Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Moja ya hofu kubwa aliyonayo Rais John Magufuli ambaye pia anagombea nafasi ya Urais ni Kuwa watanzania wawe makini na kura Maana wanaweza kuwapigia Kura Watu halafu wakaiuza nchi ama wengine kuharibu miundombinu ambayo Serikali yake inaijenga.Rais ameenda mbali na kuwataka watanzania wasifanye majaribio Kwenye kuchagua.
Nadhani namna pekee ambayo inaweza kuwa tiba dhidi ya hofu ya Mh Rais ni kuibadili katiba yetu pamoja na mfumo mzima wa kiutawala ili tujenge taifa lenye Taasisi Imara Kama alivyopata kushauri Prof Mussa Assad wakati akihojiwa na idhaa ya Kiswahili ya umoja wa mataifa.
Kama hofu ya Rais Magufuli inatoka moyoni na anamaanisha basi Hii ni ishara nchi hii....
1.Katiba yake ni dhaifu Maana haina ubavu wa kumzuia mtu kutorosha mali,Kwa nini Rais Magufuli Kwenye Kampeni zake asianze Sasa kuahidi kuendeleza mchakato wa kuandika Katiba mpya ili tuwe na Katiba inayowadhibiti viongozi?
2.Nchi Hii ina taasisi dhaifu ambazo haziwezi kuwadhibiti viongozi wasifanye watakavyo,Kama ni hivyo Kwa nini Rais Magufuli asiwaahidi watanzania Kuwa akichaguliwa Kuwa Rais atabadili Katiba ili tuwe NA Katiba ambayo itajenga taasisi imara(Bunge,Mahakama,Vyombo vya ulinzi na usalama),ambavyo vitawadhibiti viongozi wetu wasifanye watakavyo.
Binafsi nauona mwarobaini wa hofu aliyonayo Mh Rais,labda huko mbele ataungana na wagombea wengine kuahidi mabadiliko ya Katiba Kwa kuandika Katiba mpya ambayo itajibu changamoto za nchi.
Wasalaam.