Kwanini Lowassa havai vazi rasmi la CHADEMA maarufu kama gwanda?

senzighe

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,745
2,000
Nawauliza hasa wanachama wa CHADEMA. Tangu kuhamia kwake katika chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa amekuwa havai mavazi wala nembo za CHADEMA.

Kwanini? Lowassa haonekani kuvaa magwanda wala fulana za CHADEMA mahali popote. Fulana hubeba nembo za chama chake. Nembo za CHADEMA hubeba itikadi na msimamo wa chama. Kwanini yeye havai?

Is he a temporary member of CHADEMA? Hapendi au kukubaliana na mavazi na nembo rasmi za CHADEMA? Katika mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA huko Dodoma leo,ni Lowassa tu ambaye hakuvaa fulana wala gwanda rasmi la CHADEMA. WHY?

Kwani hujui ? Mmoja nje Mmoja ndani
 
cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,137
2,000
Roho yake bado ipo CCM, huko ni mwili wake tu upo kuwa na cheo tu na kuwaburuza wasiojielewa.
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
9,853
2,000
One thing;
Lowassa ni mwanasiasa ambaye ana wapenzi kutoka vyama vyote vya siasa. Na ndivyo alivyouza brand yake .

Angalia kampeni kama ulipo tupo utagundua ana haki ya kuwa alivyo.
Actually ina faida pia.
Unaona Magufuli ameshindwa kuiunganisha nchi kwaajili ya kuwa too partisan. Actually ana ride on luck . Likitokea janga kubwa la kitaifa kama vita utanielewa zaidi .

So, Lowassa yuko poa.
Halafu kama unafuatilia kinachoendelea katika siasa duniani kote, watu wamekuwa na tendency ya kuachana na vyama na kutafuta mtu Neutral anayeweza kubeba hoja zao na kuunganisha taifa.
Umekuwa kama Mkikuyu ambao hata mlevi akionekana kalewa busaa humlaumu Odinga,wewe kila siku ukitokea ujinga wenu humlaumu raisi Magufuli.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
8,798
2,000
Tupia hata picha moja ambapo Nyerere amevaa shati la kijani na kofia ya njano. Je, Nyerere was a temporary member ? Au alikuwa hakubaliani na vazi la ccm ?
 
na unimanye

Member
Apr 20, 2014
84
125
Chadema imeingia choo cha kike.... Na siku Dr. Slaa akiamua atoe ya moyoni lazima Chadema ipasuke vipande vipande tu
 
sebastian longfellow

Senior Member
Feb 13, 2014
173
250
Mkuu ,swali lako sio baya ila majibu yake sasa ndio mabaya.

mavazi ya cdm si mabaya ila rangi zake na nembo yao ndio tatizo.

kwanini havai? havai kwasababu moja rangi za chama-Blue ina maana ya Freedom from Harm .

sare za Chama-Magwanda.Husimama kama mbadala wa mavazi ya kijeshi hivi .(harufu ya Vita)

Mkuu ,Nimekuraisishia tu we Fanya kama unaunga dot na mauaji ya mwangosi .utapata majibu ya kwanini havai.
 
jiwe la majiwe

JF-Expert Member
Sep 18, 2016
2,539
2,000
Nawauliza hasa wanachama wa CHADEMA. Tangu kuhamia kwake katika chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa amekuwa havai mavazi wala nembo za CHADEMA.

Kwanini? Lowassa haonekani kuvaa magwanda wala fulana za CHADEMA mahali popote. Fulana hubeba nembo za chama chake. Nembo za CHADEMA hubeba itikadi na msimamo wa chama. Kwanini yeye havai?

Is he a temporary member of CHADEMA? Hapendi au kukubaliana na mavazi na nembo rasmi za CHADEMA? Katika mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA huko Dodoma leo,ni Lowassa tu ambaye hakuvaa fulana wala gwanda rasmi la CHADEMA. WHY?
Ebu naomba onesha mahali Nyerere alivaa mavazi ya CCM.
 
Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,344
2,000
Yanayohusu nini? Andaeni wanashida wa kwenda londoni kujibu madai ya macontainer
 
kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,063
2,000
hhahaha kwa wingi huo nna uhakika zinachemsha makande mpk yanaiva:D:D
 
Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,771
2,000
Lowassa ana mashabiki vyama vyotee vya siasa hapa tz so Hana haja ya kuvaa sare ya chama

Napia chadema hatuangalii kuvaa magwanda bali matendo

Waweza vaa suti na kubeba bibilia kumbe ni muasherati au jambazi no 1
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom