Kwanini Maandamano leo hii yanakuwa nongwa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
M. M. Mwanakijiji

Wakati wa ukoloni wanaharakati za kisiasa nchini wakiongozwa na TANU walijenga hoja mbalimbali za kutaka dhulma mbalimbali ziondolewe na utawala wa kikoloni. Siyo kupitia vyama vya kisiasa tu bali pia vyama vya wafanyakazi. Katika historia yetu kuna matukio kama mgomo wa wafanyakazi wa bandarini (ambao kina Sykes wanakumbwa kwao sana) umeacha historia ya nguvu ya wafanyakazi nchini. Mgomo wa kugomea bia nao ulikuwa ni wa harakati za shinikizo la kisiasa. Mgomo wa bandarini ndio ulimvuvia sana Mzee Shafi Adam Shafi kuandika lile simulizi la KULI (natumaini bado vijana wetu wanakisoma kitabu hiki).

TANU baada ya kushika fikra za ukombozi hakikubali mbinu mbalimbali za wakoloni kuzuia vuguvugu la uhuru nchini. Kwa mfano, Serikali ilipojaribu kukataza watumishi wa umma kujishughulisha na siasa - baadhi yao waliamua kuachana na utumishi wa umma (kina Nyerere, Kawawa na wengine) kuliko kuacha harakati za kisiasa. Hata kukataza siasa maeneo ya kazi na vyuo ilikuwa ni vitu vilivyopingwa vikali. Wakoloni walitumia pia mbinu ya kulazimisha vibali lakini kuna wakati kina Nyerere walisema watafanya maandamano yao hata bila vibali kwani ni haki yao.

Kwa wanaojua historia yetu maandamani nchini ya kisiasa hajaanzishwa na CHADEMA wala CUF; Maandamano ya kupinga serikali au kuishinikiza serikali nchini hayaasisiwa na kina Dr. Slaa au Mbowe! Hatakari za kutumia maandamano, migomo, mikutano ya hadhara yameanzishwa Tanzania na kuboreshwa sana nchini ya TANU. Kuanzia kwenye mgogoro wa MERU, mgogoro wa Mwanza, na hata mwamko wa Zanaki kule kote kulitumiwa mikutano ya hadhara, maandamano, na migomo kama mbinu halali ya kidemokrasia ya kuishinikiza serikali.

Kuanzia Kenya hadi Afrika ya Kusini, Zimbabwe hadi Zambia, Tanganyika hadi Zanzibar migomo na maandamano yamekuwa ni mbinu halali ya kisiasa ya kuishinikiza serikali na hata kuikatalia serikali kufanya mambo ambayo wananchi wanaona hayana manufaa kwao au mambo ambayo wanaona ni ya kiukandamizaji. Kumbe basi kama maandamano yalikuwa halali kushinikiza serikali wakati wa mkoloni kupinga sheria mbaya, udhalimu au vitendo vya kutumia nguvu (kama mgogoro wa Meru na ule wa Mwanza) ni wazi kuwa mbinu hizo zaweza (na mwingine anaweza kusema zapaswa) kutumika tena kwa namna moja au nyingine.

Katika nchi za kidemokrasia - zilioendelea na zinazojaribu kuendelea - maandamano ya amani, mikutano ya hadhara na mashinikizo ya kisiasa kwa watawala ni mbinu halali za kisiasa na kidemokrasia kufikia malengo ya kisiasa. Wananchi wanafahamu kabisa kuwa njia za kawaida za kuwashawishi watawala ni kupitia kura, mikutano na mazungumzo ya kawaida; lakini vile vile wanafahamu kuwa kuna wakati watawala hawasikii wala hawaambiliki na pale wanapojifanya wanaambilika hupindisha maneno na mizunguko na kusababisha kukata tamaa zaidi au kukasirika. Wengi tuliyaona haya kule Misri, Tunisia na tunaendelea kuyaona nchi nyingine. Hata Marekani kwa mfano serikali zinajikuta zinapata mashinikizo zaidi kwa njia mbadala za kidemokrasia baada ya njia za kawaida kushindikana. Wengi tumeona hili mapema mwaka huu kwenye serikali ya jimbo la Minnesota Marekani, tumeyaona Athens, Ugiriki na hata Uhispania. Demokrasia kumbe siyo tu kuwakubalia watawala bali pia kuwakatalia na kuwagomea.

Kinachosikitisha sasa kwa nchi yetu ni kuwa ni kama tumesahau historia yetu. Mambo ambayo tuliyakataa wakati wa Mkoloni leo tunajaribu kuyakubali na kuyatungia sheria. Wakoloni walikataza watu wetu kushiriki siasa kwa sababu ni watumishi wa umma, leo tunakataza. Wakati siasa iliruhusiwa hadi mahali pa kazi wakati wa chama kimoja leo wafanyakazi kuonekana kwenye siasa inakuwa ni jambo la ajabu. Wakati migomo ilichangia kulazimisha serikali ya kikoloni kubadilisha sera zake - kama kwenye tukio la mgomo wa bandarini - leo hii wafanyakazi wa umma wakigoma wanaitwa "mbayuwayu".

Maandamano kinyume ya inavyofikiriwa hayana lengo la kumdhalilisha mtu yeyote. Maandamano mazuri ni yale ambayo yanasimama kupinga sera, vitendo na mwitikio fulani wa serikali. Maandamano siyo yale ya kumpinga mtu kama mtu isipokuwa kama mtu huyo ndiye msimamizi wa sera, vitendo, na mwitikio huo na ya kuwa maamuzi yake yanaweza kubadilisha mwelekeo wa jambo fulani.

Maandamano mazuri mara zote ni ya amani yenye kujali heshima, utu, haki, na usawa. Kwa maneno mengine maandamano ambayo yanalengo la kunyanyasa watu ni maandamano ambayo kwenye zisizoyazoea yanaweza kuchukuliwa kama ugomvi. Lakini uzuri mmoja wa demokrasia ni kuwa maandamano si lazima yawe na sura tunayoipenda sisi; ndio maana maandamano huwa na mabango ya kejeli, vikaragosi na hata maneno ya madongo ya wazi. Kwani maandamano pia yanaendana kabisa na uhuru wa maoni. Huwezi kuwa na maandamano au migomo ya haki kama huruhusu uhuru wa maoni vile vile.

Kumbe basi jukumu la serikali ni kuhakikisha yote mawili; kwamba maandamano yanafanyika katika mazingira ya usalama na kuwa haki ya wananchi kutoa maoni yao inalindwa - hata kama maoni hayo yanakera watawala. Wakati wa ukoloni, wakoloni waliandika sheria ambazo ni mbaya sana na ambazo bado tunazo vitabuni. Sheria kwamba ni makosa kuichukia serikali! au kuzungumza maneno ambayo yanaweza kuwafanya watu waichukie serikali. Hivyo, wakoloni walitumia sheria hizo hadi kumtia hukumuni Nyerere na waandishi kadhaa wa magazeti wa zama hizo (kina Makange kwa wanaokumbuka). Watawala wa kikoloni hawakupenda watu wawachukue kwa sababu walikuwa wanafanya "mambo mengi mazuri".

Hawakuelewa kwanini wanachi wanawapinga sana wakati wamejenga mabarabara, shule, hospitali na hata kutoa nafasi za masomo majuu! Hawakuelwa kwanini wafanyakazi walikuwa wanalalamika sana kuhusu ujira wakati walikuwa wanalipwa kuliko watu wengine wengi tu nchini. Kitu ambacho hawakukielewa na ambacho tunaona kinajirudia miaka hamsini baadaye huko Mashariki ya kati na hata nchini mwetu ni kuwa utu wa mwanadamu hauuzwi kwa lami! Mfungwa aliyewekwa kwenye jumba la fahari bado ni mtumwa! Huwezi kumfunga mtu (physically, emotionally or mentally) huku unampa gari, nyumba na umeme na kumwambia "si ufurahie utumwa wako mzuri"? Mtumwa hata avishwe suti na kupewa saa ya kiswisi bado ni mtumwa. Unaweza kumuita "msaidizi maalum" a "Afisa Mbadala wa nyumbani" lakini bado ni mtumwa kwa kadiri ya kwamba hana uwezo wa kufikiri atakavyo, kutenda atakavyo au kwenda atakako bila baraka za mwenye nyumba. Kwa kadiri ya kwamba utu wa mtu umepigwa pingu mtu huyu si huru hata kama amesoma na kuwa na maisha fulani ahueni. Hili ni somo ambalo Gaddafi hakulisoma vizuri au hata Bashir Assad hakulisoma vizuri.

