Kwanini Lowassa amepotea baada ya kipigo uchaguzi mdogo? Ni aibu au amekata tamaa?

naona nyie lumumba bila kumwongelea Mheshimiwa Lowassa cku haitaenda hata kidogo maana ndio sera ya chama chenu cha majambazi
 
W
Wadau, amani iwe kwenu.

Mlengwa hapo juu katika kipindi cha kuelekea uchaguzi Mdogo na wakati wa kampeni, alipita mikoa kadhaa kwa lengo la kujenga chama chake, CHADEMA kwa madai kuwa hakina mizizi kwa wananchi. Nakumbuka alivyoweka kambi kanda ya Ziwa huku akitoa ahadi hewa mithili ya zile ahadi za mvua ya Thailand. Kwamba, ataongea na wafadhili ili washushe chakula kuwasaidia wananchi wenye njaa. Hadi sasa, mzee Lowasa hajaleta chakula cha msaada alichoahidi.

Baada ya kipigo kitakatifu ambapo CHADEMA waliambulia Kata moja tu huku wakipokonywa nyingine na CCM kati ya kata 20 zilizogombaniwa, hakika mzee sijui kajificha wapi. Haonekani kwenye media wala social media. Yaani kwa ujumla kapotea mithili ya kakakuona.

Najiuliza maswali kibao na sipati jibu. Je kupotea huku ni aibu ya kipigo hicho? Au amekata tamaa na vyama vya upinzani kwa vile anaonekana kutwanga maji kwenye kinu? Au kawasusia CHADEMA? Au kakasirika? Au kaishiwa pumzi? Au? Au? Au? Mliopo jirani na huyo mzee naomba mjitokeze na kutueleza nini kinaendelea.
waeza ona hivyo uonavyo, siasa si vivyo uidhaniavyo kwamba mtu aibuke kwa utashi wa watu furani. Iwapo hivyo, hatima yake fupi tu. Lowssa ni mwanasiasa aliyekomaa kuliko kisigino cha babu yako kilichotembea peku miaka yote kikiijenga "ninyiem" wakti yeye akibaki kapi. Anajua afanye nini wakti gani na wapi na si kinyume chake kama utamnukuu Zitto kuhusu mwalimu wa zamu wiki hii. Anajielewa na yuko pahala sahihi sana. Unakaribishwa sana
 
Back
Top Bottom