Kwanini makada wa CCM wameumia sana Chadema kususia uchaguzi kuliko wafuasi wa Chadema wenyewe?

kusini kuna CCM,kasikazini kuna NEC,mashariki kuna polisi!!halafu bwege (CDM)yupo katikati ndio anatafuta mpira akiupata mala polisi ana mwambia ni foul umetumia double karachi!!rudisha mpira kwa ccm!!akiupata tena NEC,anakuja na kusema a tena ni foul umeiunua miguu hukuwa na nia nzuri'!!sasa bwege amejitoa mpira hauchezeki tena!!!
Hii hahaha
 
Acha unafki dogo. Hata wewe unazitamani izo nafasi za ubunge na udiwani ndomaana umejitoa ufahamu na kushinda humu jf ukipayuka kusubiri uteuzi.
Kwahio anae support CCM anataka nafasi za ubunge na udiwani ila wanaopinga hawazitaki basi endeleeni kupinga maana hizo nafasi mshaziona sio kwa ajili yenu
 
Bora wizi wa kura uendelee kama Mbowe ataendelea kukifanya chama kuwa cha kikabila na kifamilia.

Hakuna Mtanzania atakaye ipigania Chadema inayoongozwa na Dikteta Mbowe , eti kwa sababu ya kutetea demokrasia.
Hayupo mtanzania kama huyohuyo ,bora tu tuendelee na udikteta wa CCM kuliko huu wa Mbowe anayetumia udikteta wake kulazimisha wabunge na viongozi wa Chadema kupinga maendeleo ya nchi.
Bora CCM wanaotumia udikteta kuleta maendeleo.

Chadema haina intelijensia ya Kisiasa.
Ndio maana CCM inapanga njama kushirikiana na watu ndani ya Chadema lakini hawajui.
Kama Chama cha Mbowe Kingekua na itelijensia nzuri Hakika kisingethubutu kumsauri Mbowe aendelee kukalia kiti hata kwa dakika moja mbele. Mbowe hakubaliki kabisa kwa wanachadema wa makabila mengine nje ya wale wachache sana wa kabila lake. Watanzania wengi wamechoka siasa za Mbowe.

Chini ya Mbowe 2020 itafika bila tume huru na hakuna mpinzani atarudi Bungeni
Aliyesoma anipe summary jaman
 
Ukiona unapigwa vita sana hasa na mahasimu wako wa Ccm basi ujue unakubalika kwa 100% na Mbowe kwa sasa ni mwiba kwa ccm, kwanini Ccm msimpigie kelele Lipumba,Mbatia, John Cheyo na wengine ? Hii ni kwa sababu Mbowe ni strong powerful leader pia hanunuliki kwa bei yoyote ndo maana mnaweweseka.
Ndo ukweli huo hata ukicheki chadema siyo chama pinzani pekee lakin ukisema upinzani akili ya maccm inawazaga chadema tu wamemsahau hata zito sahiv
 
Lazima tukubaliane kwamba kuongoza taasisi kubwa ya kisiasa kubwa kama CHADEMA Ambayo ina viongozi nchi nzima, chama kikuu cha upinzani ni kazi nzito sana. Hili lipo wazi. Viongozi wetu lazima Wapewe pongezi.

Concern yangu kubwa ni baada ya sasa. Tumeachana na chaguzi 36 za udiwani na jimbo la Liwale. Ni uamuzi sahihi, lakini baada ya hapo nini kinafuata? Tuendelee kusubiri huruma ya JIWE kuelekea chaguzi za TAMISEMI 2019 na uchaguzi mkuu 2020?

Nimesikia kauli ya chama kupitia kwa mwenyekiti, akisema kwamba kurejea nyuma au ku' surrender, ni kujipanga na mbinu mpya za kivita. Hii ni sawa, natarajia kuona namna ya kuipata sheria mpya ya uchaguzi, muundo mpya wa tume ya Taifa ya uchaguzi, hii inashurutishwa, sio ombi. Jiwe ni 'rigid' lazima alazimishwe.

Hatuwezi kususia chaguzi hizi za marejeo kwa sababu hizi zilizotolewa na baadae tukashiriki chaguzi zingine chini ya tume hii ambayo leo tunaukataa muundo wake. Kususia kuendane na 'total retaliation' itakuwa sawa. Tusubiri maamuzi ya baadae.

Kuna watu wanachanganya hizi masuala. Haya sio maamuzi ya Freeman Mbowe sio maamuzi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Ni maamuzi rasmi ya kamati kuu ya CHADEMA Ambayo inafanya kazi na majukumu yake kwa niaba ya mkutano mkuu wa CHADEMA Taifa. Hayo ni maamuzi ya wana CHADEMA.

Ingawa sio kosa, sio jinai kwa mwanachama kufikiri tofauti na maamuzi hayo. Kwa sababu, wanachama wote sio wajumbe wa kamati kuu, sio wenye kubeba maamuzi hayo. Hivyo anaweza kufikiri tofauti, na kutoa maoni yake kinzani, asionekane ni 'mkosefu' huu ndio ukomavu wa kitaasisi. 'Floatation of thinking'

Kushiriki hizi chaguzi kumerejesha nyuma sana morali ya wapiga kura, wanapiga kura, wanachagua maamuzi yao hayana umuhimu. Wameamua kuacha kupiga kura. Ingawa hii ni platform iliyotumika kuwafikia wanachama kwa nguvu na kuwaeleza mwenendo wa siasa za nchi yetu sasa.