Kwa ufupi, tunajiuliza maandamano yana ulazima kweli? Well.. kama yalikuwa na ulazima miaka hamsini iliyopita katika mazingira karibu yale yale ya kisiasa kwanini yasiwe na ulazima leo hii? Au mwingine anauliza kwanini watu wasiandamane tu na wasubiri kuona serikali inafanya kazi yake? Je ni kwlei kwamba bila kuwawekea shinikizo wakoloni wakoloni wangekubali tu kuondoka na kubadilika kwa sababu ya wema wao? Kama wananchi wa Afrika ya Kusini wasingetumia maandamano, migomo na hata harakati za nguvu kweli utawala wa Kikaburu ungeamua tu siku moja kusema "well lets give them some more rights and human dignity"? Kwamba kama maelfu ya vijana wa Misri wasingesimama pale Tahrir square usiku kucha na mchana kweli Mubarak angeamua tu kufanya mabadiliko ya kisiasa ambayo alishindwa kuyafanya kwa miaka thelathini nyuma yake?

Jawabu liko wazi. Kuna wakati wananchi wanajikuta wanalazimika kuwapa msukumo na shinikizo watawala wao. Swali kubwa ni je watawala wanaitikia vipi? Jibu la swali hilo ni tofauti kati ya mabadiliko kwa njia ya amani na mabadiliko kwa machozi na damu. Natumaini Watanzania tunajua kutofautisha kati ya hayo mawili. Tunajua historia yetu imetuonesha kuwa watawala wa kikoloni hawakutaka kutumia sana matumizi ya nguvu (hasa kipindi cha Mwingereza) na matokeo yake ni kupatikana kwa uhuru kwa njia ya amani.

Je tunapoanza kuelekea miaka hamsini ijayo, tutaweza kuleta mabadiliko ya kisiasa bila kutumia migomo, maandamano, na mashinikizo ya aina hiyo ya kisiasa? Je watawala wetu watakubali kuona haja ya mabadiliko bila kulazimishwa kufanya hivyo na wanaharakati? Kama wanaweza kwanini hawakuweza kufanya hivyo miaka ishirini iliyopita hadi ndani ya miezi hii michache ambapo maandamano yamekuwa yakiwasimanga kila kukicha?

Je Tanzania mpya bila maandamano, migomo, na mashinikizo ya kisiasa inawezekana? Je Tanzania mpya bila dola kutumia nguvu dhidi ya raia wake kuzima harakati zao inawezekana? Kwanini hadi leo hii kwa mfano viongozi wa CCM wamekataa na hawajawa tayari kukaa meza moja na CDM kuangalia mustakabali wa nchi yetu kisiasa na badala yake wanagombania suala la maandamano? Yawezekana kuwa mpasuko uliopo ndani ya Tanzania sasa hivi unakaribia kabisa ule mpasuko uliokuwepo wakati wa ukoloni? Katika mazingira kama hayo walioko madarakani wakitumia nguvu zaidi ili wakae madarakani nani atawalaumu? Na je wale walioko nje ya madaraka wakitumia nguvu zaidi ya maandamano na migomo na mikutano kulazimisha mabadiliko nani atawalaumu. Yawezekena kumbe basi historia imejirudia tena?
 
wameangalia tunisia na misri ndo wakatambua kuwa maandamano yanaweza yakawamwagia ugali kwani wao lengo lao ni kutawala milele.kwa hiyo lazima watumie nguvu yote na maneno ya uongo ya kila aina kupambana na maandamano.mimi naona wameshachelewa.sisi hatuna uwezo wa kutumia silaha kupingana na uonevu,upendeleo,rushwa na ubadhilifu.tunachofanya ni kuandamana.mia
 
Mzee mwanakijiji nimeisoma post yako, ina mengi ya kucomment lakini kwa sasa nakumbuka machache (nimetandika kabia hapa, akili inarukaruka)...

Kwanza, Tanzania kuna maandamano mengi kila mwaka (siku ya wanawake, wafanyakazi, kuchangia chakula, uhuru wa Tanganyika, kushinikiza serikali, n.k. kati ya haya yote yaliyoonekana mabaya ni ya kushinikiza serikali. Yaliyoongezewa neno vurugu, ni ya kushinikiza serikali. Swali ni kwa nini? Moja wapo ya jibu ni kuwa kuishinikiza serikali ni kuichongea kwa mwajiri wake (wananchi). Watu wanaandamana ili waonekane na watu fulani. Sidhani kama kuna watu wanaweza kwenda kuandamana ndani ya mbuga ya serengeti, ili waonekane na nyumbu. Maandamano ya kuishinikiza serikali yanafanya ili wananchi waone, na waichukie serikali. ili serikali ione na ijue inachukiwa na wananchi pia.

MMKJ, kinachofanywa na CDM kuandamana sio kigeni hapa TZ, na duniani kote, lakini pia kinachofanywa na CCM kuyapinga, kuyahujumu na kuyazuia maandamano hayo sio kigeni hapa Tz na duniani kwa ujumla. Kama una mifano naamini itakuwa michache, kuwa hapa duniani kuna mahali yaliwahi kufanyika maandamano ya kupinga au kushinikiza utawala fulani, then utawala huo ukayaunga mkono na kuyapa support maandamano hayo. Hata hivyo maandamano yote yaliyowahi kuleta mafanikio kwa watetewaji yalileta mafanikio hayo licha ya kupingwa na washinikizwaji. So, kwa sisi wananchi ambao tunaamini kuwa maandamano yanayofanywa na CDM au kundi lolote ambayo yana nia ya kutetea maslahi yetu, tutakuwa watu wa ajabu kama tukitegemea "kkukosa" upinzani kutoka kwa tunaowashikiza.

Ninachotaka kusema ni kuwa, kufanywa kwa maandamano Tz sio kitu cha ajabu, kupingwa kwa maandamano hayo sio kitu cha ajabu, matokeo ya maandamano hayo sio kitu cha ajabu.

Hivi mwanakijiji unaweza ku-imagine miaka kadhaa ijayo CDM wakiwa wanatawala Tz (naamini hiyo siku ipo), watakuwa wanatumia jeshi la polisi kuwapiga mabomu waandamanaji wa vyama vya upinzani watakaokuwa wanatutetea wananchi? Unaweza ku-imagine CDM watakuwa wanawatumia wakuu wa wilaya, na wasimamizi wa uchaguzi kuchakachua matokeo? Kama hau-imagine hayo, then better you quit politics very now...
 
Tuko, nimependa take yako. Katika mazingira ambayo yote mawili yanawezekana ni kwa namna gani basi tunaweza kufanya mambo yote mawili bila kumwaga damu au kuleta madhara kwa watu na vitu?
 
Anything against CCM ni nongwa at last in their book of thought! Leo CCM ina redio (redio uhuru), chadema wakianzisha yao Usijeshangaa maoni kama ooh! hizi redio zinachochea uvunjifu wa amani, redio sio maendeleo, hizo hela za edio si wangepeleka kwenye maendeleo!!!!!!!!
 
Maandamano si kitu kibaya katika dunia hii na hasa kwa nchi zisizo na mpangilio wa kiuongozi kama yetu..
Kwanza ni njia mbadala au sahihi ya kufikisha manug'uniko ya watu, au kutokuridhika kwa watu kutokana na mwenendo wa mambo ya kimaslahi..
Pia ni kipimo na changamoto ya utendaji kazi wa uongozi na vyombo vya serikali husika.
Si hivyo tu bali ktk njia ya maandamano ni rahisi kuibua hisia, fikra, machungu au mawazo walonayo wananchi na hii husaidia uongozi kujifunza, kugundua na hali kadhalika inaweza ikawa njia ya kujirekebisha..
Maandamano kama kusanyiko au matembezi ya watu wenye nia moja ni msingi ktk nchi yeyote yenye watu wenye ufahamu na kujitambua..
Kupinga au kusanifu ufanyikaji wa maandamano ni kutojua nini maana ya uongozi na utekelezaji wa kero za wananchi..
Katika maandamano ndiko kulo na haki na hakika siku zote ambaye hataki ndio mbaya na mfilisi wa haki..
Tubadilike na tuamini ktk hili..
Tanzania itaendelea.
 
Ratiba Ya Safari Kwenda Kwenye Maandamano dhidi ya Vasco-Dagama (Jakaya Mrisho Kikwete). Kila kituo kitakuwa na Basi Moja. Mabasi Yote yatakuwa Coach Amerika. Hii ni kwa WAZALENDO na Mashujaa wote waliothibitisha kuja. Akija Basi maandamano Yataanza Tarehe 23-25

  • Atlanta (Texas, Alabama, Kansas etc)–DC September 22. 9pm (50 confirmed) Meeting Point : 2424 Piedmont Road Northeast, Atlanta
  • Columbus Ohio (Pennsylvania, Maryland and Midwest) September 22, 11pm (58 confirmed) Meeting Point : 111 East Town Street, Columbus
  • New-York (New-Jersey, CT, Rhode Island na Majimbo ya Juu pamoja na Canada) September 23, 5am (38 confirmed) Meeting Point : 625 8th Avenue, Manhattan (Next To Bank of America)
Kwa watakao Kuja kivyao, Tunakutana 1707 L Street NW, Washington D.C., DC 20003, (202) 293-7755. Ikiwa Vasco Dagama atakuja Basi tunakumbana naye uso kwa uso Tarehe 23/09/2011. Kuna wapelelezi wetu ambao watakuwemo kwenye DICOTA. Atakapofika Vasco Dagama wote tutaingia either kwenye ukumbi au nje ya Ukumbi Ambayo anwani yake ni Hapa chini. Asipokuja, basi hatutakuwa na budi kutokufika kwenye ukumbi. Tutawaachia DICOTA waendelee na shuguli yao.

Mabasi hayo hayo ndio yatakayowarudisha. Chakula na malazi yatatolewa kuanzia Tarehe 23-25 Mchana. Muda wa mabadiliko umefika, huu ni mwanzo tu. Mashujaa wengine wanatayarisha mikakati Tanzania. Moto mtindo mmoja Kote kote. Wangine watasema hii ni kazi ya CHADEMA. Ukweli ni Kwamba sisi ni CCM. Tumechoshwa na Kikwete. Kikwete atapita ila Tanzania itabadi, siyo Chadema, CCM, CUF au UDP. Wote ni Watanzania

Marriott Washington Dulles Airport hotel
45020 Aviation Drive
Dulles, Virginia 20166, USA.
Tel: 1-703-471-9500

Mzee mwanakijiji nimeisoma post yako, ina mengi ya kucomment lakini kwa sasa nakumbuka machache (nimetandika kabia hapa, akili inarukaruka)...

Kwanza, Tanzania kuna maandamano mengi kila mwaka (siku ya wanawake, wafanyakazi, kuchangia chakula, uhuru wa Tanganyika, kushinikiza serikali, n.k. kati ya haya yote yaliyoonekana mabaya ni ya kushinikiza serikali. Yaliyoongezewa neno vurugu, ni ya kushinikiza serikali. Swali ni kwa nini? Moja wapo ya jibu ni kuwa kuishinikiza serikali ni kuichongea kwa mwajiri wake (wananchi). Watu wanaandamana ili waonekane na watu fulani. Sidhani kama kuna watu wanaweza kwenda kuandamana ndani ya mbuga ya serengeti, ili waonekane na nyumbu. Maandamano ya kuishinikiza serikali yanafanya ili wananchi waone, na waichukie serikali. ili serikali ione na ijue inachukiwa na wananchi pia.

MMKJ, kinachofanywa na CDM kuandamana sio kigeni hapa TZ, na duniani kote, lakini pia kinachofanywa na CCM kuyapinga, kuyahujumu na kuyazuia maandamano hayo sio kigeni hapa Tz na duniani kwa ujumla. Kama una mifano naamini itakuwa michache, kuwa hapa duniani kuna mahali yaliwahi kufanyika maandamano ya kupinga au kushinikiza utawala fulani, then utawala huo ukayaunga mkono na kuyapa support maandamano hayo. Hata hivyo maandamano yote yaliyowahi kuleta mafanikio kwa watetewaji yalileta mafanikio hayo licha ya kupingwa na washinikizwaji. So, kwa sisi wananchi ambao tunaamini kuwa maandamano yanayofanywa na CDM au kundi lolote ambayo yana nia ya kutetea maslahi yetu, tutakuwa watu wa ajabu kama tukitegemea "kkukosa" upinzani kutoka kwa tunaowashikiza.

Ninachotaka kusema ni kuwa, kufanywa kwa maandamano Tz sio kitu cha ajabu, kupingwa kwa maandamano hayo sio kitu cha ajabu, matokeo ya maandamano hayo sio kitu cha ajabu.

Hivi mwanakijiji unaweza ku-imagine miaka kadhaa ijayo CDM wakiwa wanatawala Tz (naamini hiyo siku ipo), watakuwa wanatumia jeshi la polisi kuwapiga mabomu waandamanaji wa vyama vya upinzani watakaokuwa wanatutetea wananchi? Unaweza ku-imagine CDM watakuwa wanawatumia wakuu wa wilaya, na wasimamizi wa uchaguzi kuchakachua matokeo? Kama hau-imagine hayo, then better you quit politics very now...
Nakubaliana na mengi uloandika isipokuwa sehemu moja tu...ile niloiweka bold..

Mkuu wangu watu huandamana sii kwa sababu ya kuonyesha chuki bali kuufikisha ujumbe wao iwe kwa wananchi au vyombo husika..Hivyo hata maandamano ya wanawake kuadhimisha siku ya wanawake duniani ni ujumbe unaohamasisha sawa kabisa na ule unaopinga serikali kwa sababu lengo lao wote ni kuufikisha ujumbe kwa wananchi...hakuna chuki na ndio maana siku zote maandamano yoyote hupewa kibali cha kulindwa dhidi ya wale wanaoweka chuki. Kwa bahati mbaya siku hizi muandamanaji ndiye kawa mkosa kama vile Mwanamapinduzi anavyoitwa Gaidi, depends on who is in power.
 
M. M. Mwanakijiji

Wakati wa ukoloni wanaharakati za kisiasa nchini wakiongozwa na TANU walijenga hoja mbalimbali za kutaka dhulma mbalimbali ziondolewe na utawala wa kikoloni. Siyo kupitia vyama vya kisiasa tu bali pia vyama vya wafanyakazi. Katika historia yetu kuna matukio kama mgomo wa wafanyakazi wa bandarini (ambao kina Sykes wanakumbwa kwao sana) umeacha historia ya nguvu ya wafanyakazi nchini. Mgomo wa kugomea bia nao ulikuwa ni wa harakati za shinikizo la kisiasa. Mgomo wa bandarini ndio ulimvuvia sana Mzee Shafi Adam Shafi kuandika lile simulizi la KULI (natumaini bado vijana wetu wanakisoma kitabu hiki).
Shafi Adam Shafi katika simulizi ya KULI hichi kitabu Mzee MM, siku hizi hakisomwi mashuleni.
 
Maandamano ni njia ya kisataarabu kabisa ya kueleza hisia ziwe nzuri au mbaya, lengo likiwa kufikisha ujumbe kwa wanaohusika na kushuhudiwa na umma. Maandamano si lazima yawe ya kupinga, tumeona ya kupongeza pia, kwahiyo ni 'two way traffic'.

Si lengo la maandamano kujenga chuki kati ya wananchi na serikali yao kwasababu yanaweza kuwa dhidi ya mtu au taasisi. Tunakumbuka yale ya LONRHO au kupinga IMF. Tunakumbuka yale Azimio la Arusha n.k. Kwa mantiki hiyo, dhana kuwa maandamano ni kujenga chuki kati ya serikali na wananchi si ya kweli.

Lakini pia tujiulize yanajengaje chuki kama kinachosemwa ni kweli? Kwa mfano Chadema walipokuwa na maandamano ya suala la Arusha wananchi 'wakateka nyara' na kueleza hisia zao kuhusu bei ya sukari. Serikai ikakiri upungufu na ongezeko la bei linalomuumiza mwananchi, sasa hapa maandamano yalilengaje chuki. Nadhani hii dhana ya kujenga chuki inatumika kisiasa kwasababu kimantiki haiingii akilini mtu kuandamana akidai hajapata mshahara miezi miwili halafu tuseme anajenga chuki na serikali au waandaji wanajenga chuki na serikali yao!! Kwamba kudai haki yako ni kujenga chuki!

Nini kifanyike ili kusiwe na umwagaji wa damu, ni kufumua mfumo wetu tuliokubaliana wa kujitawala. Kwamba waajri (wananchi) wapewe nguvu ya kusikika, na waajiriwa (viongozi) wajue kuwa hawana hati miliki ya kazi au ofisi wanazokalia na kwamba hata kama mkataba haujamalizika basi mwajiri ana haki ya kumwadhibu mwajiriwa.

Tanzania leo rais amejihakikishia kuwa akichaguliwa lazima amalize miaka 5, hilo halipo Japan.
Wabunge ni lazima wamalize miaka 5 na wanawajibika kwa mawakala wao(vyama) na si waajiri. Haya yote ndiyo yanajenga kiburi cha hawa viongozi kutumia madaraka yao vibaya hata kuvuruga maandamano halali kama alivyofanya mwingereza.

Tuandike mkataba (Katiba) itakayomfanya kila mmoja wetu kuanzia rais hadi mwanafunzi kuelewa kuwa haki inakwenda sambasamba na wajibu na kwamba kila mtu amekalia kuti kavu na kwamba waajiri ndio wenye nchi na wasikilizwe hata kama ni 50.

Tuandike mkataba utakaomweka kila mmoja roho juu katika kuwajibika, mkuu wa polisi awajibike kwa waajiri wake ambao ni wananchi, mkuu wa mkoa awajibike kwa waajiri vivyohivyo hadi kumfikia mkuu wa nchi na kwamba lilitokea lislo tarajiwa kila mtu ataubeba msalaba kwa uzito wake na si kama ilivyo sasa.
 
Tuko, nimependa take yako. Katika mazingira ambayo yote mawili yanawezekana ni kwa namna gani basi tunaweza kufanya mambo yote mawili bila kumwaga damu au kuleta madhara kwa watu na vitu?

Maandamano ya kuishinikiza serikali hayawezi kuwa na amani, siku zote watawala watatumia nguvu za dola kwa kisingizio cha kulinda amani wapo tayari kuua kutetea maslahi yao.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Tuko, nimependa take yako. Katika mazingira ambayo yote mawili yanawezekana ni kwa namna gani basi tunaweza kufanya mambo yote mawili bila kumwaga damu au kuleta madhara kwa watu na vitu?

MMKJJ kuna principle inasema 'every action has equal and opposite reaction (mimi sikusoma physics, so sijui kama naipatia). As long as kuna kupingana, lazima kuwe na matokeo ya kupingana huko. Kupigwa virungu, kupuliziwa hewa ya machozi, kupigwa risasi, ndiyo namna 'sahihi' ya serikali kupinga. Nasema sahihi sio kwa sababu naiunga mkono, bali najua no effective alternative, it just depend on the projected and persieved impact ya maandamano, kama inavyokuwa determined na serikali inayokuwapo madarani.

I afraid that if we want to have demonstartions with impact, no way to avoid killings
 
Back
Top Bottom