Kwanini mafundi magari (mechanics) walio wengi ni wachafu?

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,953
Habari zenu wakuu.

IMG-20130802-WA0001.jpg

Wakuu naomba tueleweshane kwenye hili,ni kama macho yangu yameshazoea kuona fundi anayejiusisha na magari,pikipiki na vinavyovanana na hivo kuwa ni WACHAFU. Sisemi ni wote ila nadhani kati ya 70% - 85% wapo hivo,sasa sijajua kwanini inakuwa hivi ??

Natanguliza shukrani zangu.
 
Am happy kuwa wa kwanza kureply

Labda utuambie uchafu maana yake nini...

Je, mwalimu akipakazwa na vumbi la chaki naye anakuwa mchafu?? Daktari akitapakaliwa na damu anaweza akaitwa mchafu?? Mvuvi akinuka shombo la samaki anakuwa mchafu?

Je, uchafu wa hawa mafundi ni kwakuwa wanakuwa wameshika grease na oil??
 
Kwako unaweza kuona ni uchafu lakini kwake Ndo namna pekee ya kung'arisha maisha yake. Je Wewe ukipeleka gari lako gereji ukakuta mekanika kaulamba suti utamwamini?
 
Labda utuambie uchafu maana yake nini...

Je mwalimu akipakazwa na vumbi la chaki naye anakuwa mchafu?? Daktari akitapakaliwa na damu anaweza akaitwa mchafu?? Mvuvi akinuka shombo la samaki anakuwa mchafu?

Je uchafu wa hawa mafundi ni kwakuwa wanakuwa wameshika grease na oil??
1. Uchafu maana yake ni kutoweza kujitunza kwa maana ya kujiweka nadhifu,wewe mwenyewe,mazingira yako na wale wanaokutegemea.
2. Yes, Mwalimu,Dr na Mvuvi kama watatoka mazingira ya kazi yao na bado wapo vile walivyokuwa kazini ni WACHAFU TU NA WENYEWE.

3. Uchafu wao ni kutokujibadilisha,yaani sanasana atabadili nguo za kazi tu,lakini jinsi mwili wake utakavyokuwa ndio hivo hivo anaenda nyumbani.
 
Kwako unaweza kuona ni uchafu lakini kwake Ndo namna pekee ya kung'arisha maisha yake. Je Wewe ukipeleka gari lako gereji ukakuta mekanika kaulamba suti utamwamini?
Tatizo sio wakati yupo kazini,ila baada ya kazi ndio hoja yangu ilipo unakuta wengine bado wapo wachafu wachafu.
 
Tatizo la wale mafundi ni mazoea tu hata baada ya kazi wameizoesha akili yao km vile mda wowote mteja anaweza tokea sasa akiwa msafi atashindwa kipiga kazi
 
Tatizo la wale mafundi ni mazoea tu hata baada ya kazi wameizoesha akili yao km vile mda wowote mteja anaweza tokea sasa akiwa msafi atashindwa kipiga kazi
Wanapiga pesa ndefu,lakini usafi bila.
 
Asante sana kwa mwanzishaji wa uzi huu. Hakuna kitu kinachoudhi kama kupeleka gari yako kwa fundi ikiwa spotless clean halafu jamaa na ovaroli lake chafu kabisa likiwa na grisi anakaa kwenye kiti bila kujali chochote. Yote tisa kumi unarudishiwa gari ikiwa na alama za grisi na vidole kwenye bodi na dashboard. Inaboaaaa!
Maoni yangu nik kwamba wengi wa mafundi hawa hawapati formal training. Hufundishana wenyewe tu. Na bahati mbaya wanarithi tabia mbaya za waalimu wao wakidhani ni sehemu ya ufundi. Wabadilike.
 
Labda utuambie uchafu maana yake nini...

Je mwalimu akipakazwa na vumbi la chaki naye anakuwa mchafu?? Daktari akitapakaliwa na damu anaweza akaitwa mchafu?? Mvuvi akinuka shombo la samaki anakuwa mchafu?

Je uchafu wa hawa mafundi ni kwakuwa wanakuwa wameshika grease na oil??
Naona ushamjibu
 
Habari zenu wakuu.

Wakuu naomba tueleweshane kwenye hili,ni kama macho yangu yameshazoea kuona fundi anayejiusisha na magari,pikipiki na vinavyovanana na hivo kuwa ni WACHAFU. Sisemi ni wote ila nadhani kati ya 70% - 85% wapo hivo,sasa sijajua kwanini inakuwa hivi ??

Natanguliza shukrani zangu.
Ni wachafu au wanavaa nguo zenye mafuta mafuta na vumbi vumbi? Mavazi yanategemea sana na mazingira ya kazi.
 
Ni wachafu au wanavaa nguo zenye mafuta mafuta na vumbi vumbi? Mavazi yanategemea sana na mazingira ya kazi.
Uchafu wao ninaouzungumzia hapa ni ule wa baada ya kazi, sio ule wa wakati wa kazi.
 
SIO wote hufanya ivyo . NA pia ni kujitambua tuu ..Pia hata www na utanashati wako pia somtimes ni mchafuu
 
Uchafu wao ninaouzungumzia hapa ni ule wa baada ya kazi, sio ule wa wakati wa kazi.
Ukivaa miwani ya bluu kila kitu utakiona ni cha bluu, uchafu baada ya kazi ni mazoea ya mtu binafsi haijalishi anafanya kazi gani! Nadhani unazungumzia unaowaona wanapiga Story nje ya gereji mida ya jioni kabla ya kujisafi
 
Kwanza tuombe radhi mafundi wote wa magari,
Pili ni hivi
Ukiona fundi mchafu basi tambua huyo ni mlevi kwanza

Ukiona fundi mchafu
huyo ni mshamba
Naona ni ujiko kuitwa fundi garage

Ukiona fundi ni mchafu
Labda mazingira ya kazi siku hiyo yalimrazimisha kuchafuka kwa bahati mbaya na akuwa na jinsi kwa sababu akuwa na nguo za kazi
Na fundi magari uwa atulembi popote kambi
Ukiaribikiwa na gari lako sisi tunakuuliza tu unaspana basi lakini uwa atuulizagi una overllor
Ukinipa spana mie nazama tu uvunguni hata nikiwa nimevaa suti, kazi ipo kwenye damu.
 
sio uchafu bwana,nimazingira ya kazi zao, hivi ulishawahi kumuona mchinjaji wa ng'ombe pale vingunguti ni MSAFI?
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom