Kwanini maneno yasiyotamkwa mbele ya kadamnasi ya watu wameamua kuyaweka katika kamusi ya Kiswahili sanifu? What's the logic behind this?

Haya maneno si matusi. Ni majina ya sehemu za mwili wa binadamu. Ila nina imani unajua yakitumiwa vipi ndio huwa tusi.
 
Labda kwa kuanza kwanza tujue maana ya kamusi, kwa uelewa wangu mimi kamusi ni kama kitabu cha marejeo chenye misamiati iliyokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani na kupangwa kwa utaratibu maalum kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo msomaji anaweza kuelewa au tunaweza kusema ni kitabu cha tafsiri za maneno.

Ina maana kwamba lengo la kamusi sio kukufundisha wewe kipi ni kibaya cha kuongea na watu na kipi kizuri bali kukupa uelewa wa neno husika. Mfano mtu anakuambia kwamba wewe ni k**a na wewe labda huelewi maana ya neno k**a ni jukumu la kamusi kukudadavulia maana ya neno husika halafu wewe sasa ndo utaelewa kama ni tusi au sifa!!!
 
Mbona JIBU umeandika mwenyewe kwenye heading? UNAKWAMA WAPI dogo? Yaani maneno hayo hayafai kutamkwa mbele ya kadamnasi lakini yanatumika katika mazungumzo ya faragha. Kamusi imekusanya maana ya maneno yote ya Kiswahili yawe ni ya faragha au wazi kuyatumia ili kuweka utu na heshima wakati wa mazungumzo.

Ndio maana hayo maneno yenyeukakasi yana maneno/majina mbadala ya kutumika katika hadhara. Mfano : Sehemu za siri, haja kubwa, msalani, shoga, kujamiiana n.k .

Mfano ukiwa na dokta hospiltalini anaweza kuyatamka hayo maneno kwa minajili ya kutoa elimu ya ugonjwa. Au hayo maneno yanaweza kutumika kwa sababu maalumu kama shuleni kwa kujifunza sayansi ya mwili lakini si kwa mazungumzo ya kawaida.
 
Swali zuri sana baba lao. Ngoja wataalam wa lugha husika waje
Utafiti umefanyika Rais Magufuli atashinda kwa 98% Miaka mitano tu Rais Magufuli ametupeleka uchumi wa kati miaka mitano ijayo, Rais Magufuli atatufanya tuwe kama Qatar.
 
Hicho ulichokipresent hapa ni zao la unayoyawaza kichwani mwako.Nasi tuulize nini kilikupelekea uanze kutazama yasiyotamkika
 
Hebu wewe mwenyewe anza kwa kuyaweka hayo maneno matatu uliyopigia mstari kwenye heading ya uzi wako.
Nikiyaweka Mods watanipiga BAN na huu ndio msingi mkuu wa swali langu.

Kama ni maneno mabaya kwanini yatambulike kama Kiswahili safi? Mantiki yake ni ipi?
 
Ni kazi ya kamusi hasa. Hiyo kwamba utayatumia ama la ni juu ya watumiaji.
Miongoni mwa sifa muhimu ya lugha ni kukua, basi kila yanapokuja maneno mapya na kukubaliwa kimatumizi ktk jamii huwekwa rasmi pia katika KAMUSI.

Kamusi za Lugha ya Kiingereza zina baadhi ya maneno mengine yameandikwa katika mabano; (ancient, formal) ~a zamani, rasmi, n.k. hudhirisha namna wingi na mbadala wa maneno ulivyo ktk lugha. Sasa neno sehmu za siri wengine huita utupu, lakini jina rasmi ni uchi. Ila uungwana tu sawa na mahali ndio unaopelekea mtu kuweka tafsida nyiiiiiingi.

Pia tusi ni:
Tusi ni matumizi mabaya ya kauli au neno. Neno laweza kuwa tusi kwa mtu A na lisiwe tusi kwa mtu B kutegemeana na muktadha wa mazungumzo. Mimi ni mweusi lakini kuna mazingira ya kuzungumzia weusi wangu kutafanya lionekane ni tusi ama la!.

Sasa binadamu ukimuita k**a, mbwa, kima, moja kwa moja umemtukana.

Lakini binadamu mwenye sifa stahiki ya ushoga, usenge, upumbavu, n.k. ukimuita hivyo si tusi, Linakuwa TUSI kwa LISIYEMUHUSU k.m. rijali, kidume, mwerevu n.k.

Huo ndio muono wangu
 
Back
Top Bottom