VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Kila analolisema,litajadiliwa na kujibiwa. Kuanzia na wa chini hadi wa juu kabisa Serikalini na chamani. Kila analosema,litapondwa bila kupendwa na kila 'mzalendo' wa Serikalini na ndani ya CCM.
La mwisho ni la jana. Akichangia bajeti huko Dodoma,Lissu alitoa maoni kuwa Rais Mstaafu Kikwete hapaswi kupona katika sakata la madini kwakuwa ni yeye ndiye mtiasaini wa kwanza wa nyaraka za madini miaka ya tisini.Tena wakati huo Kikwete hakuna na kinga.
Maoni hayo ya Lissu yakaripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi. Imekuwa nongwa! Rais Magufuli na hata Waziri Mwakyembe wameonya juu ya kuwazungumzia Marais wastaafu. Marais wastaafu,wakuu wanasema,wanapaswa kuachwa wapumzike.
Vyombo vya habari ndivyo vilivyoonywa. Lissu amesababisha hayo. Lissu anaponza media. Kwanini maneno ya Lissu yasiwe yanapuuzwa? Kuanzia makinikia hadi sasa,imekuwa too much!
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam