Kwanini maiti inapoingizwa nyumbani hutangulizwa kichwa tofauti na kanisani(Anglican) ambapo miguu hutangulia?

bush crazy

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
757
1,020
Naomba mwenye uelewa atuelezee juu ya hili la maiti kutangulizwa kichwa inapoingizwa nyumbani tofauti na kanisani(Anglican) ambapo miguu hutangulia?
 
Kanisani(Anglican na kanisa katoliki mengine sijui)akisimama ai face madhabahu ambapo kwa mapadri kichwa hutangulia akisimama awa face waumini
 
Inategemea na yule wa mbele ameshika upande upi, kama umeshika upande wa mapajani bc upande huo huo utakuwa wa kwanza kutangulia
 
Ni utaratibu tu ambao watu hujiwekea ili wajitofautishe na wengine hususani katika jambo ambalo linafanywa na watu tofauti tofauti

kwaiyo kila mtu hubuni aina yake ya upekee katika kulitekeleza jambo ili kuweza kujitofautisha na wengine ambao nao wana desturi ya kufanya hilo jambo

Mfano: dini karibia zote hapa africa na uimwenguni kiujumla zinatambua ibada ya mazishi vipi kama lundo hilo la dini lingetumia kanuni na utaratibu unaofanana bila kutofautiana? Tungetofautishaje?

Na ndio maana waislamu hawaziki kwa jeneza na sio kwamba mbao hamna la hasha ni tamaduni ya kiupekee kujitofautisha na wakristo

Kwaiyo kabla hujaanza kuuliza kwanini miguu inaanza kuingia ndani ebu jiulize, kwani ndio hicho kitu pekee kinachofanya hilo dhehebu litofautinae na madehebu mengine au kuna kitu kingine extra?

Historia ya Martin luther inaonesha alitokea catholic akaanzisha madhehebu yake mengine nadhani na hilo la anglican likiwemo, je katika hayo madhehebu yake angetumia kanuni zile zile zilizokua zinatumika akiwa catholic ungewezaje kuyatofautisha madhehebu yake aliyoyaanzisha na huko alikotoka?
 
Naomba mwenye uelewa atuelezee juu ya hili la maiti kutangulizwa kichwa inapoingizwa nyumbani tofauti na kanisani(Anglican) ambapo miguu hutangulia?
Sorry, ni ujinga tu wa imani za kishirikina zisizo na scientific backing. Wote huo ni woga wa mwanadamu wa kifo! A dead body is a manure in the making ready for nutrient circulation...
 
Ni utaratibu tu ambao watu hujiwekea ili wajitofautishe na wengine hususani katika jambo ambalo linafanywa na watu tofauti tofauti

kwaiyo kila mtu hubuni aina yake ya upekee katika kulitekeleza jambo ili kuweza kujitofautisha na wengine ambao nao wana desturi ya kufanya hilo jambo...
Hivi hapa umeongea nini? Sijui kama unaeleweka
 
Back
Top Bottom