Kwanini LOWASA ANAKUBALIKA? Monduli wapo naye pamoja damu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini LOWASA ANAKUBALIKA? Monduli wapo naye pamoja damu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Msanii, Sep 18, 2010.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kuna ule ukweli kwamba DAMU nzito kuliko maji ambao ndio hasa unambeba mtanzania hyyu ambaye ameandamwa na kila aina ya harufu ya ufisadi na ujambazi wa mali za umma.

  Kwanza kwa kulazimika kujiuzulu kwa aibu baada ya deal ya RICHMONDULI kuingia mchanga kulimfanya aonekane hafai ktk jamii na ni mtu dhalili, Ila kutokana na hulka yake na UTHUBUTU wa kifisadi alio nao ameamua kujijenga upya kutamalaki himaya mwaka 2015. Amepandikiza vicheche(vibaraka) wake kuanzia ngazi za chini za uongozi ndani ya CCM, pia ndiye ambaye alipendekeza kwa JK majina mengi ya DCs na RCs ambao wanaushwishi ktk kamati za maamuzi za ccm ktk level zao. Amemijengea jina kwa style yake ya majibu na wajibu wa papo kwa hapo ambapo alishaleta madhara ktk ajira za watu hasa hulka yake ya kuwavua madaraka watendaji was erikali hadharani pasipo kutimiza ile kanuni ya NATURAL JUSTICE.

  Ujambazi wake wa mali za umma ulianzia akiwa angali mdogo au kinda serikalini ambapo kila mahala alipopita aliacha makapi, na sana sana nyingi ya wizara ama ofisi alizopita ziliishia kuungua kwa moto (kupoteza ushahidi). Hatukatai kwamba anawekeza ila shida inakuja pale ambapo yeye ni mtumishi wa UMMA inazua maswali anapata wapi muda wa kutafakari na kufanya uwekezaji mkubwa alio nao ndani na nje ya nchi. Mtaji alipata wapi? maana wazazi wake hawana historia ya ubepari ambao labda alirithi kutoka kwao.

  Kuna baadhi ya sababu ambazo zinamfanya aonekane shujaa nazo ni:-

  1. fabrications za habari zinazochechemizwa na magazeti yaliyo kwenye payroll yake na kutoka kwa waandishi makini waliopigwa upofu kwa fedha anazowalipa.
  2. Maswahiba zake ambao amewaweka ktk posts mbalimbali kwa manufaa yake ya kisiasa hasa pale wanapotumia gharama yoyote kumfuta matope aliyojitumbukiza kwayo ionekane kwamba alionewa.
  3. ukaribu wake na rais ambapo kama asemavyo hawakukutana njiani. IKUMBUKWE pia kwamba hawa waheshimiwa wana ubia wa kufa na kuzikana hivyo mkuu wa kaya hawezi kumwacha aanguke kibudu.
  4. Kukubalika umasaini hasa MBULU ambapo wapo naye pamoja kwa kila hali (hapa ndipo kwenye hoja mbadala sasa)
  Wanamonduli ambao wameapa kufa naye ni aina nyingine ya matokeo ya ufisadi ambayo madhara yake ni makubwa zaidi ya bomu la atomik. Ule usemi wangu pale juu kwamba DAMU NZITO i meant kuwa baada ya wizi wa kutisha alihakikisha anakula na nduguze ili wasimtose. Ni sawa na kusema kwamba Mke au ndugu hawezi kumtosa nduguye kwa kumpigia kura ya ujambazi akamatwe vivyo hivyo wanamonduli hawawezi kuwa miongoni mwa WATANZANIA wanaolalamika kukosa huduma za afya, maji safi, elimu na shule bora. Ni sawa na kusema kwamba Wanamonduli hawaoni kosa lolote kwa ndugu yao LOWASA na sanasana wanamwona shujaa ambaye amewafanikisha mambo mengi. Je tuamini kwamba ufusadi unaweza kuathiri sehemu ya jamii na kuamini kwamba the theme is lunatic? Je Tuamini kwamba WANAMONDULI ni sehemu ya jamii ambayo imewasaliti WATANZANIA kwa kumkumbatia na kumficha JAMBAZI wa mali ya umma kwa kumpa ulinzi na fursa ya kuendelea kuwanufaisha kwa ufisadi mpya atakaoufanya?

  Sitaki kushindwa kufikiria kwamba LOWASA amewasumisha wanamonduli kiwango hiki.
  Kuhusu maswahiba zake tunafahamu kwamba wanatumikia kafiri wapate mradi wao.

  Ikumbukwe LOWASA aliwahi kuwa waziri mkuu na mawaziri wakuu wengi nchini walijiingiza hata ndani ya mfumo (UwT) kwa manufaa yao ya mbeleni, sishindwi kuamini kwamba inawezekana walishawahi kuwachomeka baadhi ya watu wao humo ndani ya hilo dubwasha kwa minajili ya kujihalalishia mawasiliano ya core. Je kwa hulka ya UTAWALA aliyonayo LOWASA haiyumkiniki kwamba anao vijana wake ndani ya UwT ambao wanafuata maelekezo yake?

  Mie nimewaza kwa muda mrefu naamini kuna anayejua mengi zaidu kuhusu MTU huyu. mwageni data tuzinyanyambue
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Msanii,
  Unakumbuka ile stori ya muuza madawa ya kulevya Jamaica? Alikuwa anatafutwa na Wamarekani afunguliwe mashtaka lakini serikali ya Jamaica ililazimika kupambana na wapiganaji katika mtaa alikokuwa anaishi kabla ya kukamatwa kwake. The analogy ya kupendwa kwa Lowasa kule kwao ni the same.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Wameapa kufa naye.
  Very sad
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sio LOWASA tu yaani mtu akishakuwa waziri anaonekana kama ana kinga fulani. may be

  • Wananchi wanaamini ana uwezo wa ku loby miradi fulani kwa faida ya jimbo lake
  • wanaamini wasipomchagua wanakuwa wamakosesha jimbo lao kuwa na waziri.
  • Wanaachi wanafarijika tu kuwa waziri kutoka jimboni mwao
  Yaaani inakuwa kama mtego fulani mtu akishakuwa waziri anakuwa kama ana akakinga fulani kwa wapiga kura sasa kwa waziri mkuu ndio usiseme.
   
 5. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Hata Lowasa akishinda ubunge, bado hatadumu kwenye ule mjengo. Maana Slaa anatarajiwa kuwa Rais, na wote waliotumia madaraka vibaya wataishia lupango. Waache tu wapiganie ubunge sasa.

  These guys are living on borrowed time.
   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280

  nicheke kitajiri miye "tehetehethe"
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Utacheka sana mwaka huu mwanetu!
   
 8. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Mimi nachoweza kujuakwa huyu EL Nikwambz hata kabla yakuwa PM akiwa waziri maji mifugo kafanya mambo mengi pale monduli kwanza tatizo lililokuwepo na likiwasumba wamasai ni maji ameweka miundo mbinu ya maji mji wote akawawekea mabwawa mifugo yao ikapata maji akaboresha huduma za jamii amewakamata wahisani monduli kuna mashirika mengi ya kimataifa yanatoa huduma za kijamii akaanzisha mashule ya ma yatima wazungu wanapa misaada sana amefungua mashule vijijini unajua ghalama za jamii umasaiini ni bure ukilinganisha na kwingineko akaweka masoko,akaweka rami mji wote na alikuwa na mipango ya kuweka barabara kutokea ngorongoro maana monduli nikama kisiwa barabara yakuingilia ndiyo yakutokea kazi ameifanya ndiyo maana wamasai hawawezi kumuelewa yeyote zaidi ya EL.
   
 9. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi wanamonduli wana matatizo gani, mbona wanampenda hadi kupitiliza
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Usisahau hili ..kwamba anafanya tafrija kila mara, ambapo anachinja wanyama wengi, na Mmasai kwa hilo unakuwa umegusa mishipa yake yote ya fahamu!
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,547
  Trophy Points: 280
  PayGod, ni kweli wanampenda hadi kupitiliza kwa sababu the guy is a starter na ni performer!. JK ni non starter na non performer na bado anaimbiwa nyimbo za shangwe na mapambio, kama non starter na non performer ndio anashangiliwa hivyo, huyu ambayer kiukweli ni starter na performer, si ndio ataabudiwa kabisa na kutukuzwa!, nenda Rombo ushuhudie jinsi masiya Bazili Pesambili anavyo abudiwa!

  Yote haya "Yanamwisho Haya"-'Kuli' by Shafi Adam Shafi- Page No. 99.
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nakimbiza hisia kichwani kwangu kukubali kwamba Wamonduli ni wafaidika wa UFISADI wa Lowasa.
  Wametuuza
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ata ungekuwa wewe ungemsapport bse ufisadi anaoufanya anawaaidia watu wake
  Kama alikuwa nalamba milioni 152 daily kama capacity charge ya Richard Monduli sasa kwa nini asijenge zahanati,maji safi,barabara.
  Ata mzazi mtoto wako mwizi na unajua fika siku akikamatwa lazima utamtetea
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Which line are you purporting to align?
  Kama mzazi au ndugu anakula na kufaidi mali za wizi za nduguze atajitoaje kuitwa MWIZI?
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mtu mwingine anayeingia ktk pool ya aina ya lowasa ni chenge na watu wake jimboni
   
 16. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Mi nahisi kunafaida kubwa sana wameipata kutokana na uwepo wa huyu bwana!!
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Dudu
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  jamaa yupo chali mikononi mwa CIA.
  let us GET THEM THIS TIME
   
 19. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  jamaa yupo chali mikononi mwa CIA.
  let us GET THEM THIS TIME
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wamasai hawana longolongo... fanya kazi wakuheshimu na lowassa pamoja na greedy yake ya pesa, ni mtu anayefanya kazi to the end, he has the vision and is determined to fulfill the assignment (he has the end in all his missions)

  Unfortunately ni wachache wako hivyo

  I would rather have EL mmoja kuliko JK kumi
   
Loading...