Kwanini makamo wa rais atoke zanzibar? Sioni mantiki yake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini makamo wa rais atoke zanzibar? Sioni mantiki yake!

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Ngekewa, Mar 30, 2011.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wanajamii Forums hapo juu nawakilisha swali langu na pia kueleza mtizamo wangu juu ya jambo hili. Naomba mchango wenu lakini naomba tuchangie kwa hoja za kujenga!
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hili limo kwenye KATIBA ya JMT.
   
 3. R

  Rangi 2 Senior Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tayari wanaye rais wa SMZ!!
   
 4. m

  mob JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  ni kwamba katiba inasema ikiwa rais atatoka bora makamu atoke zanzibar virse versa
   
 5. D

  Deo bony Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fact ni kwamba ktk united republic state yoyote presda anapotoka side flani side nyingine inabidi atoke makamu ili kuensure muungano kwani kwakutofanya hivyo side mojawapo inaweza kujiengua kwa kile kinachoelezwa kuwa kutothaminiwa.
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wenzangu najua kuwa Katiba inasema hivyo lakini jee waliotia hili kwenye Katiba walikusudia liwe na maana gani katika Muungano wetu?
   
 7. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Takribani Wzanzibar wengi kama mimi wana mawazo kama hayo yako, kwanza huyu sio makamo wa Raisi ktk sheria ya katiba ya Muungano, Kisheria Raisi wa Zanzibar ndio makamo wa Raisi na huchaguliwa na Wzanzibar wenyewe sio huyu alopendekezwa na chama.a.) b.)nikuwa huo Muungano wenyewe haupo tena between Tanganyika na Zanzibar hivi sasa kuna mazowea tu.
  Muungano umekufa baada ya kufa tu kwa Tanganyika na katiba ya Tanganyika, sasa hivi tunaishi kutokana na Mazowea ya kuwa tuliungana na ikifa ccm ndio sizani kuwa Muungano utakuwepo Zanzibar.
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  sijakuelewa ..... haa haaaaaaaa
   
 9. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Iwapo huyo Makamo anatoka zanzibar inakuwaje anashughulikia mambo ya Tanganyika? Na kama ulivyosema alipata wapi ridhaa ya Wazanzibari kuwawakilisha?
   
 10. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kasome katiba.
   
 11. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sijakataa kuwa hilo jambo limo ndani ya Katiba. Nionavyo mimi hao walioandika kipengele hichi Katiba walilifanyia uchunguzi suwala hili? Huu ulikuwa ni uamuzi wa papo kwa papo wa CCM waliokuwa wakifikiri kuwa hii nchi ni yao peke yao. Sioni mantiki ya kuwepo Makamo wa Rais iwapo Rais anatoka Bara. Tuchukulie mfano wa DR Gharib Bilali hivi sasa yuko kumsaidia Kikwete kwa upande gani, Tanganyika au Zanzibar. Zanzibar kuna Rais wake na ndie mwenye mamlaka ya serikali ya Zanzibar na hata siku moja kwa kipindi cha miaka zaidi ya 15 toka uanze utaratibu huu, Makamo wa Rais hajawahi kushughulikia mambo ya Zanzibar.
  Nimekuwa nikijiuliza kati ya Makamo wa Rais na Rais wa Zanzibar nani ana mamlaka makubwa na nikijiuliza sana kwanini Makamo wa Rais wa Tanzania anaacha kazi ya umakamo na kuwa Rais wa Zanzibar.
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Hii katiba iliyopo haikufuata utaratibu ule uliokubaliwa na waasisi wa Muungano.

  Imekuwa ikibadilishwa na CCM kiaina aina tu, kutokana na political calculations zao.
  Bora inawasaidia kubakia katika madaraka.

  Sijui lini "watanzania" tutatambua kuwa hii katiba ni bomu tu linalosubiri kutupasukia na kutumaliza.
  Vizuri kabla ya Katiba mpya, yatangulie majadiliano ya Muungano wenyewe kwanza.

  Mimi ningependa sana iandikwe katiba mpya kwa ajili ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Si lazima kuwa na katiba kwa muungano. makubaliano tu ambayo yako elaborative yanatosha.
  La msingi na muhimu ni kuwa na katiba ya Tanganyika na Zanzibari wawe na Katiba yao.

  Inapokuja Urais wa Serikali ya Muungano.Iwe ni kwa kubadilishana.Kipindi kimoja Rais kutoka Tannganyika na makamo kutoka Zanzibar na kinyume chake inapofika muhula mwengine.
  Hii inaweza kuwa miaka miwili, miwili.
  Kuwe na bunge dogo la Muungano.EAC style.

  Au iwe Urais uwe katika mikono na marais wawili kwa pamoja. Yaani rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar kwa pamoja wawe ndio Taasisi ya Urais wa Muungano.

  Kwa hivi ilivyo leo katiba iliyopo ,mimi naona hakuna mantiki wala seriousness juu ya Muungano.
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kinachonishangaza ni kuwa mwanzilishi mmoja wa Muungano (Nyerere) alipigia sana debe mfumo huu tata.

