Kwanini maiti inaelea majini?

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
232
616
Kwanini baadhi ya watu walio hai hawawezi kuelea majini lakini mwili wa mtu aliyekufa huibuka na kuelea majini?

Ni nini faida yake katika Sanaa ya uchunguzi?

Wahusika wa matukio ya mauaji ya watu yaliyotokea miaka ya 2016-18, ambao waliitupa miili hiyo mtoni na baharini, awali hawakujua kama miili hiyo itaibuka. Baadaye wakawa wanaongeza mawe kwenye sandarusi ili kuongeza uzito na kuzuia miili isiibuke. Lakini iliibuka.

Kwanini?

Mwili wa mtu aliye hai unaweza kuelea majini ikiwa mtu atavuta hewa na kujaza mapafu yake. Lakini maiti haiwezi kujaza hewa mapafuni, haiwezi kupumua.

Maelfu ya bakteria waliopo kwenye njia ya chakula, hasa tumboni hufanya shughuli zao za kuozesha mabaki ya chakula na kwa kufanya hivyo huzalisha gesi za aina mbalimbali. Shughuli hizi za bakteria hufanyika kwa watu walio hai na waliokufa.

Kwa mtu aliye hai, gesi hizi hutolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo - kujamba. Lakini mwili wa mtu aliyekufa haujambi wala hauna namna ya kutoa hewa hizo, hasa hasa unapokuwa chini ya maji.

Matokeo yake ni gesi/hewa hizo kujililimbikiza mwilini na kuufanya mwili kujaa hewa tumboni na maeneo mengine na hivyo kuelea majini.

Hali ya joto kati ya nyuzi 20-30 huchochea zaidi shughuli hizo za bakteria, wakati hali ya baridi hupunguza kasi ya shughuli hizo. Maana yake ni kuwa, katika maeneo ya joto, miili inayotupwa majini huibuka ndani ya muda mfupi kuliko inavyokuwa katika maeneo ya baridi - kwa sababu shughuli za bakteria za kuozesha na kuzalisha gesi hufanyika kwa haraka zaidi maeneo ya joto.

Inakadiriwa kuwa, mwili wa mtu unaweza kuibuka baada ya siku 5 hadi 10 kwa maeneo ya joto, na huweza kuchukua muda mrefu zaidi katika mazjngira ya baridi.

Aidha kwenye baridi kali kupita kiasi, mwili wa marehemu unaweza usiibuke kabisa kwani shughuli za Bakteria hazitofanyika kwenye mazingira hayo.

Katika sayansi ya uchunguzi wa matukio ya UHALIFU, wachunguzi wanaweza kutumia tukio la mwili kuelea majini kwa kukadiria muda uliopita tangu mtu huyo auawe (siku 5 hadi 10).

Dr.Christopher Cyrilo
 
Back
Top Bottom