Kwanini Maduka mengi ya dawa za binadamu hayajiungi na mfuko wa Taifa wa bima ya afya(NHIF)?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,294
217,294
Upo ushahidi wa macho na masikio wa maduka mengi ya dawa ya rejareja kutotaka kabisa kufanya kazi na NHIF , hii ni hata yale maduka yaliyo karibu kabisa na Hospitali kubwa , kama Muhimbili , Amana na Temeke , ambako wagonjwa wanaotumia bima hii ni wengi , na kwa vile Hospitali zetu hazina dawa za kutosha , wanahitaji huduma hiyo.

Shida iko wapi , mbona naona kama wanapoteza fursa ya kutajirika ?
 
Maduka mengi yapi? unataka hata kiduka chako cha huko Kimanzichana kikubaliwe NHIF hebu acheni kutughasi tunaonufaika na hii huduma. Na awamu hii bima binafsi (Jubilee, STRATEGIS n.k mtaisoma namba BoT, TRA na mashirika mengine ya umma wameambiwa waamie NHIF mtabaki na tukampuni twa binafsi twa mfukoni) hakuna dili za serikalini tena.
 
Si kwamba maduka yanaitaka NHIF , la hasha ! Bali NHIF ndio inayataka maduka lakini wenye maduka wanaikataa .
 
Wana sababu zao labda mkuu
Zipo tetesi kwamba NHIF haiwalipi watoa huduma kwa wakati , inasemekana inaweza kuchukua mpaka miezi 6 bado mtoa huduma halipwi , sasa hili ni la kweli ? Maana kiukweli wagonjwa wanahitaji huduma .
 
NHIFwanachagua maduka makubwa na yale ya uhakika hivi vya uchochoroni wanavipotezea
 
Zipo tetesi kwamba NHIF haiwalipi watoa huduma kwa wakati , inasemekana inaweza kuchukua mpaka miezi 6 bado mtoa huduma halipwi , sasa hili ni la kweli ? Maana kiukweli wagonjwa wanahitaji huduma .
Ni kweli na pia NHIF Ina madaktari ku approve kila huduma na kama hawajaridhika hawalipi,sasa si unajua vyeti vyetu ugonjwa mmoja madawa kumi.
 
Kosa lake ni kujua kuwa angeweza kutoa dawa za aina mbili tu,ila katoa nane. Angeweza kutoa dawa za siku tano tu ila katoa saba.
Nilidokezwa kwamba sheria za Pharmacy haziruhusu ku edit prescription , dawa zimeandikwa na daktari hospitali haiwezekani mtoa dawa kuzikataa.
 
Nilidokezwa kwamba sheria za Pharmacy haziruhusu ku edit prescription , dawa zimeandikwa na daktari hospitali haiwezekani mtoa dawa kuzikataa.
Wala hukudanganywa,ni kweli kabisa ila nani wanaomiliki hizo pharmacies na dispensary? Hudhani kuwa wanafanya kazi pamoja na wanashirikiana kupeana maisha?
 
Nilidokezwa kwamba sheria za Pharmacy haziruhusu ku edit prescription , dawa zimeandikwa na daktari hospitali haiwezekani mtoa dawa kuzikataa.
In addition sheria ya prescription ni kuanza na cheapest medication kabla ya iliyo ghali.ugonjwa wa kutibu na amoxyline capsules unaanza na ceftraxone injection halafu unategemea bima watalipa kweli! No way.
 
Sometimes bima hawaangalii na kuupdate bei zao keandana na bei ya soko. Unakuta ukitoa dawa kwa bei yao unapata hasara. Pia kama unamtaji mdogo utabaki na duka tupu maana hawalipi kwa wakati.
 
Sometimes bima hawaangalii na kuupdate bei zao keandana na bei ya soko. Unakuta ukitoa dawa kwa bei yao unapata hasara. Pia kama unamtaji mdogo utabaki na duka tupu maana hawalipi kwa wakati.
Hii yaweza kuwa sababu ya msingi .
 
Back
Top Bottom