Rais wa JMT ni Magufuli kwa sasa. Najiuliza maswali mengi kwanini sio Lowasa? Najiuliza kwa sababu tangu uchaguzi upite hadi sasa Lowasa amepita sehemu nyingi au hata baadhi ya wana CHADEMA wamesema kuwa uchaguzi uliopita tulishinda. Swali ni kwanini hawako madarakani? Labda jibu rahisi ni kusema WALIPOKONYWA ushindi. Sawa ikiwa hili ni jibu, je hao wapokonyaji 2020 hawatakuwepo? Au watakuwa wameacha hiyo tabia? Binafsi naona kama ni kutuhadaa kuambiwa 2020 tupige kura kwa wingi. Oh tutashinda. Wakati huo huo tunaambiwa 2015 tulishinda. Ombi kwa CHADEMA na ukawa kwa ujumla. Kutafuta namna ya kumdhibiti huyo mpokonyaji kwanza, ni kazi bure kuhamasisha oh tupige kura kwa wingi. Au ni kazi bure kuendelea na nyimbo za oh tutalinda kura, oh hakuna kura itakayoibiwa. Hayo yakishafanyiwa utatuzi wa uhakika ndipo mlete nyimbo zingine za kupiga kura kwa wingi. Kinyume na hilo kilichomfanya leo Lowasa asiwe rais wa JMT hakitashindwa asiwe hata 2020 au 2025 au hata wakati mwingine wowote. Si Lowasa tu hata mgombea yeyote wa upinzani. Maoni yangu tu