Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
M. M. Mwanakijiji
Wakati wa ukoloni wanaharakati za kisiasa nchini wakiongozwa na TANU walijenga hoja mbalimbali za kutaka dhulma mbalimbali ziondolewe na utawala wa kikoloni. Siyo kupitia vyama vya kisiasa tu bali pia vyama vya wafanyakazi. Katika historia yetu kuna matukio kama mgomo wa wafanyakazi wa bandarini (ambao kina Sykes wanakumbwa kwao sana) umeacha historia ya nguvu ya wafanyakazi nchini. Mgomo wa kugomea bia nao ulikuwa ni wa harakati za shinikizo la kisiasa. Mgomo wa bandarini ndio ulimvuvia sana Mzee Shafi Adam Shafi kuandika lile simulizi la KULI (natumaini bado vijana wetu wanakisoma kitabu hiki).
TANU baada ya kushika fikra za ukombozi hakikubali mbinu mbalimbali za wakoloni kuzuia vuguvugu la uhuru nchini. Kwa mfano, Serikali ilipojaribu kukataza watumishi wa umma kujishughulisha na siasa - baadhi yao waliamua kuachana na utumishi wa umma (kina Nyerere, Kawawa na wengine) kuliko kuacha harakati za kisiasa. Hata kukataza siasa maeneo ya kazi na vyuo ilikuwa ni vitu vilivyopingwa vikali. Wakoloni walitumia pia mbinu ya kulazimisha vibali lakini kuna wakati kina Nyerere walisema watafanya maandamano yao hata bila vibali kwani ni haki yao.
Kwa wanaojua historia yetu maandamani nchini ya kisiasa hajaanzishwa na CHADEMA wala CUF; Maandamano ya kupinga serikali au kuishinikiza serikali nchini hayaasisiwa na kina Dr. Slaa au Mbowe! Hatakari za kutumia maandamano, migomo, mikutano ya hadhara yameanzishwa Tanzania na kuboreshwa sana nchini ya TANU. Kuanzia kwenye mgogoro wa MERU, mgogoro wa Mwanza, na hata mwamko wa Zanaki kule kote kulitumiwa mikutano ya hadhara, maandamano, na migomo kama mbinu halali ya kidemokrasia ya kuishinikiza serikali.
Kuanzia Kenya hadi Afrika ya Kusini, Zimbabwe hadi Zambia, Tanganyika hadi Zanzibar migomo na maandamano yamekuwa ni mbinu halali ya kisiasa ya kuishinikiza serikali na hata kuikatalia serikali kufanya mambo ambayo wananchi wanaona hayana manufaa kwao au mambo ambayo wanaona ni ya kiukandamizaji. Kumbe basi kama maandamano yalikuwa halali kushinikiza serikali wakati wa mkoloni kupinga sheria mbaya, udhalimu au vitendo vya kutumia nguvu (kama mgogoro wa Meru na ule wa Mwanza) ni wazi kuwa mbinu hizo zaweza (na mwingine anaweza kusema zapaswa) kutumika tena kwa namna moja au nyingine.
Katika nchi za kidemokrasia - zilioendelea na zinazojaribu kuendelea - maandamano ya amani, mikutano ya hadhara na mashinikizo ya kisiasa kwa watawala ni mbinu halali za kisiasa na kidemokrasia kufikia malengo ya kisiasa. Wananchi wanafahamu kabisa kuwa njia za kawaida za kuwashawishi watawala ni kupitia kura, mikutano na mazungumzo ya kawaida; lakini vile vile wanafahamu kuwa kuna wakati watawala hawasikii wala hawaambiliki na pale wanapojifanya wanaambilika hupindisha maneno na mizunguko na kusababisha kukata tamaa zaidi au kukasirika. Wengi tuliyaona haya kule Misri, Tunisia na tunaendelea kuyaona nchi nyingine. Hata Marekani kwa mfano serikali zinajikuta zinapata mashinikizo zaidi kwa njia mbadala za kidemokrasia baada ya njia za kawaida kushindikana. Wengi tumeona hili mapema mwaka huu kwenye serikali ya jimbo la Minnesota Marekani, tumeyaona Athens, Ugiriki na hata Uhispania. Demokrasia kumbe siyo tu kuwakubalia watawala bali pia kuwakatalia na kuwagomea.
