Bana likasi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2020
- 6,927
- 6,417
Katika nchi nyingi za kiafrika ambazo watu wanauawa hovyo, kutekwa, majanga kama mafuriko, wakulima hawana masoko wafanyakazi mishahara duni biashara kudorola halafu unakuta Television ya taifa hilo kila uchao linapiga nyimbo za kumsifia rais.
Nchi hizi hutegemea fedha za Mabeberu ktk kukopa na wananchi ndio wanalipa madeni hayo yenye riba kubwa. Lakini wakipata pesa kutoka kwa Mabeberu utasikia eti Rais katoa pesa kujenga barabara. Pesa wametoa Mabeberu kwa mkopo halafu yana jitukuza eti ni Rais katoa wakati yeye mwenyewe analipwa mshara na malupulupu na wananchi wanyonge wa nchi hizo. Kwa nini madikteta hupenda sana kusifiwa?
Madikteta hupenda kujionesha yako jirani na watu na yanapendwa. Utayaona yanaigiza kula chakula au kunywa chai wakiwa na watu na wakiwa wanakula lazima tukio hilo litangazwe ili watu waone kuwa Dikteta amekula na watu au amekunywa chai na watu.
Kule Kenya nakumbuka Rais Moi vyombo vya habari vilikuwa vikimuita Mtukufu Rais Daniel Araph Moi. Nyimbo katika radio zilikuwa zinamsifia yeye na KANU tu. Kumbe watu huku wakimuimbia nyimbo za sifa Moyoni wanamng'ong'a hiloo linapenda sifa.
Leo KANU ya Moi iliyokuwa ikisifiwa na kutukuzwa tunajua ilipo.
Maendeleo hayana vyama.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tafuta kitabu kinaitwa dictator's mind kimeelezea yote,kuhusu chanzo cha udikteta, tabia zao,hulka zao,nk.
Kiufupi chanzo cha udikteta unaanzia kwenye malezi mabovu muhusika aliyopata au masaibu yoyote aliyopata dikteta utotoni yakaathiri brain yake wengine walishuhudia wazazi wao wakiuliwa kikatili mbele yao,wengine wazazi waliachana utotoni,wengine walitelekezwa utoto,ni jumuisho la matendo yote ya ukatili waliyopitia utotoni mfano shida,umasikini, dhiki,vikapelekea brain kujaa sumu.
Nini tiba yake ni hadi muhusika apate uponyaji wa ndani utakapelekea kuachilia kusamehe yote aliyopitia ili aanze upya.Asipopata uponyaji wa ndani ugeuka kuwa mnyama katili,mlipa kisasi hapa Mara nyingi wanaolipwa visasi au fanyiwa ukatili huwa sio wahusika yaani wengine ndio wanathirika na sio wasababishi wa kumuumiza dikteta utotoni. Kwann wanapenda kusifiwa na kuabudiwa jibu ni walikosa upendo utotoni yaani wariruka stage za ukuaji awakupata upendo utotoni hivo ikawapelekea usugu.
Thus tunashauriwa watoto wadogo tuwe na tabia za kuwabeba na kuwakumbatia vifuani hii ni tiba tosha inawafanya wajihisi salama kwa ajili ya kukuza brain zao na kuleta mizania ya balance.Usimtese mtoto,usimbeze mtoto,usimpuuze mtoto akiwa analia inatakiwa umbembeleze usipofanya hivo unamjengea usugu na hali ya ukosefu wa utu akiwa mkubwa kama akikosa muongozo sahihi mfano dini na elimu chance ya kuwa dikteta ni kubwa.
Wenzetu wamefanikiwa kupata viongozi bora sababu wanafatilia historia ya utoto wa MTU,thus wao wanasonga tu awafail wanapata viongozi bora tofauti na Africa. Pia Africa mifumo yetu ya kimalezi imejengwa kwenye mifumo dume