Kwanini Makonda anapenda kutumia vyombo vya habari binafsi?

masare

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,719
1,782
Najiuliza tu hivi inakuaje RC Paul Makonda anapenda kutumia vyombo vya habari binafsi kwenye shughuli zake za kiserikali..!

Tukio la yeye kutimiza mwaka mmoja tangu awe Mkuu wa Mkoa wa DarEsSalaam leo limerushwa mubashara kupitia Azam Tv pamoja na 107.3 Ufm.

Hivi ni vituo vya kibiashara na ni dhahiri kodi za watanzania zimeteketea kwenye kulipia matangazo hayo.

Halmashauri ya jiji la DarEsSalaam inamiliki radio yake 91.7 City fm.Swali kuu Je ni kwanini Makonda asiitumie na badala yake anapenda kutumia vituo vingine vya radio binafsi.

Je tuamini huko ndipo kujitafutia umaarufu wa kisiasa japo alikanusha jana..!

Au naye ameamua kufuata staili ya Mkulu ya kuikwepa Tbc na kuipenda Clouds..!

Tujadili
 
Ndio hapo sasa hao Azam TV,Clouds TV,Ufm kurusha matangazo mubashara si wanalipwa hela nyingi tu ambazo ni za walipa kodi wa Tanzania.

Niliwahi kusikia Star TV kwamfano wao matangazo ya live kwa masaa mawili tu wanafanya full coverage ni Tsh milioni 64
 
Hopeless idea

Ila umeelewa..sio lazima kwenda Tbc au city Fm,hivi vyombo ni vya serikali so wanalipwa na serikali....cloudz na others private media wanakula kwa kupitia watu kama makonda na Dr.Ndodi....ndo mana nikasema niliyoyasema hapo juu...kama hutaki nenda ww tbc au city fm ukaongee ujinga wako na uwalipe.
 
Back
Top Bottom