Kwanini madereva wengi wana ukosefu wa nguvu za kiume? 18+

ANKOJEI

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
998
742
Madereva wanaoendesha magari ya masafa marefu na wale wanaoendesha magari muda mrefu bila kupumzika, waendesha farasi, waendesha baisikeli na wale wanaokaa maofisini muda mrefu wanao uwezekano mkubwa wa kuwa na upungufu wa nguvu za kiume. Ukaaji kwenye kiti muda mrefu unasababisha mzunguko wa damu kutokuwa mzuri kwa sababu mishipa midogo ya damu sehemu za siri hushindwa kabisa kusukuma damu vizuri na wakati mwingine mishipa hiyo inaharibika kabisa.
Ulagi wa mirungi, Ulevi wa kupindukia (isipokuwa mvinyo mwekundu), Ulaji wa nyama choma na ugali wa mahindi yaliyokobolewa, Kutokula matunda, Kutolala usingizi wa kutosha, Michepuko na kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume zenye kemikali na kusimumua mishipa ya fahamu. Madereva wengi huwa na msongo wa mawazo kutokana na muda mwingi kuwa mbali na familia pia vikwazo mbalimbali vya kazi ofisini na barabarani. Wengine hukosa elimu sahihi ya kujamiiana kama kunywa konyagi kabla ya tendo la ndoa wakidhania inawaongezea stamina. Kuna sababu nyingine nyingi pia zinazosababisha upungufu wa nguvu za kiume kwa watu wote lakini pia kwa medereva lakini hapa sijaziorodhesha lakini pia zinahusika kudhoofisha uwezo wa nguvu za kiume kwa madereva.

Ikiwa wewe dereva utakuwa umeathirika na upungufu wa nguvu za kiume lazima ufanye kazi ya ziada kuliko wale ambao sio madereva. Ni muhimu sana kuangalia unakula nini, wapi, saa ngapi na kivipi. Chunguza afya yako mara kwa mara hasa sukari, presha, figo, ini na magonjwa ya moyo. Tumia virutubisho katika umakini wa hali ya juu utarudi katika ujana wako.


[h=1]1. ULAJI WA MIRUNGI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME[/h]
Mirungi imekuwepo tangu karne ya 13 – 15 hivi hapa duniani hasa maeneo ya Yemeni na kusambaa hadi Ethiopia, Kenya, Somalia na sasa Tanzania. Kuna aina nyingi za mirungi lakini maarufu Kenya na Tanzania ni Alenee, Kangeta, Giza na Mbaga. Mirungi inakuwa taratibu sana na inahitaji maji mengi sana kwa ajili ya ukuaji wake. Yemeni kwa mfano inatumia 40% ya maji yake kwa ajili ya mashamba ya mirungi. Mirungi imepigwa marufuku nchini Tanzania kwa sababu imewekwa katika kundi la madawa ya kulevya na ni kilevi chenye uwezo wa kati. Mirungi mingi inayoingia nchini Kenya inatokea Somalia wakati ike inayoliwa nchini Tanzania inatokea nchini Kenya. Tanzania mirungi inaliwa kwa wingi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Dsm, Zanzibar, Mara na Mwanza. Mikoa hii ni ile iliyokaribu na Kenya pamoja na Somalia kwa kuwa inakuwa rahisi kufikisha mirungi katika maeneo haya ikiwa na ubora wake, yaani bado mbichi.

Vichwa vya majani mabichi ya mirungi kama vinavoonekana katika picha hukatwa kimoja kimoja na kusokomezwa mdomoni na kisha kutafunwa na kutunzwa shavuni tayari kwa kusokomeza majani mengine. Utaona mafundo fundo shavuni mwa mlaji mara yakiwa upande huu wa shavu mara ingine upande mwingine. Mlaji akishajaza mirungi mdomoni huendelea kutafuna mpaka ile juice ya mirungi imeisha na kisha makapi huyatema. Juice ya mirungi yenye kemikali za kusisimua huingia mmwilini mwa mlaji kupitia ngozi nyororo ya mdomoni na nyingine hupitia katika ngozi ya uchujaji ya tumboni


KWA NINI MIRUNGI INALIWA?

Mirungi inaliwa kwa sababu inauchachu na utamu flani ambao humfanya mlaji aendelee kula bila kuukinai. Mirungi ina kemikali zinazompatia mtu utegemezi wa kuendelea kuila (addictive) hata kama haina faida yeyeto. Mlaji wa mirungi hutumia kati ya masaa 3 – 4 ya kula furushi la mirungi kila siku. Ndugu msomaji unaweza kujua kwa mwaka anatumia masaa mangapi. Baadhi ya faida za kula mirungi ingawa faida hizi ni za mpito na za muda tu ni:
· Mirungi humfanya mlaji aendelee kuwa mchangamfu hata kama anausingizi.
· Mirungi humfanya malaji aone vizuri nyakati za usiku na pia mirungi inamfanya mlaji azingatie sana kile kitu anchokifanya muda huo (concerntrate).
· Mirungi katika Yemeni na Somalia inaliwa kama mazoea tu na kwa kuwa serikali haijapiga marufuku ulaji wa mirungi wananchi hawana habari ya kwamba inakuwa na kemikali za madawa ya kulevya.

WALAJI WA MIRUNGI NA SABABU ZA KUWAFANYA WALE MIRUNGI

Walaji wengi wa mirungi ni madereva wa masafa marefu na wale wanaosafirisha watalii, huwa wanaamini hawatapata usingizi na pia wataweza kuona barabara vizuri na kukazia mawazo yao katika usukani, madhara yake ni kukosa kitu muhimu katika maisha yaani starehe ya bure – KULALA USINGIZI. Walinzi wa usiku pia wanakula mirungi karibia kila siku nao wakitoa sababu zile zile kama za madereva – nao wanakosa USINGIZI.

KWA NINI WALAJI WA MIRUNGI WENGI WANAKUWA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME?

· Dawa za kulevya siku zote hupunguza nguvu mwilini, misuli inalegea
· Unakosa hamu ya chakula na hivyo kuharibu mfumo mzima wa afya ya mwanume
· Ulaji wa mirungi unadidimiza hamu ya tendo la ndoa
· Kuongeza uwezekano wa kupatwa na vidonda vya tumbo
· Haja kubwa inakuwa ngumu na saa zingine kunakuwa na ukosefu wa haja kubwa kwa muda mrefu
· Matatizo ya ini, hivyo kupekea ukosefu wa uchujaji wa sumu mwilini
· Kukosa usingizi, kupumzika
· Kutokujali familia, mke na watoto
· Kukosa haya na kuwajibika kama baba – na kujiingiza kwenye michepuko
· Kushuka kwa msisimuko wa tendo la ndoa

MADHARA MENGINE YA ULAJI WA MIRUNGI

· Uharibifu wa kinywa na meno, meno yanakuwa meusi naya brown pia kinywa kinatoa harufu mbaya
· Kuuma fizi za meno
· Mama anayetumia mirungi ikiwa anayenyonyesha maziwa yake yanaharibika hivo kumkosesha mtoto lishe bora
· Kutumia muda mwingi katika kula mirungi kunapunguza nguvu kazi na pia masaa ya kupumzika.

Nimatumaini yangu kwamba somo hili litaleta manufaa kwako ili kuokoa TAIFA na adui wa 4 UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

NI PM kama una lolote la kuwasilisha kwangu
 
Back
Top Bottom