Kwanini kwetu Waafrika Mzungu ndiyo UKWELI wa MWISHO Duniani?!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Hapa kwetu TanZania jambo lolote linalofanyika ili lihalalishwe na kumaliza ubishi basi ni lazima tutoe mfano wa Marekani au Ulaya, kwa mfano ukiongelea kuhusu mtoto wa Raisi kupewa madaraka utajibiwa mbona George Bush Marekani alikuwa mtoto wa Raisi, ukiongelea kuhusu gharama za uchaguzi na Wafanyabiahara kuchangia Kampeni za Uraisi utaambiwa mbona Marekani wall street wanachangia, ukiongelea kuhusu viongozi wa mashirika ya umma kwenye nchi masikini kama yetu kuhusu kulipwa mshahara milioni 30 kwa mwezi utaambiwa mbona CEO wa City Bank analipwa milioni 100, ukiongelea kuhusu Viongozi wa TanZania kutibiwa hapa hapa nyumbani utaambiwa mbona Prince wa Uholanzi alipelekwa kutibiwa Uingereza kwa gharama ya nchi!

Mifano mingi sana ambayo inaonyesha kabisa kwamba kwetu sisi Mzungu ndiyo UKWELI pekee hapa Duniani na kila tulifanyalo maadamu kuna Mzungu fulani kalifanya mahali fulani basi ni sahihi kasoro moja tu ndiyo tunapingana na Wazungu nalo ni kuhusu haki za Wasenge na Wasagaji wakati huwo huwo tunataka vyombo vyetu vya Habari viandike chochote kile na kama vikifungiwa tunalalamika kuhusu Uhuru wa vyombo vya Habari na kukimbilia kwa Mzungu utasikia mbona Marekani New York times iliandika hivi na hakuna tatizo sasa kama Mzungu ndiyo kipimo ni kwa nini Ushoga tunaupinga?

Mfano mwingine mzuri ni Kitila Mkumbo tena anajiita msomi anasema kwamba siku 100 za Raisi Magufuli ameshindwa kwa sababu Raisi wa Marekani ndani ya siku 100 alifanya hivi na vile hivyo kwa kuwa Raisi Magufuli hajafanya vile kama Raisi wa Marekani basi ameshindwa tena alienda mbali kabisa na kusema Raisi Obama alisema Afrika inahitaji mifuno imara na siyo Kiongozi Imara lkn anashindwa kuelewa kwamba Obama haijui Afrika, Obama ni Mzungu na anaongelea kuhusu Afrika akilinganisha na Marekani sasa kwenda kuchukuwa ushauri wake kwamba ndiyo UKWELI PEKEE na bila kufanya hivyo hatuwezi kwenda mbele inathibistisha jinsi gani tunavyoamini kwamba anachosema Mzungu ndiyo UKWELI PEKEE hapa Duniani!

*Hii Mada haihusu Ushoga nimetumia ushoga kwenye mfano mmoja tu kati ya mingi niliyotoa!
 
Una mix vitu tofauti....

Kwanza tunayo mifano ya hapa hapa Africa

Ethiopia wanajenga barabara nzuri zaidi kuliko za TZ na gharama nafuu zaidi
Ethiopia wana train za umeme addis ababa kwa dola milioni 430 tu
huku Tz gharama za daraja la coco beach tunalotaka kujenga ni mara mbili ya hizo gharama

Kenya wana kampuni za mafuta zinazolipa kodi nyingi na mafuta yanauzwa nafuu kuliko TZ
sababu kampuni zao ziko listed stock exchange hivyo kuna transparent ya kutosha

Kenya na nchi nyingi za Africa zinakusanya kodi ya kampuni za simu kubwa kuliko TZ
ingawa TZ ya nne africa kwa soko la wateja wa kampuni za simu

Ukweli ni kuwa tunatoa mifano miingi tu ya hapa hapa Africa lakini
serikali hii ya CCM ni sikio la kufa
 
Ingawaje uko nje ya Mada labda ni kosa langu nimeshindwa kuiweka mada jinsi ambavyo nilitegemea ieleweke lkn pia siyo mbaya nikikujibu kuhusu mifano yenu ya Ethiopia na kosa kubwa ambalo wengi wenu mnalifanya ni kujaribu kulinganisha mambo juu juu tu bila kwenda ndani zaidi nitakupa mfano wewe umeisifu Ethiopia kwamba wametuzidi kwa sababu wamejenga treni ya Umeme lkn pia hivi tunavyoandika nchi ya Ethiopia kimetangaza baa la njaa na Umoja wa Mataifa tayari umeanza kujipanga ili kuepusha balaa kama ya mwaka 84' mpaka ukatungwa wimbo wa We are the world sasa ni kwa nini wasiwekeze kwenye chakula cha uhakika kwanza badala ya kujenga treni ya Umeme? Na kama wao wako mbali kiasi hicho ni kwanini wanategemea chakula cha msaada ktk UN? lkn sisi ingawaje pia kuna watu wetu hawapati chakula bora hatuna baa la njaa!

Hiyo treni ya Umeme ya Ethiopia unayoiongela mimi kuna Muethiopia nimekutana Dar ambaye ni Dr.(PhD) Chuo Kikuu huko kwao na akaniambia kwamba anasifu sana mradi wa Dar wa Dart na akasema kwamba anatamani nchi yake ingeanza na mradi kama huu wa kwetu, anasema hizo treni za Umeme kwanza umeme wa uhakika hakuna unakatika katika kama Dar sasa utaziendesha vipi? Na akasema mradi wetu wa Dart uko realistic zaidi kwa nchi yenye maendeleo ya chini kama TanZania na kama tukiusimamia vizuri unatosha kabisa kupunguza kama siyo kuondoa kero ya usafiri hapa Dar!

Kuhusu Kenya sitaki kwenda huko kwa maana nitajaza kurasa hapa!
 
Hivi vinakilishi tunavyotumia ni kazi ya mzungu. Nguo tunazovaa ni kazi ya mzungu. Magari mazuri kazi ya mzungu. Tumetawaliwa kwa miaka mingi, hivyo akili zetu zinashindwa kujitenga na kila anachokifanya mzungu.
 
Ingawaje uko nje ya Mada labda ni kosa langu nimeshindwa kuiweka mada jinsi ambavyo nilitegemea ieleweke lkn pia siyo mbaya nikikujibu kuhusu mifano yenu ya Ethiopia na kosa kubwa ambalo wengi wenu mnalifanya ni kujaribu kulinganisha mambo juu juu tu bila kwenda ndani zaidi nitakupa mfano wewe umeisifu Ethiopia kwamba wametuzidi kwa sababu wamejenga treni ya Umeme lkn pia hivi tunavyoandika nchi ya Ethiopia kimetangaza baa la njaa na Umoja wa Mataifa tayari umeanza kujipanga ili kuepusha balaa kama ya mwaka 84' mpaka ukatungwa wimbo wa We are the world sasa ni kwa nini wasiwekeze kwenye chakula cha uhakika kwanza badala ya kujenga treni ya Umeme? Na kama wao wako mbali kiasi hicho ni kwanini wanategemea chakula cha msaada ktk UN? lkn sisi ingawaje pia kuna watu wetu hawapati chakula bora hatuna baa la njaa!

Hiyo treni ya Umeme ya Ethiopia unayoiongela ni white elephant project mimi kuna Muethiopia nimekutana Dar ambaye ni Dr.(PhD) Chuo Kikuu huko kwao na akaniambia kwamba anasifu sana mradi wa Dar wa Dart na akasema kwamba anatamani nchi yake ingeanza na mradi kama huu wa kwetu, anasema hizo treni za Umeme kwanza umeme wa uhakika hakuna unakatika katika kama Dar sasa utaziendesha vipi? Na akasema mradi wetu wa Dart uko realistic zaidi kwa nchi yenye maendeleo ya chini kama TanZania na kama tukiusimamia vizuri unatosha kabisa kupunguza kama siyo kuondoa kero ya usafiri hapa Dar!

Kuhusu Kenya sitaki kwenda huko kwa maana nitajaza kurasa hapa!

Tuanze na la njaa kwanza....

Njaa ya Ethiopia haina tofauti na ya njaa ya TZ...
watu maskini wa vijijini wakikosa mavuno sababu ya mvua wanakumbwa na njaa
sababu hawana income zingine
njaa yao na ile ya Tanzania kila mwaka vijijini haina tofauti
Why ya Ethiopia inapata attention zaidi?sababu ya population yao...
ya kwetu tunaweza idhibiti wenyewe kwa serikali kugawa vyakula
kama alivyofanya PM Majaliwa hivi karibuni jimboni mwake
ya Ethiopia sababu ya population kubwa inabidi waombe msaada nje

hiyo ya mwaka 84 usisahau Ethiopia ilikuwa na civil war pia...

Sasa kama hata sisi tunapata njaa je ni busara kujenga daraja la coco beach?
kwa vigezo hivyo?

White Elephant ipi kubwa zaidi? treni za umeme au daraja la kigamboni au coco beach?
 
Ingawaje uko nje ya Mada labda ni kosa langu nimeshindwa kuiweka mada jinsi ambavyo nilitegemea ieleweke lkn pia siyo mbaya nikikujibu kuhusu mifano yenu ya Ethiopia na kosa kubwa ambalo wengi wenu mnalifanya ni kujaribu kulinganisha mambo juu juu tu bila kwenda ndani zaidi nitakupa mfano wewe umeisifu Ethiopia kwamba wametuzidi kwa sababu wamejenga treni ya Umeme lkn pia hivi tunavyoandika nchi ya Ethiopia kimetangaza baa la njaa na Umoja wa Mataifa tayari umeanza kujipanga ili kuepusha balaa kama ya mwaka 84' mpaka ukatungwa wimbo wa We are the world sasa ni kwa nini wasiwekeze kwenye chakula cha uhakika kwanza badala ya kujenga treni ya Umeme? Na kama wao wako mbali kiasi hicho ni kwanini wanategemea chakula cha msaada ktk UN? lkn sisi ingawaje pia kuna watu wetu hawapati chakula bora hatuna baa la njaa!

Hiyo treni ya Umeme ya Ethiopia unayoiongela mimi kuna Muethiopia nimekutana Dar ambaye ni Dr.(PhD) Chuo Kikuu huko kwao na akaniambia kwamba anasifu sana mradi wa Dar wa Dart na akasema kwamba anatamani nchi yake ingeanza na mradi kama huu wa kwetu, anasema hizo treni za Umeme kwanza umeme wa uhakika hakuna unakatika katika kama Dar sasa utaziendesha vipi? Na akasema mradi wetu wa Dart uko realistic zaidi kwa nchi yenye maendeleo ya chini kama TanZania na kama tukiusimamia vizuri unatosha kabisa kupunguza kama siyo kuondoa kero ya usafiri hapa Dar!

Kuhusu Kenya sitaki kwenda huko kwa maana nitajaza kurasa hapa!
Majibu mazuri sana. Mradi wa CDA Dodoma ambao sisi tunaudharau ndio uliotumika katika kulijenga jiji la Abuja Nigeria. Wanigeria waliangalia ni wapi wanaweza kupata mradi sahihi wa kujenga makao yao makuu mapya, wakaja kwetu Dodoma. Lakini mtanzania ambaye keshazoea kukiona cha kwake ni kibaya na kina matatizo wala hawezi kuumiza kichwa na kukubaliana na ukweli kwamba yapo mengi mazuri ambayo watu wa nje wanayapata kutoka kwetu.
 
Hapa kwetu TanZania jambo lolote linalofanyika ili lihalalishwe na kumaliza ubishi basi ni lazima tutoe mfano wa Marekani au Ulaya, kwa mfano ukiongelea kuhusu mtoto wa Raisi kupewa madaraka utajibiwa mbona George Bush Marekani alikuwa mtoto wa Raisi, ukiongelea kuhusu gharama za uchaguzi na Wafanyabiahara kuchangia Kampeni za Uraisi utaambiwa mbona Marekani wall street wanachangia, ukiongelea kuhusu viongozi wa mashirika ya umma kwenye nchi masikini kama yetu kuhusu kulipwa mshahara milioni 30 kwa mwezi utaambiwa mbona CEO wa City Bank analipwa milioni 100, ukiongelea kuhusu Viongozi wa TanZania kutibiwa hapa hapa nyumbani utaambiwa mbona Prince wa Uholanzi alipelekwa kutibiwa Uingereza kwa gharama ya nchi!

Mifano mingi sana ambayo inaonyesha kabisa kwamba kwetu sisi Mzungu ndiyo UKWELI pekee hapa Duniani na kila tulifanyalo maadamu kuna Mzungu fulani kalifanya mahali fulani basi ni sahihi kasoro moja tu ndiyo tunapingana na Wazungu nalo ni kuhusu haki za Wasenge na Wasagaji wakati huwo huwo tunataka vyombo vyetu vya Habari viandike chochote kile na kama vikifungiwa tunalalamika kuhusu Uhuru wa vyombo vya Habari na kukimbilia kwa Mzungu utasikia mbona Marekani New York times iliandika hivi na hakuna tatizo sasa kama Mzungu ndiyo kipimo ni kwa nini Ushoga tunaupinga?

*Hii Mada haihusu Ushoga nimetumia ushoga kwenye mfano mmoja tu kati ya mingi niliyotoa!
Kwasababu mpaka sasa sisi bado watumwa kifikra
 
Una mix vitu tofauti....

Kwanza tunayo mifano ya hapa hapa Africa

Ethiopia wanajenga barabara nzuri zaidi kuliko za TZ na gharama nafuu zaidi
Ethiopia wana train za umeme addis ababa kwa dola milioni 430 tu
huku Tz gharama za daraja la coco beach tunalotaka kujenga ni mara mbili ya hizo gharama

Kenya wana kampuni za mafuta zinazolipa kodi nyingi na mafuta yanauzwa nafuu kuliko TZ
sababu kampuni zao ziko listed stock exchange hivyo kuna transparent ya kutosha

Kenya na nchi nyingi za Africa zinakusanya kodi ya kampuni za simu kubwa kuliko TZ
ingawa TZ ya nne africa kwa soko la wateja wa kampuni za simu

Ukweli ni kuwa tunatoa mifano miingi tu ya hapa hapa Africa lakini
serikali hii ya CCM ni sikio la kufa
Hoja iliyopo ni kuleta maendeleo na sio kutafuta mshindi wa ubishi,vijana wa ukawa wengi ni mambumbu japo mnajiona mnajuwa sana...kwanza hujajibu mada,pili hizo takwimu za ujenzi koko beach na reli ya Ethiopia umenukuu wapi au unatoa kichwani ili uonekane mshindi humu JF...."usipige kelele jitahidi kuboresha hoja"
Una mix vitu tofauti....

Kwanza tunayo mifano ya hapa hapa Africa

Ethiopia wanajenga barabara nzuri zaidi kuliko za TZ na gharama nafuu zaidi
Ethiopia wana train za umeme addis ababa kwa dola milioni 430 tu
huku Tz gharama za daraja la coco beach tunalotaka kujenga ni mara mbili ya hizo gharama

Kenya wana kampuni za mafuta zinazolipa kodi nyingi na mafuta yanauzwa nafuu kuliko TZ
sababu kampuni zao ziko listed stock exchange hivyo kuna transparent ya kutosha

Kenya na nchi nyingi za Africa zinakusanya kodi ya kampuni za simu kubwa kuliko TZ
ingawa TZ ya nne africa kwa soko la wateja wa kampuni za simu

Ukweli ni kuwa tunatoa mifano miingi tu ya hapa hapa Africa lakini
serikali hii ya CCM ni sikio la kufa
 
Tuanze na la njaa kwanza....

