Jumong S
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 7,312
- 10,492
...Katika taasisi imara na tajiri duniani ni kanisa Katoliki. Kanisa hili tajiri na linaloutumia utajiri wake kuifaidia jamii (sio wachungaji wake tu), ina wachungaji wasomi sana na wanasayansi wakubwa. Ndilo kanisa lenye wachungaji wasomi kuliko makanisa yote, mfano Mapadre huweza kusoma miaka mpaka 8-12 baada ya form six achilia mbali wanaoongeza specilizations mf utabibu, engineering, sheria nk.
Mapadre ni washauri wazuri wa mambo ya ndoa na hutoa mahubiri mazuri wakati wa ndoa. Hutumiwa sana ktk kuzijenga ndoa zinazotetereka (refer wimbo wa Baba Paroko).
Leo napenda kuuliza, maswali yafuatayo;
1. Kwa nini watawa na mapadre wake hawaruhusiwi kuoa?
2. Moja ya factor ya kuwa padre ni kuwa rijali (dume la mbegu), je, wachungaji hawa hufanikiwaje kujizuia dhidi ya hitaji muhimu (basic human need) la kujamiiana?
3. Kama ilivyo kwa mapadre, watawa nao hujidhibitije juu ya kujamiiana?
4. Nini adhabu ya mtawa/mchungaji anapokiuka kiapo chake cha useja? (celibacy)
5. Kwa nini wachungaji wake wasihasiwe ili kuzuia kuanguka ktk dhambi ya uzinzi?
6. Lini kifungo hiki kitakatwa ili mapdre waoe, au masista waolewe?
7. Unatoa maoni gani, watumishi hawa waruhusiwe ndoa kama walivyo watumishi wa makanisa mengine?
8. Unatoa maoni gani, je, jamii hii inauishi uharisia wa kiapo chao?
Nawakaribisha Maaskofu, monsinyori, mapadre, mashemasi, mafrateli, maburuda, watawa, makatekista, wanovisi, ministranti, makleri, waamini nk mje hapa jukwaani mtoe darasa mpaka hata mimi mkristo nisiye na kanisa nielewe vzr.
NB: Lengo la mada hii ni kujifunza na kukuza miito kwa vijana wanaotaka kujiunga na timu hii ya waseja!!
Sent using Jamii Forums mobile app