Kwanini magerezani na mabenki uchawi haupiti?

B'REAL

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
4,279
2,733
Habari za saa hizi wakulugwaa.

Kuna swali huwa najiuliza sana nakosaa majibu. Uchawi upo hata kama hatuamini Ila upo. Je, ni kweli kwamba magereza na mabenki mengi huwa kuna zindiko so nguvu za Giza haziwezi kufanya kazi? Mfano mtu amefungwa kwenye gereza hakuna uwezekano wa kutumika mfungwa atoroshwe/atoweke gerezani?

Kwenye mabenki hakuna nguvu za giza zinaweza kumfanya mtu aingie asionekane mpaka strong room(wanapo hifadhi pesa na kuchukua pasipo kuonekana?
 
Nikiwa darasa la kwanza asubuh moja mstarini aliletwa bingwa mmoja mwanakijiji. Alikuwa ameletwa na askari Polisi. Wanafunzi wote na Walimu wetu tulikuwepoa kama kama.

Issue ilikuwa yule bingwa alikuwa anakamatwa kwa uhalifu wa aina mbalimbali na kupelekwa mahabusu lakini bingwa alikuwa anatoka bila kujulikana anatokaje na kurudi kijijini.

Polisi walichoka. Ikawa kama wanamuachia kumbe hawamuachii. Ilibidi siasa itumike. Walimsihi aache kutoroka kimazingara maana hiyo siyo tabia ya raia mwema. Sasa aliletwa mbele yetu shuleni akikiri kutoroka mahabusu kimazingara na kuwa asingerudia kufanya hivyo maana ni raia mwema sasa na kwamba alichokuwa anafanya si tabia nzuri.

Kweli. bingwa hakurudia tena mauzauza yake, akabaki huko mahabusu. Duniani kuna mambo.
 
Magerezani huwa wanatoroshwa kwa nguvu ya giza.Nikiwa mwanafamilia wa Askali mstaafu wa gereza la Kasungamile wilayani Sengerema, kuna mfugwa alikuwa akitoroka mara kwa mara kwa kugeuka ndege na anaporushwa nje ya ngome basi huyo jamaa utoweka hivyo hesabu ya mfugwa/mahabusu upungua.
avatar yako inatisha kinyaaama
 
Kitendo cha kushindwa kuiba hela bank kwa kutumia uchawi, kushindwa kutoroka gerezani kwa kutumia uchawi, kushindwa kushinda kombe la dunia la mpira wa miguu kwa kutumia uchawi na kadhalika inathibitisha kuwa uchawi haupo!
Mbona wananchi wanapiga mayowe ya paka ..paka hadi hii leo navyokwambia hawaamini mtani wao anao uwezo huo....!
 
Au sheli aiseee kuna mtu muendesha bajaji alisema akihisi pesa anayopewa ni chuma ulete anapeleka shell kule hizo mambo hazifanyi kazi
 
Nasikia mabenki yote yanalindwa na majini mawili yenye nguvu sana kuliko hivi vijini vinavyotumiwa na watu watu wa kawaida huku mtaani.... Yaani kwa kifupi fedha iko chini ya shetani ambapo ameweka watoto zake wawili kuzilinda.
 
Uchawi ni ishu kama ya kudimbadimba. Ni kitu cha kujifurahisha, hani madhara yoyote ya maana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom