Kwanini Lunyamila ni maarufu sana jijini Kampala, Uganda?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,702
45,021
Winga wa zamani wa kimataifa wa Yanga na Tanzania, Edibily Jonas Lunyamila ana umaarufu mkubwa sana jijini Kampala, katika mashabiki watano wakongwe wa mpira basi watatu lazima wamuulizie Lunyamila hasa wakijua kama wewe ni Mtanzania.

Huku kwetu wabongo tushamsahau, je ndio kusema nabii hakubaliki kwao? Je ni kitu gani Lunyamila aliwafanya Waganda mpaka leo wanamkumbuka? karibuni.
 
Kama kumbukumbu ziko vizuri kizota na lunyamila wakiwa yanga miaka ile ya 90 waliuzimisha kabisa mji wa kampala kwa kuzisambaratisha club za vila na express na hatimaye kuwanyang’anya ‘ waganda ndoo ya cecaf, miaka kama 4 tena baadaye lunyamila akishirikiana na kalimangonga waliweza kuisaidia yanga kuisambaratisha sports club villa mjini kampala na hatimaye kuwanyang’anya tonge mdomoni tena waganda na kufanikiwa kubeba tena ndoo ya cecafa
 
Licha ya umahiri wa Lunyamila, pia Waganda walikoshwa na uhodari wa Said Mwamba Kizota alipomdhibiti straika hatari wa Kiganda, Majid Musisi.

Baadhi ya wachezaji wa Yanga ni pamoja na Salum Kabunda Ninja, Kenneth Mkapa, Bakari Malima,
 
Kama kumbukumbu ziko vizuri kizota na lunyamila wakiwa yanga miaka ile ya 90 waliuzimisha kabisa mji wa kampala kwa kuzisambaratisha club za vila na express na hatimaye kuwanyang’anya ‘ waganda ndoo ya cecaf, miaka kama 4 tena baadaye lunyamila akishirikiana na kalimangonga waliweza kuisaidia yanga kuisambaratisha sports club villa mjini kampala na hatimaye kuwanyang’anya tonge mdomoni tena waganda na kufanikiwa kubeba tena ndoo ya cecafa
Ni kombe sio ndoo
 
Back
Top Bottom