Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Naomba mnisaidie hapa, kwenye uchaguzi uliopita ukawa au Muungano wa baadhi ya vyama vya Upinzani vilipata kura milioni 6 kati ya kura zote zilizopigwa, mpaka hapo sina tatizo, ila nisichoelewa ni kwa nini Lowasa husema kwamba hizo kura milioni 6 ni zake?, yaani ina maana yeye ndiye aliyeleta kura milioni 6 ukawa, hivi hili ni kweli au upotoshaji?
Tuangalie trend ya upingaji kura TZ!
Uchaguzi wa mwaka 2005,
CUF chini ya Lipumba ilipata 11.6% ya kura zilizopigwa
CHADEMA chini ya Mbowe ilipata 5.9% ya kura zote zilizopigwa na wengine ukiondoa CCM ambaye ndiyo mshindi walipata kura chache zaidi!
Uchaguzi wa Mwaka 2010
CHADEMA chini ya Slaa ilipata kura 2 271 841 ambazo ni sawa na 26.34% ambalo ni ongezeko za mara 4 ya kura za mwaka 2005 yaani ktk 5.6-26.34%
CUF chini ya Lipumba ilipata kura 695 667 ambazo ni sawa na 8.06% ya kura zote zilizopigwa na wengineo walipata chini ya 1.5%
CCM chini ya Kikwete walipata kura 5 276 827 sawa na 61.17% ya kura zote zilizopigwa!
Mwaka 2015
CHADEMA walipata kura 4 627 923 sawa na asilimia 31.75%
CUF walipata kura 1,257 765 sawa na 8.63%
CCM 55.04%
Sasa swali langu ni Je, ina maana kama Lowasa asingegombea upande ukawa, wangeshindwa kweli kufikisha hizo kura, kwa maana ukiangalia trend Slaa na CHADEMA waliongeza ndani ya miaka 5 ktk 5.6% za Mbowe mpaka 26.34% ambayo ni zaidi ya mara 4 ndani ya miaka 5 tu, sasa kwanini angeshindwa au niseme CHADEMA na CUF chini ya Lipumba wangeshindwa bila ya Lowasa kuongeza 5% tu zaidi ndani ya miaka 5 mingine? Au kura nyingi zaidi?
Lengo langu hapa na kuondoa tafsiri na uongo tunaolishwa kila siku kwamba Lowasa ameleta kura milioni 6 ukawa hali inayopelekea baadhi ya watu kuamini na kukubali upotoshaji huu kwani hata kama Lowasa asingegombea ukweli kwa kutumia kielelezo cha chaguzi za nyuma bado ukawa wangeweza kufikisha hizo kura kama siyo zaidi ya hapo, kwa maana ukawa wameongeza 5% tu ktk 26% walizopata CHADEMA 2010, hesabu hazidanganyi!
Hivyo acheni kuabudu watu, Lowasa hana kura milioni 6, bali kilichompa kura milioni 6 ni ukawa, hivyo ukawa yaani vyama ndivyo vilivyompa kura na siyo yeye ndiyo aliyevipa vyama kura kuweni makini sana kwenye hili, msipotoshwe kila kitu kipo wazi fanyeni hesabu tu, hivyo acheni kuabudu watu na fwateni sera za vyama hii itasaidia kujenga taasisi kwenye vyama na siyo kuabudu mtu!