Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015

Katika hali niliyoitafusiri kama kuchanganyikiwa leo magufuli katoa tena mpya jangwani baada ya kumwambia Rais Kikwete.Nasema wazi, Mheshimiwa Rais Kikwete unisamehe. Uliweka baadhi ya watu madarakani ambao walituchelewesha kwenda mbele
Nimejiuliza huyu mtu naweza kuwa Rais kweli.Huku akijisibu serekali ya JK imefanya makubwa,Huku anakiri maendeleo yamecheleweshwa kwa uteuzi mbovu wa JK
Huyu mtu ni wa kuangalia mara mbili mbili,La sivyo tutazamisha taifa
 
EDWARD LOWASSA TUMEKUCHOKA KUKUSUBIRI, TUMECHOKA KUISUBIRI NURU YA MATUMAINI ULIYO NAYO.

Kila kona ya nchi wanyonge wamekata Tamaa kwa kukusubiri Erdward Lowassa , kila uwaanda uwe wa juu ama wa chini bado 'twasaka matumaini. Tumekuwa wakiwa kwa miaka hamsini, Baba wa wanyonge alie jaribu kila njia kuitafuta nuru, nuru ambayo ilikuwa Nyuma ya Giza la Umasikini, Maradhi na Ujinga.

Tumechoka kila siku ahadi zako Edward Lowassa, ukituahidi kuungana nasi kuundoa huu ukungu, Ukungu ulio wasumbua Alhaji, Benjamin na sasa Shahiba wako Jk bado anatafuta nuru. Tumesha hesabu miongo ya kutosha kuutaka mwanga wa Uwanda wa Monduli, ambao tuliamini tutaupata kwa kaka yako kipenzi Sokoine ambaye ni Mshumaaa ulio zima. Sokoine alijaribu na kuthubutu kama ilivyo nia na dhamira yako.

Edward Lowassa tusaidie haya, Kwetu nanjilinji hakuna madawa hospitali, wakwere na wazaramo bado wanachezwa ngoma kipindi cha kwenda Darasani , Usukumani bado kwetu tulipata Maji tukaonja nuru lakini sasa bado kilimo cha pamba kinakosa masoko.

Edward Lowassa sisi Boda Boda tuliiona Nuru kwa ajira ulizo zalisha nchi nzima , ona sasa twataabika kuisaka nuru ya bima ya maisha, ona Muhimbili Mwaisela mahafidhina wametuacha twalazwa chini kwa maumivu yalio kithiri kwa ajali za uzembe wa Kitengo cha usalama barabarani na lawama za umbumbu Wangu wa ufinyu wa sharia za barabarani.

Edward Lowassa tumechoka kusubiri ujio wako sisi Mama ntilie , Kwetu mikopo midogo midogo imekuwa wimbo kutufikia kwani mabilioni ya swahiba wako Dk Jakaya wahafidhina wamekula. Tunahitaji nuru kuliko ile ya Machinga complex inayo liwa na wajanja huku wakitulazimishe tuamie kwao kutunisha mifuko yao ya familia zao walio peana.

Edward Lowassa tumechoka kuuana wenyewe kwa wenye huku kiteto na Kule morogoro , hebu njoo utuunganishe kama enzi zile ukiwa Waziri wa ardhi miaka ya tisini, Tumekuwa wanyonge hakuna wakumkimbilia. Hebu njoo ulipo utoe sauti ya Matumaini, tuione nuru.

Erdward Lowassa Tumechoka kukusubiri ujitokeze kwa kutangaza nia ya kuwa Rais wa Tanzania, Edward Lowassa makundi kwa makundi tumejitokeza kukuomba, Toka ulipo una nuru ya kulivusha hili Taifa maana mashekh na Wachungaji wameitoa sauti ya kiroho iliyo ndani yako, Edward Lowassa usihofu kwa kejeli na za wachache wenye kuziba Mwanga wanuru yako maana ya Ng'ara hata mchana wa jua kali. Baba ulie thubutu kuwalinda na kuwaonyesha njia Watanzania wapi pa kupita ,sasa twakuhitaji ulipo jificha kwa miaka Saba . Edward Lowassa hakika wewe ni Nuru ya Kweli tunayoihitaji kwa maendeleo ya Taifa jipya , tuka na wewe , tunaenda na wewe ikulu 2015.

MAAMUZI NA MATUMAINI MAPYA 2015 NA EDWARD LOWASSA, NURU TULIOCHA KUISUBIRI.

Na John Okello.

Ddddddd
 
Watanzania tufike mahali tuwe na weledi.Siasa majitaka zimetufikisha hapa tulipo. Miaka 10 iliyopita tuliaminishwa ujiowa masiah Leo tukiangalia nyuma tunajuta

Ni vema tukawa na njia mbadala za kunadi wagombea kwa sifa, historia, uadilifu, uaminifu na uwajibikajina wala si dhana ya mawazo ya mtu

Nchi inaongozwa na sera na si mawazo binafasi. CCM ndio kabisa maana unapotofautiana nao wanakuchinjilia mbali kama walivyomtosa Mansour Himid kwa mtazamo tofauti.


Haiwezekani EL akaenda kinyume naestablishment aliyoikuta na iliyomlea.

Baada ya hayo napenda nionyeshe siasamajitaka.
Siasa safi zinaambatana na ukweli, huu uzi ni la utamaduni wa kutakakuuzia watu mbuzi ndani ya gunia.

Tunafanya hivi si kuzuia au kumharibia EL,bali kuwaonyesha Watanzania jinsi wapambe wake wanavyoziba mashimo kwa hoja muflisi.


Mleta mada: Lindiwe Sisulu(Rangi yabluu)
Watanzania ..wakinung'unika na kukata tamaa ndani bila kupatamajawabu...majawabu yao ni kwa Edward Lowassa kuwa Rais.

Jbu la hoja:EL ni sehemu yauongozi wa nchi kwa muda mrefu. EL haja tofautiana na sera za CCMzilizotufikisha hapa. Alimtengenezea njia JK,mpango wao ni mmoja chini ya CCM.


Ukuaji wa uchumiuna muhitaji Lowass. Akiwa waziri waMazingira na Umaskini aliweza umudu na kusaidia Tanzania kukabiliana naumaskini na ukuaji wa Uchumi na Taifa liliondolewa misamaha ya madeni.
Tuonyeshweuchumi ulikua kwa kiasi gani tofauti na umasikini uliopo sasa.
Pili, CD Msuya alikuwa waziriwa fedha na chini ya Paris club tulifutiwa madeni.
Wakati yakitokea EL alikuwa hanajina nchini. Nawala CD hakuwahi kuwa Rais kwa kigezo cha kufutiwa madeni na Paris club. ELhakwenda Paris kama mtu binafasi, alipewa instruments kama waziri na si mtu binafsi.


Lowassa alianzishamamlaka ya Maji, kuondoa uhuni wa NUWA na kuanzishwa kwa Dawasco baada ya CityWater kuzingua.Leo Sera ya Maji aliyoisimamia Lowassa inafanya kazi
Shirika la DSSD lilikuwepo kabla yaEL. DSSD ilipovunjwa si kazi ya EL.
Alichokikuta ni city water. Kama sera zake ndizo zinafany kazi, wakazi wa Dar es salaam wanaoishi kwa maji ya madumu hawapaswi hata kumsikia akitajwa. Credit anazopewa ni ndogo kuliko failure


Lowassa aliletamapinduzi ya soko la Mifugo na kuanzishwa viwanda vya usindikwaji wa maziwakama Tanga Fresh na ASAS.

Musoma kulikuwa na kiwanda cha maziwa mwaka 1973 EL akiwa shuleni.
Viwanda kule Arusha na Moshi vilikuwepo EL hajawa mbunge. Tanga fresh kilikuwepo kabla hajawaPM.

Labdakama kujiuzia ranchi ya Handeni yeye na shemeji zake ni sera nzuri, vinginevyo uhuni huo ndio uliomlea na kulitia taifa katika hasara na aibu.
EL alikwapua ranchi ya taifaikiwa ni precursor iliyompa uzoefu katika mambo mengine


Sekta ya Elimu nani Kama Lowassa??Kusimamia kujengwa kwaUDOM. Shuleza Kata ni msukumo wa Lowassa na aliwasimamia.Leo tunajivunia hizi shule.
UDOM unapoitaja wapo wanaogeuka hukokaburini. Shule za kata ni felia nyingine ya EL.

Alipita akichangisha watu pesahuku akihujumu taifa kwa kulinda wezi marafiki zake.
EL alikurupuka kujenga shule bila kujua walimu wanatoka wapi, na walimu hao wanamaeneo ya kuishi. Kukurupuka kwake ndiko kumezaa tatizo la shule kutokuwa na maktaba au maabara.

Leo back to square one, watu wanachangishwa kujenga maabara licha ya upotevu wa mamilioni unaondelea ulisosimamiwa na EL. Ni kutokanana upofu wake na kukosa uaminifu, mipango ilifanywa kwa jazba.
Tunazalisha devision 5unatuambia ni mafanikio ya EL.


Huyu mtu nimakini sana na kamati yake yote.
Hakuna anayejua kamati ya EL isipokuwa wewe, ni makosa kuaminisha umma kamati za chumbani na umakini wake


Lowassaanateswa sana na kuwasaidia vijana kwenye suala la Ajira maana kwake analiitabomu.
Alipoku wawaziri katika nafasi mbali mbali na hata PM hajawahi kuja na solution zaidi yamalalamiko.
Hajatuambia anategua bomu hilo kwa namna gani.
Kama ununuzi wa boda boda ndiyo sera yake,taifa hili litakuwa la wendawazimukuifikiria hiyo sera


Lowassa ana kiu ya kuona sekta ya elimu inakuwa kwa kasi na kutatua matatizo yawasomi.
Hiyo kiuunaijua wewe. EL hawezi kuja na sera tofauti na aliyotangaza JK juzi.

Ni sera za CCM na si mtu binafasi. Hana sifa za kuongelea matatizo ya wasomi si nje au ndani ya bunge.Baada ya kufukuzwa uwaziri mkuu hatujamsikia akizungumzia lolote kwa wananchizaidi ya kujikita makanisani akishawishi waumini kwa kutumia dini.

Hana sera usitueleze ana solution. Kama anayo basi anaijua yeye na mkewe pengine na wewe.
Iliyopo ni ya CCM aliyotangaza JK


Lowasaa anaonakuwa bado sekta ya Afya haijawa sawa hasa kwa wakina Mama, Watoto na Wazeekatika kupata matibabu.
Anaweza kuona kama mtu mwingine. HanaHistioria yoyote ya maana au mbovu kama ya shule za kata kuhusu afya.


Lowassa anatakakuona mabadiliko hasa ya sekta ya Kilimo chenye tija kwa mkulima na pembejeozake.
Hizo nazo ni hadithi unazozijua wewekama mpambe.
Hana historia ya kushughulikia kilimo. Kinyumechake alimponda Pinda kwa kilimo kwanza.


Lowassa anatakakuona Taifa hili linakuwa sawa kwenye masuala ya Miundombinu na Sekta yaUchukuzi.
Hana lolote la kuonyesha, ni ndoto tu alizowasilimulia.Hajawahi kueleza anafikiria nini kuhusu miundo mbinu.

Bngeni amekuwa kimya miundo mbinu ijkijadiliwa. Leo anatoa wapi akili ya miundo mbinu aliyoshindwa akiwa PM na hata kumshauriswahiba yake

Lowassa anatakakuona Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wakiendelea kudhibiti uingizwahi na utokajiwa madawa ya kulevya pamoja na rasilimari za taifa hili.
Hakuweza kudibiti Richmond hanauiwezo wa kupambana na 'drug barons'. Ni hadithi tu za kusaidikika

Lowassa anatakakuona Tanzania yenye Ndege zake binafsi kwa Kenye Airways na Ethiopia Airlinesna kwa nini enzi za Nyerere mpaka Mkapa tulikuwa na ndege zetu.
Alipokuwa PM na Mustafa Nyanganyi mwenyekiti wa bodi ATC ikifikia kifo chake.
Leo ana akili gani mpya aliyopata zaidi ya ile aliyoitumia kuua ATC


Lowassa anatakakuona Taifa hili linakuwa na Haki na Usawa kwa kila Mwananchi.
Haki gani anayotaka ikiwa wapo wanaochangishwa ada zakujenga shule, na kodi zao zikienda mifukoni mwa rafiki zake wa Richmond.

Tanzania yenyviongozi makini ambao ni Wazalendo, Wachapakazi, Wawajibikaji, Waadilifu nawenye kusimamia maamuzi yao na kuyatekeleza.Viongozi watakao pambana na Rushwana Ufisadi.
EL hapaswi kuzungumzia rushwa. Kitendo cha kusema neno rushwa tu, rushwa yenyewe inashangilia.

Akiwa PM alishindwa kusimamia kwa uadilifu mali za Watanzania. Akaamua U-PM wake nibora kuliko taifa.
Akakaa kimya wezi wakikwapua mali za taifa hili. Uzalendo ukamshinda hata kukemea.
Hana sifa ya kupambana na rushwa, uaminifu au uadilifu.


Hakika nduguwana jamvi naomba niwaambie kama ulipata nafasi ya kujua vipaumbele vya Lowassabasi TANZANIA TUITAKAYO inawezekana kwake Kipaumbele cha EL ni kuwa Rais, hanajingine.
Uzalendo hanana Richmond ni shahidi, hana maono shule za kata zinamhukumu, na hana uaminifu alipoachiawezi wakwapue mali za taifa, hana uadilifu kwasababu tumbo lake ni muhimu kuliko taifa

EL ni kiongozi pekee aliyesimama kimya wezi wakiiba. Alisimama ndani ya bunge na kusema hakukuwa na uhalifu ili hali alijua ulukuwepo.

Alitumia taarifa ya PCCB kwa kuifinyanga ili kulinda wezi marafiki zake.

Akalitia taifa hasara naleo anasema hakuwa yeye. Kama si yeye kwanini alisimama bungeni na kusemahakukuwa na uhalaifu?

Alikuwa na uwezo wa kukemea, hakufanya hivyo. Alikuwa nauwezo wa kuzuia hakutenda, alikuwa na uwezo wa kukataa kwa kujiuzulu hakufanyahilo, alichokifanya ni kufukuzwa kazi.

Msidanganye umma, huyu kimaadili hafai kabisa. Kama hakuweza kuzuia uhalifu hana sifa za kupambana na wahalifu. Hajajibu tuhumanzito zinazomkabili.

Tumechoka na upambe sasa tupo hapa kuwaeleza Watanzania EL ni nani ili wawe na hiari kama waliyokuwa nayo miaka 10 iliyopita. Ni haki yao kuelezwa na ni haki yao kuamua.
Ulichambua vizuri sana ila tatizo mkamchukua huyo Mamvi
 
Back
Top Bottom