Kwanini marafiki wakubwa ndio uwa maadui wakubwa hasa wanawake...?

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
......Kwa wale wakristo wanafahamu kuna andiko kwenye Biblia linasema adui yako ni yule wa nyumbani mwako..Nilikuwa sielewi vyema msingi wa hili andiko..Lakini siku za karibuni nimeona wasichana wawili waliokuwa marafiki mpaka wakaanza kufanana kwa sura na hata kuvaa nguo sare sasa wamekuwa maadui kama paka na panya...na sababu ni za matatizo ambayo yanaweza kutatulika..ni kutofautiana kwa kauli dhidi yao..Nimejaribu kuwasuluhisha lakini wapi.Huu ni mfano mmoja lakini mara nyingi marafiki ndio wanajenga uadui kwanini? Nashindwa kuelewa sayansi iliyopo hapa..Maana nilitegemea kuwa marafiki ndio wanaweza kumaliza tofauti zao kirahisi kitu ambacho hakitokei kwa ulimwengu wa leo.
 
wanazuoni wakubwa waliwai kusema! Muogope rafiki yako mara 100 na muogope adui yako mara 1. Kwa sabau rafiki akigeuka anaweza kukuangamiza kirahisi kwa kua anakufaham sana na ana njia nyingi za kukuangamiza..adui anaweza kugeuka akawa ndo rafiki mkubwa..
 
1.Huwezi kugombana na mtu usiye intaract naye

2.they more someone gets in your inner cycle the more you become friends ......the more and more u enteract na kumegeana siri za ndani

3.in every reaction there is equal and opposite reaction........more kupatana ........more kugombana
 
Nadhani kwa hao inakuwa ngumu kupatana kwakuwa kilammoja anakuwa kichwa ngumu kumuomba mwenzake msamaha...
 
..yes its true watu wakiwa karibu zaidi ndio wanaweza kuathiriana. Ila kitu watu wengi hawajawahi kufikiri ni kwamba, wanalazimisha kuwa karibu na watu ilhali hawaamini kihivyo! au unakuta ni washindani toka wanaanza huo urafiki(friendenemies), wanaignore dalili ndogondogo zinazoonesha kutofautiana, hawagundui mapema kupungua kwa imani ya mmoja kwa mwingine.Wana 'confide to each outher blindly'. Sasa Collection ya hiyo mizigo ikikutana na kitu kiitwacho 'the last staw that broke the camels back' wanakuwa sworn enemies, hapo mtu yuko tayari kufa katika harakati za kumteketeza mwenzie...
 
Mi naona ni kwa sababu hawezi akatokea mtu asiyekufahamu na kuanza kukuchukia au kukufanyia kitu kibaya, lazima mtu huyo awe anakufahamu ndio haya mengine yatokee, mtu huyo anaweza kuwa rafiki yako wa karibu au hata ndugu yako, hii inaweza tokea sababu ya wivu tu wa kawaida au wa kimaendeleo au chuli tu juu ya kitu fulani....na hii haiwezi kuisha ilikuwepo na tutaiacha, cha muhimu tujitahidi kubadilika na kutendea wenzetu mema
 
Urafik iusio na kinga ya kudumu huja baada ya kuwa kuna kitu kinacho waweka , kitu hicho kikiondoka na Urafiki huo huishia hapo
Urafiki ambao utakuwa na neema na Baraka za Mungu ni mpaka Mungu mwenyewe autengue, Hapa Mungu ndie ameutengeneza urafiki kati ya Watu na ni Yeye anahusika na kuutegemeza

Kwa nguvu zetu na akili zetu Hatuwezi, Mungu atusaidie na kutushika katika yote
 
Back
Top Bottom