye atatuvusha watanzania kuelekea taifa lenye uchumi imara. Hawa wa Marekani wanapenda kukumbatia viongozi mafisadi.
Kwa Tanzania ya Magufuli ujinga unalipa, si bure!
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
47,272
2,000
#ZEC mnaulizwa hawa Wapiga Kura yenu ya Mapema hapo tarehe 27/10/2020 mmewatoa wapi katika mitaa na vijiji vya #Zanzibar? Maana Raha ya #Zanzibar tunajuana kila mtaa na kijiji. Mliwaandikisha lini? Kama mmeamua kuuharibu huu Uchaguzi nyiye ndiyo mtakaowajibika kwa matokeo ya matendo yenu.

1603500110702.png
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,076
2,000
Wewe ni zuzu kibaraka wa Jiwe
Mtakumbuka CCM na Rais Magufuli kwani hata Kenya walimwita hayati Rais Moi Dictator. Walimwondoa kwa mbwembwe na kupata katiba mpya lakini leo wakenya wamekuwa masikini kuliko enzi ya utawala wa Rais Moi na Ufisadi umezidi kuwa mbaya sana. Tundu Lissu katika kampeni zake ameipa somo zuri sana CCM na nategemea CCM itafanyia kazi. President Magufuli still is the best for this country
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,076
2,000
Katika vitu wanavyo kosea Mabeberu na vibaraka wao ni kujaribu ku mtisha kwa namna yoyote JPM. Kumtishia JPM ni kupiga rangi upepo,JPM ni chuma Cha pua.
Hawa mabeberu ni wanafiki wakubwa sana
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,372
2,000
#ZEC mnaulizwa hawa Wapiga Kura yenu ya Mapema hapo tarehe 27/10/2020 mmewatoa wapi katika mitaa na vijiji vya #Zanzibar? Maana Raha ya #Zanzibar tunajuana kila mtaa na kijiji. Mliwaandikisha lini? Kama mmeamua kuuharibu huu Uchaguzi nyiye ndiyo mtakaowajibika kwa matokeo ya matendo yenu.

View attachment 1610078

Zanzibar kuna makabila ya bara siku hizi mengi hivyo? Maana naona chacha, tarimo, hollo etc etc
 
Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
601
1,000
Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani na kuamua Tanzania iwe nchi inayojitegemea katika masuala yake za kiuchumi pamoja na kuleta mageuzi makubwa katika mikataba ya madini na uwindaji wanyama imekuwa kero kubwa kwa hawa wa Marekani.

Namkumbuka baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani kundi la maseneta waliwasili na kujaribu kuonana na Rais Magufuli lakini hawakufanikiwa.

Tumeona huko Venazuela na Bolivia jinsi serikali za nchi hizo zillizopata misukosuko baada ya kuvunja mikataba na makampuni za kinyonyaji za Marekani.

Watanzania tuache ushabiki wa kisiasa ni Rais Magufuli pekee ambaye atatuvusha watanzania kuelekea taifa lenye uchumi imara. Hawa wa Marekani wanapenda kukumbatia viongozi mafisadi.
Uko sahihi kwa asilimia 100! Naweka mkazo pale unaposema Watanzania tuache ushabiki wa kisiasa kwani Marekani wanapenda kukumbatia viongozi mafisadi. Tumeona barua aliyoandika mwanasheria wa Lissu akimuonya JPM kwa maneno makali kama vile anamuonya mtoto wake.

Umetoa mifano ya Venezuela na Bolivia ambazo zilikuwa zikijitutumua kulinda uchumi wao. Vivyo hivyo hata kwa Iraq na Libya. Tukaambiwa viongozi wao ni madikteta. Tunajionea wenyewe 'demokrasia' iliyofuatia kuuawa kwa Saddam Hussein na Moamar Gaddafi. Watanzania tujifunze kutokana na historia hiyo.
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,304
2,000
Wazungu kwa ujumla wao hawampendi kiongozi mweusi mdadisi na mwenye kujiamini kwamba yeye ni tajiri na anayo haki ya maisha mazuri.

Mungu hawezi kukupa rasilimali alizotupa halafu tuendelee kuishi kwa kujikomba kwa mataifa mengine.
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,076
2,000
Uko sahihi kwa asilimia 100! Naweka mkazo pale unaposema Watanzania tuache ushabiki wa kisiasa kwani Marekani wanapenda kukumbatia viongozi mafisadi. Tumeona barua aliyoandika mwanasheria wa Lissu akimuonya JPM kwa maneno makali kama vile anamuonya mtoto wake. Umetoa mifano ya Venezuela na Bolivia ambazo zilikuwa zikijitutumua kulinda uchumi wao. Vivyo hivyo hata kwa Iraq na Libya. Tukaambiwa viongozi wao ni madikteta. Tunajionea wenyewe 'demokrasia' iliyofuatia kuuawa kwa Saddam Hussein na Moamar Gaddafi. Watanzania tujifunze kutokana na historia hiyo.
Hivi kweli watanzania leo tuone Tanzania ikiongozwa na mawaziri ya aina ya Hallima Mdee, Lema ama Heche. Dunia itatushangaa sana
 
ruhi

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
2,428
2,000
Ujinga umemjaa mtoa mada..kila siku case study ni yale madikteta ndo mnasema wanaonewa yaani duniani kuna nchi nne tu ndo wanaonewa na Amerika?

Jana usiku kuna kundi limeondoka Kimbiji kwenda kuvuruga uchaguzi wa Zanzibar then mkiambiwa mnasema mnaonewa. Ni ujinga imewajaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom