Kwanini magari yenye namba za Serikali huwa hayakatiwi bima kwa ajili ya usalama wa abiria na watumishi wengine wa barabara kama matatizo binafsi?

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,905
Wakuu kila la heri na maandalizi ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Moja kwa moja kwenye mada, magari binafsi yanakatiwa bima kwa ajili ya usalama wa vyombo na watumiaji wengine wa barabara pindi ajari zikitokea lakini kwa magari ya serikali ni tofauti kwamba hayana bima.

Swali langu ikitokea ajali ya magari ya serikali kumgonga mtumiaji mwingine wa barabara na kumsababishia ulemavu au kifo au ajali ikawapata maofisa wa Serikali ,watu hao wanapataje haki yao ya fidia kutokana na madhara ya ajali?

Mbona huku kwenye magari binafsi unaweza kwenda kudai fidia kwenye makampuni ya bima kama vielelezo vinajitosheleza na ukapata.

Naomba kufahamishwa.
 
Mkuu sababu ni kwamba serikali yenyewe inaweza kulipa fidia kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mtu / watu binafsi katika muda wowote ule.
Lakini pia serikali ndio insurer mkubwa wa wote hao makampuni ndiomana wameweka deposit zao kwake(B.O.T)
 
Ok sasa in case gari ya serikali imenisababishia ajali taratibu za kudai fidia zikoje?
 
Kwanini unasema hayakatiwi Bima au kwakuwa hauoni Stickers
Ni kweli mkuu huwa sioni sticker na nilimuuliza dereva wa serikali akasema hakuna bima hata wakigonga au ajali ikihusu maafisa ndio inakuwa nitolee hivyo
 
Ni kweli mkuu huwa sioni sticker na nilimuuliza dereva wa serikali akasema hakuna bima hata wakigonga au ajali ikihusu maafisa ndio inakuwa nitolee hivyo
Alikupoteza.
Endapo Maafisa wa Serikali wameumia Ajalini ktk Safari yoyote ya kikazi, Serikali inalipa Fidia kupitia MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) Workers Compensation Fund na Inalipa parefu kuliko hizo Bima.
Pia endapo gari la Serikali (ST.., JW, PT, MT, UT nk) itasababisha hasara na Mahakama ikathibitisha Serikali kupitia Wizara ya Fedha itamlipa mlengwa bila kuchelewa. Angalia muuundo wa Wizara ya Fedha utaiona idara inayohusika na Fidia.
Lkn magari yenye namba za DFP,SM na SU wao wanakata bima na hivyo endapo litasababisha traffic case Bima itawajibika.
 
Ni kweli mkuu huwa sioni sticker na nilimuuliza dereva wa serikali akasema hakuna bima hata wakigonga au ajali ikihusu maafisa ndio inakuwa nitolee hivyo
huyo suka nahisi ajitambui, bima ni lazima kwa gari za serikari. nahisi muuliza swali akishapata majibu atauliza tena , madereva wa serikali nasikia hawatakiwi kuwa na leseni
 
Back
Top Bottom