Kwanini Magufuli ni Rais bora kushinda Marais wote Afrika kwa sasa

hansmak

Member
Feb 24, 2015
25
28
Kadri siku zinavyokwenda Tanzania, Mh. Magufuli anazidi kujipambanua kama kiongozi bora miongoni mwa viongozi wa Afrika.

Sababu zipo nyingi kuthibitisha ukweli wa hoja hii. Japo sababu hizi kwa kiasi kikubwa zinahitaji ufafanuzi wenye hazina kubwa ya mifano lukuki na kuntu. Lakini kwa leo nitaishia kuorodhesha nukta kadhaa, na Mungu akinipa pumzi na afya njema nitaelezea kwa kina kila nukta. Itoshe tuu kwa leo kuorodhesha nukta hizi muhimu.

1. Magufuli ni mzalendo wa kweli kwa nchi yake na Afrika kwa ujumla.
2. Magufuli ni kiongozi mwenye maono.
3. Ni Rais mwenye misimamo isiyoyumbishwa.
4. Ni kiongozi asiyechoka kujaribu kila njia yenye dalili za mafanikio
5. Ana mapenzi na huruma kwa watu wake
6. Rais Magufuli ameweza kuunda timu nzuri ya watu wanaotafuta, kuchambua, kuchanganua, kuchuja na kutafsiri taarifa zinazochangia maendeleo chanya kwa mustakabari wa taifa letu.
7. Ana uwezo mkubwa wa kutatua changamoto na majanga mbalimbali kwa njia sahihi zinazoendeana mazingira ya nchi yetu.
8. Ni kiongozi mwenye uwezo wa kujikosoa kwa vitendo.
9. Ni kiongozi mwenye hofu ya Mungu kwa mujibu wa imani yake.
10. Magufuli ni msemakweli iliyokweli.
11. Huteua mtu yeyote bila kujali chama kushika nyadhifa mbalimbali.
12. Magufuli ameonesha uwezo mkubwa wa kusimamia rasilimali za taifa na kuzitumia kwa maslahi mapana ya taifa letu.
13. Ana nia thabiti ya kupunguza kiwango cha umaskini kwa watanzania walio wengi.
14. Ni Rais ambae kwa kiasi kikubwa ameweza kurudisha na kuimarisha nidhamu kwa watumishi wa umma.

Kama nilivyotangulia kusema mwanzoni kabisa mwa bandiko hili kwamba yanahitajika maelezo na mifano kadhaa ili kunasibisha kila nukta niliyoitoa hapo juu. Nitakapopata wasaa wa pumzi, afiya njema, muda na utulivu mzuri wiki ijayo nitaelezea kila hoja.

Mbali na kuelezea kwa kina hoja hii kama kichwa cha habari kinavyoeleza, lakini nitaonesha dhahiri shahiri ni jinsi gani mambo haya yanayompambanua Rais Magufuli yamechagiza kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa nchi na watanzania kwa ujumla. Pia nitaelezea kwa kina matokeo na mapokeo ya watu wa makundi mbalimbali yalivyopokea utendaji wa Magufuli na athari zake.

Nichukue fursa hii kukaribisha wanajamvi kuchangia katika bandiko hili. Sitarajii tufanane kimtazamo lakini pia ikibidi tofauti zetu hasa katika uchangiaji wa hoja hii uwe wenye tija kwa taifa. Lakini ikitokea ni lazima kutofautiana basi tuache nafasi ya kukubaliana kutokukubaliana kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa letu.

ALAMSIKI

#PAMOJA TUTAISHINDA CORONA#
#KUMPENDA MAGUFULI NI KUPENDA MAENDELEO#
 
Yote Tisa kumi Mkuu wa mataga anapashwa kutuonesha viwanda elfu nne kavijenga wapi, pia Mil 50 kila kijiji safari hii hata mkivaa bullet proof tunawashoot kichwani, mnachochea moto huku amjui kupika.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yote Tisa kumi Mkuu wa mataga anapashwa kutuonesha viwanda elfu nne kavijenga wapi , pia Mil 50 kila kijiji safari hii hata mkivaa bullet proof tunawashoot kichwani , mnachochea moto huku amjui kupika.
Bilion 8, ziko wapi kamanda?
 
😂😂😂😂 Nitag MKUU ukijulishwa vilipo hivyo viwanda.

Yote Tisa kumi Mkuu wa mataga anapashwa kutuonesha viwanda elfu nne kavijenga wapi , pia Mil 50 kila kijiji safari hii hata mkivaa bullet proof tunawashoot kichwani , mnachochea moto huku amjui kupika.
 
Yote Tisa kumi Mkuu wa mataga anapashwa kutuonesha viwanda elfu nne kavijenga wapi , pia Mil 50 kila kijiji safari hii hata mkivaa bullet proof tunawashoot kichwani , mnachochea moto huku amjui kupika.
Utavionaje viwanda na ujawai kwenda popote Tanzania. Umezaliwa apo apo umekulia apo na utazeekea apo kwenye nyumba ya urithi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na yooote hayo, isije ibuka au kuendeleza ile mipango yenu ninaomba tuilinde katiba yetu.
 
Kadri siku zinavyokwenda Tanzania, Mh. Magufuli anazidi kujipambanua kama kiongozi bora miongoni mwa viongozi wa Afrika.

Sababu zipo nyingi kuthibitisha ukweli wa hoja hii. Japo sababu hizi kwa kiasi kikubwa zinahitaji ufafanuzi wenye hazina kubwa ya mifano lukuki na kuntu. Lakini kwa leo nitaishia kuorodhesha nukta kadhaa, na Mungu akinipa pumzi na afya njema nitaelezea kwa kina kila nukta. Itoshe tuu kwa leo kuorodhesha nukta hizi muhimu. 1. Magufuli ni mzalendo wa kweli kwa nchi yake na Afrika kwa ujumla.
2.Magufuli ni kiongozi mwenye maono.
3. Ni Rais mwenye misimamo isiyoyumbishwa.
4. Ni kiongozi asiyechoka kujaribu kila njia yenye dalili za mafanikio
5. Ana mapenzi na huruma kwa watu wake
6. Rais Magufuli ameweza kuunda timu nzuri ya watu wanaotafuta, kuchambua, kuchanganua, kuchuja na kutafsiri taarifa zinazochangia maendeleo chanya kwa mustakabari wa taifa letu.
7. Ana uwezo mkubwa wa kutatua changamoto na majanga mbalimbali kwa njia sahihi zinazoendeana mazingira ya nchi yetu.
8. Ni kiongozi mwenye uwezo wa kujikosoa kwa vitendo.
9. Ni kiongozi mwenye hofu ya Mungu kwa mujibu wa imani yake.
10. Magufuli ni msemakweli iliyokweli.
11. Huteua mtu yeyote bila kujali chama kushika nyadhifa mbalimbali.
12. Magufuli ameonesha uwezo mkubwa wa kusimamia rasilimali za taifa na kuzitumia kwa maslahi mapana ya taifa letu.
13. Ana nia thabiti ya kupunguza kiwango cha umaskini kwa watanzania walio wengi.
14. Ni Rais ambae kwa kiasi kikubwa ameweza kurudisha na kuimarisha nidhamu kwa watumishi wa umma.

Kama nilivyotangulia kusema mwanzoni kabisa mwa bandiko hili kwamba yanahitajika maelezo na mifano kadhaa ili kunasibisha kila nukta niliyoitoa hapo juu. Nitakapopata wasaa wa pumzi, afiya njema, muda na utulivu mzuri wiki ijayo nitaelezea kila hoja.
Mbali na kuelezea kwa kina hoja hii kama kichwa cha habari kinavyoeleza, lakini nitaonesha dhahiri shahiri ni jinsi gani mambo haya yanayompambanua Rais Magufuli yamechagiza kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa nchi na watanzania kwa ujumla. Pia nitaelezea kwa kina matokeo na mapokeo ya watu wa makundi mbalimbali yalivyopokea utendaji wa Magufuli na athari zake.

Nichukue fursa hii kukaribisha wanajamvi kuchangia katika bandiko hili. Sitarajii tufanane kimtazamo lakini pia ikibidi tofauti zetu hasa katika uchangiaji wa hoja hii uwe wenye tija kwa taifa. Lakini ikitokea ni lazima kutofautiana basi tuache nafasi ya kukubaliana kutokukubaliana kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa letu.
ALAMSIKI

#PAMOJA TUTAISHINDA CORONA#
#KUMPENDA MAGUFULI NI KUPENDA MAENDELEO#
Kweli?!
Ni rais bora kwa kutotoa takwimu halisi za corona hadi sasa ambapo Tanzania haijaweka wazi takwimu za corona kwa mwezi sasa wakati wenzetu wote Africa wana-update takwimu zao kila siku hata mara 2 au 3?

Ni rais bora kwa kuzika wahanga wa corona usiku wa manane?

Ni rais bora kwa kuwatimua wataalamu wenye profession na kuwajaza watu wake wa karibu ili kutatua matatizo ya kitaalam kwa kutumia siasa?

Watanzania sijui lini tutakuwa na uelewa mzuri wa mambo.
 
Back
Top Bottom