Kinachosikitisha sasa kwa nchi yetu ni kuwa ni kama tumesahau historia yetu. Mambo ambayo tuliyakataa wakati wa Mkoloni leo tunajaribu kuyakubali na kuyatungia sheria. Wakoloni walikataza watu wetu kushiriki siasa kwa sababu ni watumishi wa umma, leo tunakataza. Wakati siasa iliruhusiwa hadi mahali pa kazi wakati wa chama kimoja leo wafanyakazi kuonekana kwenye siasa inakuwa ni jambo la ajabu. Wakati migomo ilichangia kulazimisha serikali ya kikoloni kubadilisha sera zake - kama kwenye tukio la mgomo wa bandarini - leo hii wafanyakazi wa umma wakigoma wanaitwa "mbayuwayu".
Maandamano kinyume ya inavyofikiriwa hayana lengo la kumdhalilisha mtu yeyote. Maandamano mazuri ni yale ambayo yanasimama kupinga sera, vitendo na mwitikio fulani wa serikali. Maandamano siyo yale ya kumpinga mtu kama mtu isipokuwa kama mtu huyo ndiye msimamizi wa sera, vitendo, na mwitikio huo na ya kuwa maamuzi yake yanaweza kubadilisha mwelekeo wa jambo fulani.
Maandamano mazuri mara zote ni ya amani yenye kujali heshima, utu, haki, na usawa. Kwa maneno mengine maandamano ambayo yanalengo la kunyanyasa watu ni maandamano ambayo kwenye zisizoyazoea yanaweza kuchukuliwa kama ugomvi. Lakini uzuri mmoja wa demokrasia ni kuwa maandamano si lazima yawe na sura tunayoipenda sisi; ndio maana maandamano huwa na mabango ya kejeli, vikaragosi na hata maneno ya madongo ya wazi. Kwani maandamano pia yanaendana kabisa na uhuru wa maoni. Huwezi kuwa na maandamano au migomo ya haki kama huruhusu uhuru wa maoni vile vile.
Kumbe basi jukumu la serikali ni kuhakikisha yote mawili; kwamba maandamano yanafanyika katika mazingira ya usalama na kuwa haki ya wananchi kutoa maoni yao inalindwa - hata kama maoni hayo yanakera watawala. Wakati wa ukoloni, wakoloni waliandika sheria ambazo ni mbaya sana na ambazo bado tunazo vitabuni. Sheria kwamba ni makosa kuichukia serikali! au kuzungumza maneno ambayo yanaweza kuwafanya watu waichukie serikali. Hivyo, wakoloni walitumia sheria hizo hadi kumtia hukumuni Nyerere na waandishi kadhaa wa magazeti wa zama hizo (kina Makange kwa wanaokumbuka). Watawala wa kikoloni hawakupenda watu wawachukue kwa sababu walikuwa wanafanya "mambo mengi mazuri".
Hawakuelewa kwanini wanachi wanawapinga sana wakati wamejenga mabarabara, shule, hospitali na hata kutoa nafasi za masomo majuu! Hawakuelwa kwanini wafanyakazi walikuwa wanalalamika sana kuhusu ujira wakati walikuwa wanalipwa kuliko watu wengine wengi tu nchini. Kitu ambacho hawakukielewa na ambacho tunaona kinajirudia miaka hamsini baadaye huko Mashariki ya kati na hata nchini mwetu ni kuwa utu wa mwanadamu hauuzwi kwa lami! Mfungwa aliyewekwa kwenye jumba la fahari bado ni mtumwa! Huwezi kumfunga mtu (physically, emotionally or mentally) huku unampa gari, nyumba na umeme na kumwambia "si ufurahie utumwa wako mzuri"? Mtumwa hata avishwe suti na kupewa saa ya kiswisi bado ni mtumwa. Unaweza kumuita "msaidizi maalum" a "Afisa Mbadala wa nyumbani" lakini bado ni mtumwa kwa kadiri ya kwamba hana uwezo wa kufikiri atakavyo, kutenda atakavyo au kwenda atakako bila baraka za mwenye nyumba. Kwa kadiri ya kwamba utu wa mtu umepigwa pingu mtu huyu si huru hata kama amesoma na kuwa na maisha fulani ahueni. Hili ni somo ambalo Gaddafi hakulisoma vizuri au hata Bashir Assad hakulisoma vizuri.
