Kwanini mafundi wa kushona nguo hali yao ya maisha ni ya chini?

mfugaji kuchi

Member
Sep 2, 2020
9
7
Nauliza kwa nini mafundi wa kushona nguo wanakuwa hawatajiriki na
Kubaki hivyo hivyo miaka na miaka?

Yaani unakuta fundi miaka na miaka
Yuko hivyo hivyo.
 
Nauliza kwa nini mafundi wa kushona nguo wanakuwa hawatajiriki na
Kubaki hivyo hivyo miaka na miaka?

Yaani unakuta fundi miaka na miaka
Yuko hivyo hivyo.
Mindset. Wamefanya ni biashara ya kupata mkate wa kila siku tu na Mungu sio mchoyo huwapa. Huwezi kuwa tajiri, kama utajiri hujauona kwenye fikra kwanza ndio uufanyie kazi through burning desire ndipo utoboe.
 
Mafundi wa ushobaji wana levels ni kama mama lishe na kibanda chake na mmiliki wa five star hotel. Mfano bora hapa mjini kuna mafundi wakubwa tu mfano Chidy design, speshoz, ki2pe, jm international collection, na wengine wengi tu ni vijana ambao wamefanikiwa kupitia hii industry ya ushonaji. Ni wamefanikiwa kwa sababu wameamua kuifanya shughuli yao kwa ukubwa tofauti na mafundi wako wa uchochoroni wanaoshonea vibarazani.
 
Bro unawaangalia mafundi waliopo kwenye vibaraza vya nyumba uswahilini?? Nenda kaangalie mafundi nguo waliokodi floor nzima sinza, kijitonyama,posta ,wanawafanyakazi zaidi ya 30,wanapata tenda za kushonea makampuni Kama crdb,timu za mpira,nenda kaone ofisi za kina jm collection,chidi design,sheria Ngowi,Martin kadinda,halaf ndo uje tujafili upya Uzi wako, hao unaowataja haina tofauti na mama ntilie wa mtaani haimaanishi kuwa hakuna watu wenye mahoteli makubwa wanaofanya vzr
 
Hali ya chini ni kuanzia kipato gani mkuu au unatakiwa uonekane vipi ili ujuwe kuwa huyu mtu ana hali ya chini? don't judge a book by it's cover...
 
Kinacholeta hela kwenye biashara ni mauzo makubwa na mauzo makubwa yanahitaji production kubwa Sasa kazi ya mtu mmoja inazalisha mauzo kidogo Ila wale walioajiri kuongeza production kubwa na vifaa vya kuzalisha kwa haraka wapo vizuri. Kama waliotoa mfano wa hotel, alafu usidharau viraka hivyo viraka vinahela sana maana unatengeneza nguo nyingi na zinalipiwa haraka kwa watu wa chini kutoa 2000 kwa kupitishiwa uzi nguo iliyoachia hawaoni shida, mara kupunguza pazia, mara nguo, mara kubana nguo wewe usidharau viraka kabisa vinahela hivyo hata wengine vifungo vya shati vikikatika mpaka fundi amrudishie hiyo tu nikiraka.
 
Kwanza wengi wababaishaji tu, siyo wakweli, kuepuka kugombana na fundi watu wengi siku hizi wananunua nguo readymade.
 
Back
Top Bottom