Kwanini Mandela hakumsamehe mkewe Winnie?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,409
20,766
MA.jpg


Mama wa Taifa la Afrika Kusini Winnie Madikzela-Mandela amefariki dunia. Amefariki miaka minne tangu alipofariki Nelson Mandela na kuzikwa Desemba 15, 2013. Winnie atazikwa Jumamosi ya Aprili 14 kwa heshima zote kitaifa.

Katika kipindi hiki cha kuomboleza kifo chake wengi wanaimba sifa zake, ujasiri wake wa kupambana bila woga, kufukuzwa na kukamatwa na polisi wa makaburu, kuwekwa kizuizini, kufungwa kwake na kipekee alivyoendeleza mapambano wakati mumewe Nelson Mandela akiwa gerezani anatumikia kifungo cha maisha jela katika gereza la Robben Island.

Hata hivyo, wapo wanaodadisi na kuzungumzia maisha yake binafsi hasa mapenzi wakati Mandela akiwa gerezani na hata baada ya mpigania uhuru huyo kutoka jela mwaka 1990 akiwa ametumikia kifungo kwa miaka 27.

Hao ndio wanaeleza kwanini Mandela aliweza kuwasamehe watu wote waliomtenda vibaya – makaburu na polisi wao, lakini hakumsamehe Winnie Madikizela-Mandela. Ni kwa sababu katika neno NDOA waliondoa herufi ‘n’ wakabaki na neno ‘doa’ na kwa mtazamo wa Mandela, Winnie ndiye aliyetia doa.

Madoa ni mengi lakini la kwanza kubwa ni uhusika wa Winnie katika kifo cha kijana mmoja aliyetuhumiwa kuwa mpepelezi. Mei 1991 alipotiwa hatiani katika Mahakama ya Juu mjini Johannesburg kwa kumshambulia na kusaidia kumteka kijana mwenye umri wa miaka 14 aliyeitwa Stomple Moeketsi, uhusiano wake na Mandela ni kama ulikuwa umeingia doa.

Winnie aliaminishwa, kimakosa kama ilivyokuja kujulikana kwamba kijana huyo alikuwa anatumika kama mpelekaji wa habari zao kwa utawala wa makaburu. Wapambe wake walimkamata kijana huyo na baadaye aliuawa na dereva wake.

Siku hiyo Winnie na Mandela walitembea wote wakishuka kwenye ngazi za jengo hilo la mahakama. Kwa mara nyingine mwanamama huyo alipita mitaani akiwa amenyanyua juu ngumi ya mkono wa kulia katika hali ya ushindi.

Mandela alikuwa na fikra tofauti. Uso wake ulikuwa umekunjamana, macho yake akitazama chini.

Mambo yalipomzonga Mandela takriban mwaka mmoja baadaye aliamua kukata mzizi wa fitina. Aliwaita waandishi wa habari katika mkutano wa dharura kwenye makao makuu ya ANC. Mandela alijizungusha kwenye chumba kisha akakaa ili kusoma kipande cha barua. Alianza kwa kumshukuru mkewe Winnie.

Alisema; “Katika kipindi cha miongo miwili nilichokuwa katika gereza la Robben Island alikuwa nguzo imara ya msaada na faraja. Mapenzi yangu kwake yatabaki bila kupungua.”

Alivuta pumzi kwa nguvu halafu akaendelea: “Tumekubaliana kwamba uamuzi bora kwetu ni kutengana. Ninaachana na mke wangu bila lawama. Namkumbatia kwa huba na mapenzi kama nilivyokuwa najisikia nilipokuwa ndani na nje ya jela tangu nilipokutana naye”.

Halafu alisimama na kusema, “Mabibi na mabwana, natumai kwamba mtakubaliana nami kwa maumivu niliyokuwa nayo na huu ndiyo mwisho wa mahojiano”. Alitoka nje ya chumba cha mkutano akiwa ameinamisha kichwa katikati ya ukimya.

Mapenzi ya Mandela kwa Winnie yalikuwa machungu kwani hawajaishi pamoja kwa muda wa miaka 27 alipokuwa gerezani na muda waliokaa pamoja ni mfupi sana. Maisha ya siasa yalikula muda mwingi wa maisha ya ndoa kama Winnie binafsi alivyowahi kukiri.

“Sijawahi kuishi na Mandela,” alisema. “Sikuwahi kujua kile kinachoitwa kuwa karibu na familia ambapo unakaa kwenye meza moja wewe mume na watoto. Sina kumbukumbu nzuri kama hizo. Nilipojifungua watoto wangu wawili hakuwepo, japokuwa kwa wakati ule hakuwa jela.”

Winnie alikuwa na umri wa miaka 22 alipokutana na Mandela aliyekuwa na umri wa miaka 38 huku akiwa na amemuoa Evelyn wakiwa na watoto watatu na ambaye alijitolea maisha yake katika mapambano dhidi ya utawala wa kibaguzi.

Siku hiyo Winnie alikuwa amesimama kwenye kituo cha basi Soweto na akamwalika kwa ajili ya chakula cha mchana wiki iliyofuata.

“Siku iliyofuata nilipokea simu yake,” anakumbuka Winnie. “Alikuwa amezoea kunipitia kwenda kazini. Nelson, ambaye alikuwa mpenzi wa mazoezi ya viungo, mara atakwenda kwenye ukumbi wa mazoezi (gym). Nilikuwa nakwenda naye gym, kumtazama akitoka jasho! Hiyo ikawa sehemu ya maisha yangu. Wakati fulani nilikuwa namtazama. Kisha atatoweka kwenda kwenye vikao, ataniacha hosteli. Hata wakati huo, maisha na Mandela ilikuwa sawa na maisha bila Mandela.”

Baada ya kuachana na Evelyn, alimwoa Winnie mwaka 1958. Lakini punde alikwenda mafichoni, mwaka 1962 alikamatwa na kushtakiwa, akafungwa mwaka 1963. Gerezani alikaa miaka 27 akiwa ametengana na mkewe na watoto wawili na alipotembelewa na Winnie aliingizwa kwenye chumba ambako alitenganishwa na ukuta wa kioo.

Barua alizokuwa akiandika gerezani kwenda kwa Winnie zilionyesha mapenzi ya dhati na kwamba hakuna mwingine aliyemjua isipokuwa Winnie. Mapigo ya moyo yalimwenda mbio alipotazama picha za Winnie.

Ukweli ni kwamba Winnie alikuwa na wapenzi wengi kipindi ambacho Mandela alikuwa gerezani. Miezi kadhaa kabla ya Mandela kutolewa, alikuwa na uhusiano na Dali Mpofu, mwanasheria aliyetofautiana naye miaka 30 ambaye alikuwa katika timu ya wanasheria wa utetezi.

Aliendeleza uhusiano huo hata baada ya Mandela kutoka gerezani. Wanachama wa ANC waliokuwa karibu na Mandela waliufahamu mchezo huo kama ambavyo walijua matukio kadhaa ya ulevi wake.

Winnie alikuwa kituko ndani ya ANC katika kipindi cha miaka miwili baada ya Mandela kutoka gerezani. Kumfuata kumweleza ukweli huo ilifikiriwa kuwa hatua ya juu sana kwa wapigania uhuru hao wa ANC.

Lakini ulifika wakati ambapo Mandela au jamii isingeweza kujidanganya. Maelezo kuhusu mapenzi ya Winnie na Mpofu yaliwekwa hadharani, yaliandikwa kwenye gazeti moja wiki mbili kabla ya kutengana.

Barua hiyo ilikuwa mbaya sana, haikanushiki juu ya mapenzi ya Winnie. Ripoti ya gazeti ilihusu zaidi barua ambayo Winnie alimwandikia Mpofu ikifichua kwamba hivi karibuni alikuwa amezaa mtoto na mwanamke mmoja Mzungu mshenzi. Winnie alimshutumu Mpofu kwa hilo.

“...Kumbuka ni namna gani kila mara uliniumiza na kunidhalilisha. Naendelea kukueleza kwamba hali ya uhusiano inazidi kuzorota nyumbani, wewe hujali kwa sababu umeridhika mwenyewe na huyo mwanamke. Siwezi kuwa mpuuzi Dali”.

Si hivyo tu. Mandela alivumilia mateso ya unyumba kupita kiasi. Kisa kimoja kilichomuumiza sana kilihusu safari. Siku chache baada ya kesi yake, Winnie alikuwa amepata mwaliko wa kwenda Marekani kwa ajili ya shughuli za ANC. Alitaka kusafiri na Mpofu, lakini Mandela alimkatalia.

Winnie alikubali kutosafiri naye. Mandela alipompigia simu Winnie kwenye hoteli aliyokuwa amefikia New York, aliyepokea na kujibu alikuwa Mpofu ikiwa na maana alikuwa amesafiri naye. Katika uso wake, Mandela alikuwa mwanamume aliyefanyiwa uzinifu wa kutisha kuliko wowote.

Mandela anakaririwa akisema hakuwahi kumtarajia Winnie kuwa mseja wakati alipokuwa gerezani, lakini alimtaka awe msiri. Pia hakukubali kabisa aendeleze uhusiano na wapenzi wake wa nje baada ya yeye kuachiwa gerezani.


Chanzo: Mwananchi

 
View attachment 741508

Winnie alikubali kutosafiri naye. Mandela alipompigia simu Winnie kwenye hoteli aliyokuwa amefikia New York, aliyepokea na kujibu alikuwa Mpofu ikiwa na maana alikuwa amesafiri naye. Katika uso wake, Mandela alikuwa mwanamume aliyefanyiwa uzinifu wa kutisha kuliko wowote.


Chanzo: Mwananchi


Dah!
Hata hivyo jamaa alikua mwanaume hasa.
 
Tamaa za mwili zilimshinda Winnie. Mandela wote wawili wapumzike kwa Amani ,vita takatifu ya umkontho we sizwe waliipigana kwaushujaa wote wawii. Ukomboziujlipatikana ,private life ya mama yule haiwezi kumfanya dhalili kihistoria Na pia Madiba asingevumilia unyanyasaji aliokataa kwa makaburu aufanyiwe kwenye Taasisi ya ndoa. RIP Madiba and Winie.
 
Aliumizwa sana, Winnie ni mama lakini alikosea mzee kizembe hasa baada ya kutoka gerezani
 
Bado naona Mandela alikua na moyo wa tofauti.

Yani nijue mke wangu anatoka na mwanaume mwingine, hata siku haiishi atakua ameondoka mwenyewe nyumbani bila kuaga na jumla.

I can forgive an attempted murder on me from my woman but not cheating.
 
Lakini Winnie si inadaiwa alianza kuvua picchu kwa vijana tangu Mumewe yuko lupango au?

Pamoja na kukaa jela miaka 27 mzee aliharibiwa na wazungu samahani lakini jogoo hakuweza kupanda mtungi tena. Walimtesa wakitaka kujua nani anafadhili ANC
Kuoa mwanamke mzuri kuna gharama yake.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom