Kwanini maiti nyingi za watu maarufu zinahifadhiwa Lugalo?

Usilolijua uliza kwanza uambiwe. Usiaminishe watu ujinga. Ulichoongea ni uongo mtupu. Lugalo hospital ni ya jeshi lakini wafanyakazi hata raia wapo tena Specialties. Nenda idara ya macho, nenda ECG, nenda X-ray zipo nyingi tu. Kwa maono yangu na ilivyo ni hivi:
Sehemu yeyote duniani ukianzia USA, UK , Russia nk. Hospitali za jeshi ndizo zinakuwa the last resort... For everything na kikubwa ni usalama (security) hata leo Rais akafariki atapelekwa Lugalo. Lugalo ilitakiwa kuwa na hadhi zaidi ya muhimbili ama kuwa sawa Lakini inakuwa zaidi kwa issue ya Security.

Umetumia vyema kabisa kiungo chako cha ubongo kuweka mambo sawa, Hakuna kitu kikubwa,zaidi ya Security tu,
 
Ushawahi kwenda Ofisi zozote za Jeshi la polisi ukakuta raia wa kawaida??? Jeshi lina miiko na sheria zake huwezi ajiriwa tu bila kupata japo mafunzo kidogoo Never neverr...
Acha ubishi usio na tija.. Hapo Lugalo wapo Dr's na watumishi wa afya wasio wanajeshi. Wengine nawafahamu binafsi
 
Inasikitisha kuona hakuna anayejua..

Ila kwa uchache tu, maiti zote zinazotoka nje lazima ziende Lugalo sababu ndio wana special facilities za kuvunja yale machuma yanayoseal jeneza. Mjue tu jeneza linakuwa sealed na vyuma chochote kutoka kwenye jeneza kisilick na kuchafua mizigo mingine.

Hivyo yeyote anayesafirishwa kutoka nje kwa ndege lazima aende Lugalo..
Kumbe Godzillah nae alifia Ulaya eeh,,,Na Ngwair mbona hakupelekwa Lugalo??
 
Dogo wacha uongo hujui taratibu za mapot.raia lugalo wapo km kawaida.
Ushawahi kwenda Ofisi zozote za Jeshi la polisi ukakuta raia wa kawaida??? Jeshi lina miiko na sheria zake huwezi ajiriwa tu bila kupata japo mafunzo kidogoo Never neverr...
 
Inasikitisha kuona hakuna anayejua..

Ila kwa uchache tu, maiti zote zinazotoka nje lazima ziende Lugalo sababu ndio wana special facilities za kuvunja yale machuma yanayoseal jeneza. Mjue tu jeneza linakuwa sealed na vyuma chochote kutoka kwenye jeneza kisilick na kuchafua mizigo mingine.

Hivyo yeyote anayesafirishwa kutoka nje kwa ndege lazima aende Lugalo..
Bro..Kwa maiti zinazotoka nje, kuna sababu nyingine ya kupeleka Lugalo zaidi ya hiyo ya kuondoa seal?..
 
Lugalo ndio sehemu ambapo maiti hupelekwa kwa ajili ya uchunguzi wa kina.............watu ambao wameuawa kwa "mipango" ya serikali hupelekwa na hata watu maarufu wanaosaidikiwa kuuwa,ndugu wanaweza kuomba wapelekwe Lugalo ama serikali ikashawishi wapelekwe kule.
Kwa nini Lugalo?
Kule wafanyakazi wote wa afya sio raia ni wanajeshi.....sasa ile hali ya kutunza privacy....."kufunika mambo"kama kifo kilipangwa na wenyewe serikali e.g Amina Chifupa death,hufanikishwa.....au hata Kama ameuawa ki kawaida ila ni mtu maarufu,usiri unakuwepo kwa kiwango kikubwa.......kumbuka matabibu wengi wanaohusika na huduma hizo ni cardet officers na wengi kuanzia ngazi ya "captain" ,kulingana na mafunzo na viapo vyao ni ngumu kutoa Siri/kuzungumza chochote kuhusiana na uchunguzi............kumbuka hata waandishi wa habari hawana haki ya kudemand habari za jeshi labda waitwe .......tofauti na hospitali za umma.
Wapo Raia wanafanyakazi kwenye hospitali ya jeshi
 
Kwa Kiingereza, msiba ni burial ceremony, pia kuna wedding ceremony.

Ceremony yeyote hufana kulingana na kipato cha mtu.

Kama huna hela kabisa, ukifa leo, unakamuliwa utumbo ili uzioze then unapakwa chumvi, unazikwa kesho.

Kama una hela kidogo napelekwa mochwari kituo cha afya cha karibu na utakaa siku moja.

Kama ni tajiri type ya Mengi, na au una wafuasi wengi, basi mwili wako utapelekwa sehemu ya gharama na utakuwepo kwa siku wanazoona zinafaa, na utasindikizwa na magari na hata ving'ora.

The same, ukiugua, kama huna hela kabisa unakufa, labda Mungu akuhurumie.

Umasikini wako ndiyo utaamua utibiwe wapi, na ukifa mazishi yako yawe vipi.

Wewe kama hela huna, yaani umeugua, watu tunaangalia pesa chini ya godoro lako tunakosa hata buku ya boda, yaani huu ni usumbufu maana tuanze kuchangishana.

Michango kama hamna, basi Mungu atakushika.

Pesa ndiyo kila kitu.
😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Nadhani kwanza ni ukaribu na maeneo wanayoishi watu wengi wa aina hiyo mbezi beach, mikocheni na sehemu zingine.
Pili ni nafasi iliyopo pale kwa maana ya watu wengi kwenda
Tatu, ni uchache wa maiti zinzokuwa pale hivyo mnajikuta watu mnaoenda kuchukua mwili pale mnakuwa wachache tofauti na hospital zingine
Nne, uchache huo wa miili inayohifadhiwa pale inapafanya pawe mahala salama kwa utunzaji wa maiti.
Mtu yeyote anaweza kwenda pale, mm wakati naishi mitaa ya kunduchi nimewahi kuhifadhi pale ndugu zangu wawili, it s cheap n neat.
 
Wakuu.

Kila mara (na mara zote ) anapofariki kiongozi mkubwa serikalini au mtu maarufu kisiasa / kidini na kijamii lazima mwili wake ukalale / ukahifadhiwe hospitali ya Jeshi Lugalo.

Hata akifarikia nje ya nchi au hospital yoyote Dsm ama jirani na Dsm , lazima akahifadhiwe hospitali ya jeshi lugalo.


1. Kuna mchwari nzuri (standard) ?


2. Lugalo ni mahususi kwa ajili ya viongozi wakubwa na watu maarufu ?




Kuna siri gani pale Hospital ya Lugalo ?


Kuna Muhimbili , Regency , Mwananyamala , Ilala (Amana), Temeke n.k n.k !
 
Back
Top Bottom