CCM wanaweza kuwa wanaumizwa na maamuzi haya, lakini bado wanayo nafasi ya kushangilia. Tumewapa wenyewe. Labda kutokana na kuchelewa sana kufukia maamuzi haya. Labda kutokana na kufanya siasa za kulaani, kukemea na kulalamika. Wametuzoea.

Biashara ya kununua watu na Kuunga juhudi za JIWE mkono haitokuwepo tena baada ya uchaguzi wa Liwale na kata hizo. sio kwa sababu CCM wamefanikiwa malengo yao, hapana. Kwanini?

Biashara hii inakufa 'manual deary death' kwa sababu ya muda umekwisha wa kufanya chaguzi za marejeo umekwisha kisheria, hakuna chaguzi zingine zitafanyika. Hivyo hakuna biashara ya UTUMWA itafanyika baada ya sasa.

Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi hakutakuwa na uchaguzi mdogo baada ya miaka 3 (tangu kufanyika uchaguzi mkuu) hivyo ambaye hajafanikiwa kupelekwa UTUMWANI imekula kwake hadi sasa. Wavumilie. Biashara hii hadi baada ya 2020 ndio itakuwa 'resumed'

Pia, kuna masuala by defaults hayazuiliki. Diwani au mbunge ni haki yake kikatiba kujiuzulu na kuhamia chama kingine cha siasa, Diwani au mbunge kuhongwa Pesa na kununuliwa sip kosa la CHADEMA, Sio kosa la mwenyekiti, hili ni kosa la kikatiba, kosa la sheria ya uchaguzi na kosa la sheria ya vyama vya siasa na Kanuni zake za maadili. Zitengenezwe upya kunusuru hizi gharama.

Lakini kwa upande wa pili, ni muhimu utaratibu wa tathmini ufanyike, wabunge na madiwani na viongozi wa chama wapimwe, wafanyiwe tafiti kabla na baada ya kupewa nafasi ya kuchukua fomu za kuomba uongozi ndani ya chama. Muhimu vetting and sorting kufanyika. Kupunguza watu ambao hawana shibe ya falsafa na itikadi ya CHADEMA.

Tuendelee kuwapokea wanachama wapya! Tusiache! Chama ni wanachama, lakini ni muhimu kutoa muda, kuwapima nyendo na Tabia zao, kubaini uimara wao kabla ya kuwapa vitengo na nyadhifa ndani ya chama. Tuwaheshimu Wageni lakini tuwape tahadhari, tuishi nao kwa Makini. Wametuumiza sana.

Hoja ya Mwenyekiti, Freeman Mbowe kujiuzulu ni 'hoja mufilisi' nafikiri hatupaswi kuijadili sana, mkutano mkuu ndio wenye mamlaka ya kuchagua nani anapaswa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA sio mtu mwingine, sio CCM, only mkutano mkuu. Freeman, Chapa kazi Le' Field Marshal!

Kwenu CCM. na wengine wenye kutaka Mbowe aondoke, you must now deal with that kwamba ikimpendeza Freeman, achukue fomu, asipochukua tutamchukulia na kujaza particulars zake (tunazifahamu) aendelee kuwapa taabu. Andaeni 'ndimu na chumvi' maana mtatema mate sana. Labda akatae mwenyewe kuwa mwenyekiti tena.

UNASEMA Mbowe ni dhaifu, halafu unampa kesi za mauaji, uchochezi, UASI.. Mbowe dhaifu unamtupia risasi afe, Mbowe dhaifu unamtunza mahabusu siku 14, Mbowe Dhaifu unaharibu mali na biashara zake. Sasa huyo Mbowe angelikuwa Imara si-mngeliomba msaada NATO brazazi and sistazii..

Anyways.. We shall overcome. Transition period. MSICHOKE.. What doesn't kill you, always makes you stronger. In winter, we must protect one another, keep each other warm, share our strength: When everything is moving and shifting, the only way to counteract chaos is stillness.. Jah Bless..

#MMM, Martin Maranja Masese
Tuko pamoja mapambano daima. Hii ngoma haifiki mwisho ati
 
hoja imepita bila kupingwa!
Kwa kweli ni aibu ya karne kwa vyombo vya dola kwenye nchi yoyote ya kidemokrasia kusherehekea hadharani ushindi wa chama kimojawapo cha siasa kwenye uchaguzi.
 
Tatizo ni kumwita mtu ulingoni halafu anafungwa mikono yote,ndipo ngumi zinaanza,lazima aliyefungwa mikono apigwe vibaya halafu jamaa anasema yeye ni mshindi kwakuwa anazijuwa ngumi.Sasa hayupo wa kufungwa mikono,mashabiki wanaweweseka.
 
Back
Top Bottom