Kwa ufupi, tunajiuliza maandamano yana ulazima kweli? Well.. kama yalikuwa na ulazima miaka hamsini iliyopita katika mazingira karibu yale yale ya kisiasa kwanini yasiwe na ulazima leo hii? Au mwingine anauliza kwanini watu wasiandamane tu na wasubiri kuona serikali inafanya kazi yake? Je ni kwlei kwamba bila kuwawekea shinikizo wakoloni wakoloni wangekubali tu kuondoka na kubadilika kwa sababu ya wema wao? Kama wananchi wa Afrika ya Kusini wasingetumia maandamano, migomo na hata harakati za nguvu kweli utawala wa Kikaburu ungeamua tu siku moja kusema "well lets give them some more rights and human dignity"? Kwamba kama maelfu ya vijana wa Misri wasingesimama pale Tahrir square usiku kucha na mchana kweli Mubarak angeamua tu kufanya mabadiliko ya kisiasa ambayo alishindwa kuyafanya kwa miaka thelathini nyuma yake?
Jawabu liko wazi. Kuna wakati wananchi wanajikuta wanalazimika kuwapa msukumo na shinikizo watawala wao. Swali kubwa ni je watawala wanaitikia vipi? Jibu la swali hilo ni tofauti kati ya mabadiliko kwa njia ya amani na mabadiliko kwa machozi na damu. Natumaini Watanzania tunajua kutofautisha kati ya hayo mawili. Tunajua historia yetu imetuonesha kuwa watawala wa kikoloni hawakutaka kutumia sana matumizi ya nguvu (hasa kipindi cha Mwingereza) na matokeo yake ni kupatikana kwa uhuru kwa njia ya amani.
Je tunapoanza kuelekea miaka hamsini ijayo, tutaweza kuleta mabadiliko ya kisiasa bila kutumia migomo, maandamano, na mashinikizo ya aina hiyo ya kisiasa? Je watawala wetu watakubali kuona haja ya mabadiliko bila kulazimishwa kufanya hivyo na wanaharakati? Kama wanaweza kwanini hawakuweza kufanya hivyo miaka ishirini iliyopita hadi ndani ya miezi hii michache ambapo maandamano yamekuwa yakiwasimanga kila kukicha?
Je Tanzania mpya bila maandamano, migomo, na mashinikizo ya kisiasa inawezekana? Je Tanzania mpya bila dola kutumia nguvu dhidi ya raia wake kuzima harakati zao inawezekana? Kwanini hadi leo hii kwa mfano viongozi wa CCM wamekataa na hawajawa tayari kukaa meza moja na CDM kuangalia mustakabali wa nchi yetu kisiasa na badala yake wanagombania suala la maandamano? Yawezekana kuwa mpasuko uliopo ndani ya Tanzania sasa hivi unakaribia kabisa ule mpasuko uliokuwepo wakati wa ukoloni? Katika mazingira kama hayo walioko madarakani wakitumia nguvu zaidi ili wakae madarakani nani atawalaumu? Na je wale walioko nje ya madaraka wakitumia nguvu zaidi ya maandamano na migomo na mikutano kulazimisha mabadiliko nani atawalaumu. Yawezekena kumbe basi historia imejirudia tena?