Kwanini madereva wa mabasi wanaposhuka mlima Kitonga hujiachia sana ukilinganisha na wale wa malori

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,325
Huwa natafakari nashindwa kujua.. wale wenye malori utakuta wanashuka taratibu sana na kwa makini.. ila wale wa mabasi wanakanyaga tuu utadhani wamebeba pumba za mahindi.

Huwa najiuliza ikitokea breki zinapata hitilafu itakuaje?

Ebu wenye uzoefu na magari tupeni uhakika kinacho fanyika hasa haya magari ya kichina.

Picha ni sweet africa lililo gonga gema hapohapo kitonga baada ya gari kumshinda dereva.
FB_IMG_1558187953476.jpeg
 
Hawa jamaa sijui mapepo yao yanapandaga wakifika huku.Abiri tu unaona hii sehemu ya hatari lakini unakuta dereva hana habari na mara nyingi wamekuwa wakifunga breki za ghafla wakitaka kugongana lakini siku nyingine wakifika hapo bado wanaenda na spidi hiyo hiyo
 
Labda breki za mabasi zipo tofauti na zile za malori.. maana malori utamwona dereva anahangaika na gia zake lakini huyu wa basi ndio anashuka kwa mbwembwe abiria roho juu.
hawa jamaa sijui mapepo yao yanapandaga wakifika huku.Abiri tu unaona hii sehemu ya hatari lakini unakuta dereva hana habari na mara nyingi wamekuwa wakifunga breki za ghafla wakitaka kugongana lakini siku nyingine wakifika hapo bado wanaenda na spidi hiyo hiyo
 
Tabia ya dereva yoyote ni kuwa njia anayoipita mara kwa mara anajenga mazoea nayo na kama kuna sehemu ziko vibaya inafikia mahali woga unamuisha,sasa inapotokea tatizo kama hilo la ghafla anakua hana ujanja tena...
 
Mtu wa lorry kushuka kama basi ni ngumu. Kwanza inamlazimu ashift tu crawler ndo aweze kupanda au kushuka mlima. Maana wangetembelea gia za kawaida kila siku tungekuwa tunawakuta mtaroni...

Kwa upandr wa basi mzigu unarusu ndo maana wanafanya vile. Japo kiasi flani si fair.
 
Hata kama ni kuwahi, kitonga inatisha. Nimepita kwa mara ya kwanza this year kwa basi.. roho ilikua inataka kutoka.. nadhani tulishuka kwa above 50 km/ hr
Pole Tabutupu,
natamani ungejua nilivyokuwa nafundishwa kuwa pale speed yake ni ngapi...…..bora sasa siendi huko tena, maana baadae ziliwekwa patches barabarani kusudi brake ziwe zinashika kirahisi, lakini wale bus drivers ni vijana na yale ma bus huwa yanapanda na kuteremka ule mlima utafikiri ni tambalale, ila biashara ya bus huwa inakwenda kwa swali la je bus hili lina keep time na kufika mapema? na abiria wengi hupenda bus hilo na matokeo ndio haya na ndio maana hata kula pale Kitonga watu huwa wanakula utafikiri kuna moto nyuma yao…….
 
Malori yaliyo mengi akiwa mlimani au mteremkoni anatumia Crawler. Hiyo ni gear kwa ajili ya purpose hiyo, especially kama gari ina mzigo. ndo maana unaona wanatembea taratibu vile.

Nje ya hapo kila kunavoitwa leo malori mengi yangekuwa yanapata ajali...
Labda breki za mabasi zipo tofauti na zile za malori.. maana malori utamwona dereva anahangaika na gia zake lakini huyu wa basi ndio anashuka kwa mbwembwe abiria roho juu.
 
Labda breki za mabasi zipo tofauti na zile za malori.. maana malori utamwona dereva anahangaika na gia zake lakini huyu wa basi ndio anashuka kwa mbwembwe abiria roho juu.
Ni kweli hapo kuna utofauti wa brake,
Mabasi yanatumia disc ambazo hukamata haraka tofauti na malori mengi yenyewe hutumia Upepo kwenye brake ambazo sio za hapo kwa hapo.. Pia kuna malori mengine yanatumia disc ambapo kwa kiasi kikuwa ni zile zenye tanks za mafuta nazo pale kwenye mlima huwa zinakimbia sana tofauti na zile zinazotumia upepo.
 
Hii ndoo ilitakiwa kwa mabasi, maana rate ya breki kufeli hadi sasa bado ni kubwa.
sio kwamba na wao ni wastaarabu sana! no, inawalazimu kupunguza mwendo mana break za malori si za kukamata hapo hapo na ukibeba heavy load break failure risk increases, the only solution is to reduce speed/slow down
 
Mbona bado mabasi nayo breki zinafeli mara nyingi tuu pale kitonga.
Basi hata kama limejaa abiria huwa linakuwa jepesi dereva anacheza nalo tu sasa lori limesheeni mzigo wa mbao au kontena dereva anaendesha kwa adabu anajua kwenye mtelemko akileta mbwembwe mzigo unakuja kufunika kibini ya gari anaweza asitoke.
 
Mkuu ni bora washuke kwa gia kama malori kuliko kupoteza maisha ya watu
Mtu wa lorry kushuka kama basi ni ngumu. Kwanza inamlazimu ashift tu crawler ndo aweze kupanda au kushuka mlima. Maana wangetembelea gia za kawaida kila siku tungekuwa tunawakuta mtaroni...

Kwa upandr wa basi mzigu unarusu ndo maana wanafanya vile. Japo kiasi flani si fair.
 
Malori yanatumia break za upepo sasa akishuka speed atatumia break sana na upepo ukikata ndo basi tena kwenye basi sijajua
 
Ni kweli hapo kuna utofauti wa brake,
Mabasi yanatumia disc ambazo hukamata haraka tofauti na malori mengi yenyewe hutumia Upepo kwenye brake ambazo sio za hapo kwa hapo.. Pia kuna malori mengine yanatumia disc ambapo kwa kiasi kikuwa ni zile zenye tanks za mafuta nazo pale kwenye mlima huwa zinakimbia sana tofauti na zile zinazotumia upepo.
Zote zinatumia upepo..... Either disk brakes or drum brakes.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom