Kwanini mara nyingi undugu wa baba mmoja kwa mama mbalimbali huwa una nguvu zaidi kuliko undugu wa mama mmoja kwa baba mbalimbali?

Hii point.

Ukiwa na hela kila mtu atataka uwe ndugu yako kila mtu atajidai anakujua na mtu wake wa karibu.


Kwa kweli tuzitafute tu.
Hii mada hujaielewa bibie.
 
Mama mmoja baba tofauti wanapendana zaidi simply zoz akina mama wana kipawa cha kutengeneza mshikamano Team work/Team mate kuliko wababa ambao wako bize kusaka noti usiku na mchana.
Mama mmoja huwa ni ngumu sababu nasaba huwa inarudi kwa baba. Hapa ndipo nguvu ya undugu wa baba mmoja ilipo.
 
Kwangu mimi nipo kinyume na wewe, naona kwa mama kuna undugu mzuri kuliko kwa baba, kwasababu watu wengi wanakuwa sana na upendo kwa kina mama kuliko kina baba (baba zao ). Upande wa kina baba undugu wao sionagi kama una nguvu kwasababu wakina mama wengi huwa wanathamini sana familia yake (watoto wake) na kutoipa kipaumbele familia ya mama mwenzake (watoto) kwenye masuala flani flani yahusuyo familia.




mazingira nayo yanafanya kila kila mtu eje na jibu lake, ila ngoja tuangalie walio wengi ni wako wapi
 
Kwa sababu ndugu kwa Mama uhakika lakini kwa baba mashaka!

Ndiyo maana Waislael mwislael ni yule alozaliwa na Mama mwislael na siyo baba mwislael.

Wanataka uhakika na siyo mashaka!
 
Ndugu kwa mama wote mnakuwa mlilalia kitovu kimoja cha Mama pale kuna muunganiko wa ajabu hutokea wa kidugu na siyo ndugu kwa baba

Baba anaweza kuchomekewa lakini Mama siyo rahisi
 
Mama mmoja baba tofauti wanapendana zaidi simply zoz akina mama wana kipawa cha kutengeneza mshikamano Team work/Team mate kuliko wababa ambao wako bize kusaka noti usiku na mchana.

Ni hao hao wakina mama pia huwa na kipawa cha kuhakikisha ndugu hawapatani, mara nyingi wamama wakiwa peace hata watoto wanapatana ila kwa asili ya wengi ya kutaka kuwatumia watoto kwa bifu na wake wenzao au kumuadhibu mwanaume. Hiyo ndio shida

Watoto wa baba tofauti ni ngumu kutofautiana maana wanaume ni ngumu kufitinisha au kuzua ugomvi au matabaka yasiyo na msingi
 
Back
Top Bottom