Kwanini Madaktari huandika mwandiko usiosomeka? Husababishia vifo watu 7000 kwa mwaka Marekani

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
5,497
Nakumbuka Tunapoanza darasa la kwanza hadi la Tatu, Nguvu nyingi huwa inapelekwa kwenye kujua kusoma na kuandika. Sijajua sababu na wanajifunza miandiko hii kwakati gani katika carer yao.

Kwa Mujibu wa ACADEMICS OF SCIENCE INSTITUTE OF MEDICINE (IOM) report ya kitafiti iliyofanyika July 2006, Kwa nchi ya Marekani pekee Kwa maelezo hayo yasioyomeka Yanasababisha VIfo vya watu sio chini ya 7000, Na watu Million 1.3 Kujeruhiwa kwa makosa kila mwaka.

NINI KILIFANYIKA;
Coalition of Health Care na Technology Companies walianzisha kitu kinaitwa National e-prescribing Patient Safety Initiative(NEPSI)

mfano
Resize%20of%20scan%2003.jpg

mwenye maarifa zaidi katika hili msaada
source
More than 7,000 People Every Year Die from Doctors' Poor Handwriting
Doctors' sloppy handwriting kills 7,000 a year; national e-prescription campaign launched
 
Fikiria dr. Tangu afike ofisini asubuhi mpaka anatoka jioni amekuwa ameandika kurasa ngapi? Kwa sababu kila mgonjwa taarifa zake inabidi ziandikwe kwa future reference au kwa watumishi wengine kama maelekezo ya ziada.

Nafikiri nikatika huu muktadha wanaandika mpaka wanachoka na kinachobaki ni kuscrible. Wangeamua kuandika mwandiko mzuri wa darasani watachelewa kuwahudumia wagonjwa na pia inakuwa boring.
 
Huu ni uongo mtupu..kwani nchi nyingi sana duniani mfumo wa afya kuanzia mapokezi mpaka kuandikiwa dawa ni wa Computer..Labda kama useme hizo computer zao zina miandiko mibaya
 
Unaishi Tanzania mkuu?

Pale muhimbili umeshawahi kuona dr. anaandika Rx kwa computer? Au unaona raha kutype na kusema uongo.
 
  • Thanks
Reactions: ora
Nakumbuka Tunapoanza darasa la kwanza hadi la Tatu, Nguvu nyingi huwa inapelekwa kwenye kujua kusoma na kuandika. Sijajua sababu na wanajifunza miandiko hii kwakati gani katika carer yao.

Kwa Mujibu wa ACADEMICS OF SCIENCE INSTITUTE OF MEDICINE (IOM) report ya kitafiti iliyofanyika July 2006, Kwa nchi ya Marekani pekee Kwa maelezo hayo yasioyomeka Yanasababisha VIfo vya watu sio chini ya 7000, Na watu Million 1.3 Kujeruhiwa kwa makosa kila mwaka.

NINI KILIFANYIKA;
Coalition of Health Care na Technology Companies walianzisha kitu kinaitwa National e-prescribing Patient Safety Initiative(NEPSI)

mfano
Resize%20of%20scan%2003.jpg

mwenye maarifa zaidi katika hili msaada
source
More than 7,000 People Every Year Die from Doctors' Poor Handwriting
Doctors' sloppy handwriting kills 7,000 a year; national e-prescription campaign launched
Kwa US siku hizi kila kitu wanatype katika computer.
 
Huwa hawatakia wewe usiye na expirience usome usije ukaenda kujinunulia midawa ukanywa ukajifia hasa huku kwenye nchi maskini lakini USA wanako type na mashine hata ukisoma huwezi kwenda kujinunulia midawa tu lazima iwe imethibitishwa na dr
 
Hakuna chuo cha udaktari nchini Tanzania wanafundisha somo la mwandiko ili mgonjwa asijue kilichoandikwa.

Kwa taarifa tu ni kwamba dr. Anatakiwa asimfiche mgonjwa ugonjwa wake. Hayo ya kusema ili mgonjwa asijue ni hear say.
 
Mbn wao kwa wao wanasoma na wanaelewa vilivyoandikwa? Hamna cha mwandiko mbaya pale
 
Ni kweli. Watu wanashindwa kuelewa dawa moja ina generic name na brand name. Sasa kama mtu amezoea panadol halafu dr. akiandika paracetamol unakuwa huelewi.

Kwa bongo hawa ndugu zetu wanaandika sana. Tena sana. Kwa hivyo hata mwandiko wao unabadilika.

Siri moja ya kujua mwandiko wa dr. Ni herufi za mwanzoni na mwishoni.
 
Yeah mtu ht akiona Pameandikwa PCM kwa kuchalazwa yy hawez jua km ni paracetamol ataona nyota tu
 
Wanaandika mwandiko mbaya ili mgonjwa asiweze kuusoma.
Tatizo inatokea pale mtoa dawa sio daktari aliyeandika hiyo karatasi, Hapo ndip unaweza kupewa kitu kingine. Hii imetokea sehemu nyingi. Kuna jamaa Dr mmoja aliandika hizo micharango akapeleka hiyo priscription phamacy hospitalini cha ajabu anamuuliza yule dada Kimeandikwa nini pale dada anasema yeye sio kazi yake kazi yake ni kutoa dawa basi hayo mengine akamuulize daktari aliyemuandikia. Kwa elimu hizi za mwendokasi kujiongeza kidogo ukajua nini kinaendelea kama inawezekana sio mbaya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom