Kwanini Majeshi ya nchi za Afrika hukaa tayari nyakati za uchaguzi kama vile vita inaanza?

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,305
15,033
Mzee Kalinga alijaribu Kumuuliza hilo swali Mzee Sanga wakati akiwa anatafuna mkate wa kikinga na maziwa fresh ili apate nguvu kuendelea na safari yake ya ukinga milimani.

Mzee sanga akamweleza kwanza sababu kubwa chaguzi za Afrika akatania kidogo hata Tanzania ipo hua haziko huru na haki na majeshi na vikosi vyake hua vinawalinda watawala na kujiandaa kupora uchaguzi na hasa kufanya unyang’anyi wa maamuzi halali ya wananchi.

Mzee Kalinga akaguna akasema inawezekana hata hapa kwetu kweli ujanja huo hufanyika?

Mzee Sanga akamweleza Mtanzania kwa mfano akisikia tu mlio wa risasi anaanza kujikojolea pale alipo hasa huyu mtu akiona mazoezi ya kijeshi ongeza na vifaru unadhani hata kuchagua kwenyewe ataenda tena?

Basi mzee kalinga akaona hiyo hoja ya mzee sanga inaukweli maana huwezi kukaa standby kwa mtu ambae hata kisu wala panga hana na hana mafunzo yoyote ya kijeshi zaidi unakua unamtishia amani tu ndio maana chaguzi nyingi Afrika hata wawekezaji huondoka kwanza kupisha lolote litakalotokea akatolea mfano huko kenya mambo yalivo wawekezaji watawapisha kwanza na kuhamisha mitaji yao kwa muda.

Basi wakaendelea kusema nchi zilizoendelea hua chaguzi zao ni huru na haki anaeshinda hutangazwa na anaeshindwa anakubali matokeo maisha yanaendelea na malumbano ya wanasiasa wanaachiwa wao wenyewe wala hutosikia polisi au jeshi kutisha wanasiasa.

MZEE KALINGA NA MZEE SANGA SAFARI YAO LEO BADO INAENDELEA NGOJA TUSIKILIZIE KAMA KUNA JINGINE WATAKALOJADILI.ZAIDI TUWATAKIE SAFARI NJEMA WAFIKE SALAMA HUKO UKINGA.
 
Back
Top Bottom