  Najiuliza itokee siku CUF washinde Zanzibar na CHADEMA washinde Tanganyika (au CUF Zanzibar na CCM Tanganyika) tutakuwa na mkorogo gani?
   
 14. Wed

  Wed JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Swali zuri.... na bado halijajibiwa. Jibu halisi ni refu kidogo. Kwa sasa nilipita tu kuchungulia kulikoni. Nivumilie Mkuu Nitarudi baadaye kukupa jibu.
   
 15. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kinachotusumbua ni huu urafiki wa chako chetu na changu changu.
  Kwa kuwa Serikali ya Tanganyika haipo, na kama ipo haina Rais, haina Waziri mkuu wala makamu wa Rais, nasema hivi kwa sababu viongozi hawa wakuu ni wa Muungano. Kama tunajiaminisha kuwa serikali ya Muungano ndo ya Tanganyika, Je nani anaiwakilisha Tanganyika kwenye Serikali ya Zanzibar iwapo tunajua Raisi wa Zanzibar ni mjumbe wa Baraza la mawaziri Muungano, na makamu wa Rais anawakilisha Zanzibar?
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Huu mkorogo utapungua kama tutairejesha serikali ya Tanganyika.
  kama tunakubali au tumetambua sasa kuwa serikali ya Tanganyika haipo basi la kufanya ni kuirejesha serikali ya Tanganyika.
  Tatizo litakuwa limetatuka au vipi?
  Hakutakuwa na umuhimu wa Tanganyika kuwakilishwa katika serikali ya Zanzibar wala Zanzibar kuwakilishwa kwenye serikali ya Tanganyika.

  Uwakilishi wa Tanganyika na uwakilishi wa Zanzibar utahusu kwenye serikali ya Muungano pekee.

  Kwa nini Watanzania tunapenda kufanya mambo kuwa magumu na mkorogo wakati hata mtoto wa darasa la pili anajua utatuzi wa mkorogo wenyewe?

  Hivi wajemeni, kwa nini hatuzungumzii kuirejesha serikali ya Tanganyika?
  Au sote tumekuwa CCM? Tunataka kutekeleza sera ya kutoka serikali mbili kuelekea moja?
  Mtumiabusara ni wakati wa kutumia busara!

  Sioni mantiki ya kutaka aliyenacho apoteze alichonacho lakini busara ingesema kuwa asiye nacho basi afanye juhudi naye apate!
  Tuache unafiki wakuu! Hapa hapana tatizo kubwa, tatizo ni sisi wenyewe hatutaki kudai Tanganyika na serikali ya Tanganyika ambayo haipo wazi wazi.
  This leaves me wonder what a game is this? Badala ya sisi kulilia serikali yetu irudi, tunapiga mayowe wao waue serikali yao!!

  Are we still sane?
  Who brain-washed us?
   
 17. T

  Tom JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2011
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pia sawa na kusema Fact ni kwamba katika United Republic state yeyote presda anapotoka CATHOLIC inabidi Makamu atoke ISLAM, ama anapokua mwanamke makamo awe mwanaume, nk. Lakini hali halisi inatuonyesha kua duniani kote daima mnyonge humezwa na mwenye nguvu kiuchumi. Mradi JWTZ ipo, kazi yake ni kuulinda huo muungano kwa hali yeyote mpaka damu ya mwisho ndo muungano waweza enguliwa. Muungano ni nguvu, vema Zanzibar ukawa tu mkoa ili RAISI NA MAKAMU WAKE watoke sehemu yeyote ya TZ.
   
 18. C

  Chaldmhola Member

  #18
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuna udhaifu mkubwa katika Katiba, kwani hata Rais wa Muungano hana uwezo hata wa kuteua wala kumwajibisha kiongozi wa ngazi yoyote Zanzibar. Kimsingi Makamu wa Rais hana shughuli za kufanya kikatiba, bali hupangiwa na Rais. Na kwa kuwa SMZ iko juu ya Muungano kwa maswala ya Zanzibar, basi Makamu wa Rais analazimika kumsaidia Rais shughuli za Tanganyika.
   
 19. M

  Matawana JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 630
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Jambo moja lililowazi ni kuwa muungano ulivyo sasa haukubaliki kwa pande zote. Njia pekee ni kwa kila upande kuwa na katiba yake na utawala wake, halafu tuungane kupitia nchi za africa masharika, i.e Zenji na TZ zote ziingie kama nchi kamili. Kama kutakuwepo na special relantionship kati ya Zenji na TZ basi iwe kwa sababu ya ukaribu wa watu wa pande zote mbili na si kulazimishwa na chombo chochote:mmph:
   
 20. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nimegundua ndo maana mtikila anapeperusha bendera ya Tanganyika kwenye gari lake. Haya ni magumu kuyajadili kabla hujaitwa mchochezi
   
Loading...