Kwanini Marais wa Kiafrika hawathaminiwi wakienda Nchi za Ulaya?

Leo Rais Wa JMT, Amewasili Nchini Marekani, kilichonisikitisha ni namna Alivyopokelewa, Amepokelewa As If Huku Kwetu Yeye ni Mwenyeketi wa Kijiji.

Hamna Mmarekani Anayejali kama Kuna Rais Wa Nchi Fulani Kaingia Nchini Kwao, Hata viongozi Wa Kiserikali Wa Marekani Nao Pia HawanaTime! Yaani Watanzania Wanaoishi Marekani Ndio walioJitokeza Kumpokea Rais Wa JMT.

Shida ni Nini? Ni sisi Ambao huwa Tunakuza Mapokezi Au Hawa Jamaa ni Wabaguzi? Haiwezekani Rais Akiwa anatoka Ulaya Akija Huku anapokelewa Na Rais Wa JMT tena Kwa Bashasha Lote na Wananchi Kibao na Ngoma Zinapigwa Airpot Hadi Ikulu kwa Msafara Mzitoo na Barabara zinafungwa, Lakini Rais Wetu Akienda Kwao Wanamuona As If Hamna Chochote inauma Sana.

Je, hii ni ishara ya ubaguzi? Kwanini Marais Wa Kiafrica hawathaminiwi wakienda nchi za Ulaya?
Nyerere alipokelewa kwa heshima sana na Kennedy,na kulikuwa na mwitiko mzuri sana kwa wamarekani.

Lakini leo hii hawa viongozi wa sasa wanajidhalilisha na kudharauliwa kwa matendo yao yaliyo kinyume na dunia ya wastaarabu eg. Wanatesa,kuua na kudharau raia wao,ni wezi na mafisadi pia,utawaheshimu kwa lipi sasa? Labda uwe mnafiki
 
Hivi kuna jamii duniani wa2wake wakalimu kama waarabu!!!! Tusemeni ukweli tu. Sema hujaishi nao ukawanote.
Wewe inaonekana ndio unaumwa ugonjwa mkuu wa washamba wa waarabu kila siku dada zako wanauliwa saudia huko, hapa walikua wanachukua watumwa
 
Ukitembelewa nyumbani kwako na kibaka mwizi wa kura, utampokea kwa red carpet au utaweka simu zako mbali na huo ugeni?

Asking for a friend.
 
Mathalani Rais wetu kipenzi mh. SSH amekwenda MAREKANI kwa ajili ya MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA-UNITED NATIONS GENERAL ASSEMBLY(UNGA) ambao huhudhuriwa na marais wengi sasa ulitaka AKAPOKELEWE NA mh.Rais Joe Biden?!!!Khaaa
Joe Biden ingebidi ahamishie ofisi (Ikulu) airport ili kuwapokea marais wa nchi zote.
 
Sasa wengine Ni kama wameenda kutalii tu. Kuna mipango gani hapo UN ya kuendeleza Nchi yetu. Kama mipango ya maendeleo tusipoipanga kupitia Bunge na Mabaraza ya madiwani tusitarajie hivyo vikao kuwa na lolote. Nionavyo mimi wengine wameenda kutalii na kufanya Shopping. Ujinga kama huu ndo aliukataa Magufuli.
Rais wa Zambia amekwenda na watu watatu tu, ukiondoa unit ya security yake ambayo nayo lazima ipunguzwe kwa safari kama hiyo.
 
Wewe inaonekana ndio unaumwa ugonjwa mkuu wa washamba wa waarabu kila siku dada zako wanauliwa saudia huko, hapa walikua wanachukua watumwa

Ulifuatilia hiyo ishu na chanzo chake ni nini kuuawa kwa housegirl!!!!

Swala la utumwa,, walikuwa wanachukuwa alafu wanawapeleka wapi???
 
Katafute bwana, Kila analofanya Samia mnakosoa, nyie misukule ya dikteta mna tabu Sana, mnataka mama aongoze Nchi Kama alivyokuwa yule majinuni wenu
Sasa wewe unadandia treni kwa mbele
Unakurupuka hata point yangu hjaelewa
Nani kamkosoa SSH
Nmewambiaaa jpm alipokuwa hasafiri mlikuwa mnalalamika
Huyu ana safari mnalalamika,hivi nyie wabongo
Mnataka nn,mnapigania nini???

Ova
 
Dah,sorry mkuu, nilijua Ni Hawa wasioisha kulaumu kila kitu, sorry Sana chief, Yaan watz siku zote wamekuwa watu wakulaumu kila kitu
 
Leo Rais Wa JMT, Amewasili Nchini Marekani, kilichonisikitisha ni namna Alivyopokelewa, Amepokelewa As If Huku Kwetu Yeye ni Mwenyeketi wa Kijiji.

Hamna Mmarekani Anayejali kama Kuna Rais Wa Nchi Fulani Kaingia Nchini Kwao, Hata viongozi Wa Kiserikali Wa Marekani Nao Pia HawanaTime! Yaani Watanzania Wanaoishi Marekani Ndio walioJitokeza Kumpokea Rais Wa JMT.
Je, hii ni ishara ya ubaguzi? Kwanini Marais Wa Kiafrica hawathaminiwi wakienda nchi za Ulaya?
Hapana, si ishara ya ubaguzi. Maana rais Samia (pamoja na marais wengine waliofika muda huohuo) hawakuja kutembelea Marekani. Walikuja kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa mwenye makao makuu mjini New York.
Kwa hiyo serikali ya Marekani hauhusiki. Marekani -ikiwa ni mwenyeji wa taasisi ya Umoja wa Mataifa- inapaswa kumkubali kiongozi yeyote ambaye ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo walipaswa kuvumilia hata viongozi kama Ahmadinejad wa Iran na wengine ambao kwa kawaida wasingeruhusiwa kuingia Marekani. Pamoja na viongozi marafiki, lakini wakija kwa Umoja wa Mataifa, basi si kazi ya serikali ya Marekani.
Hivyo ndivyo pia ziara ya Samia na kiongozi yeyote mwingine.
 
Back
Top Bottom