Njaa ya Ethiopia haina tofauti na ya njaa ya TZ...
watu maskini wa vijijini wakikosa mavuno sababu ya mvua wanakumbwa na njaa
sababu hawana income zingine
njaa yao na ile ya Tanzania kila mwaka vijijini haina tofauti
Why ya Ethiopia inapata attention zaidi?sababu ya population yao...
ya kwetu tunaweza idhibiti wenyewe kwa serikali kugawa vyakula
kama alivyofanya PM Majaliwa hivi karibuni jimboni mwake
ya Ethiopia sababu ya population kubwa inabidi waombe msaada nje

hiyo ya mwaka 84 usisahau Ethiopia ilikuwa na civil war pia...

Sasa kama hata sisi tunapata njaa je ni busara kujenga daraja la coco beach?
kwa vigezo hivyo?

White Elephant ipi kubwa zaidi? treni za umeme au daraja la kigamboni au coco beach?

Tatizo ni kwamba unaamua tu kubisha kwa sababu unazozijua wewe! Umoja wa Mataifa wako Dunia nzima pamoja na nchini kwetu kama TanZania tungekuwa na baa la njaa kama Ethiopia kiasi cha kuhitaji msaada ya chakula ktk nje basi Umoja wa mataifa wangeshasema hivyo, na kuhusu idadi ya Watu Ethiopia hiyo siyo sababu kwani wako milioni 70 na wana nchi kubwa sana tena sehemu kubwa ni nyanda za juu na rutuba ya kutosha wana Nile imepita na isitoshe population density ikilinganishwa na eneo lao siyo kubwa kabisa!

Hapa ni kwamba ni kipi muhimu kutumia mablioni ya fedha kujenga treni ya Umeme au kutumia hizo fedha kulisha watu wako kwanza? Jibu la hilo swali linatofautiana na binadamu na binadamu kwangu mimi ningesema kwanza chakula kwa watu cha kutosha halafu mambo mengine baadaye!
 
Njaa vijijini mbona Tanzania ipo kila mwaka?
na tunajenga madaraja ghali zaidi?

Njaa ya Africa ni watu wa vijijini ambao hawana uwezo wa kununua chakula
hivyo wakikosa mavuno wanapata njaa....
iwe Ethiopia iwe Tanzania....ni the same...ni umasikini

njia moja ya kuondoa umasikini ni ufanisi wa miundumbinu
ambayo inarahisisha movement za kibiashara
ndo maana kujenga treni ya umeme ni smart way....
foleni ya Dar tu inaingiza hasara ya zaidi ya bilioni 50 kila siku...
 
Tofautisha Baa la njaa na kushindwa kupata chakula bora, hivyo vitu viwili tofauti, njaa inayoongelewa nchini mwetu mara nyingi ukosefu wa Lishe lkn siyo kukosekana kwa kitu cha kula kwa 100% lkn Ethiopia na BAA la NJAA yaani watu hawana chochote cha kuweka mdomoni na Serikali haina uwezo wa kuwalisha mpaka inaomba msaada!

Ingawaje ni kweli kwamba kwetu huwa kunatokea matatizo ya uhaba wa chakula hasa kwa jamii zilizotengwa lkn mara nyingi Serikali huwapelekea chakula mara moja na hili hufanyika kwa maana chakula kipo maghala yetu yamejaa vyakula panapotokea dharura tunachukuwa ktk ghalani na kuwapelekea watu wetu wakati Ethiopia hakuna chakula na watu wanakufa ndiyo maana UN inaingilia na ukiangala hakuna sababu ya watu kufa njaa Ethiopia kwa maana sehemu kubwa iko kwenye Bonde la Ufa na rutuba ya kutosha Mto Nile unapita Ethiopia, Mbona Misri hakuna baa la Njaa?

Na sababu ya UN kuingilia ni kwamba Ethiopia hawana fedha ha kununua chalula kwa watu wake na ndiyo maana wanaomba msaada na ukisoma ripoti ya UN fedha ambazo zinahitajika ni kama milioni 200 US Dollars lkn hawana!
 
Tatizo ni kwamba unaamua tu kubisha kwa sababu unazozijua wewe! Umoja wa Mataifa wako Dunia nzima pamoja na nchini kwetu kama TanZania tungekuwa na baa la njaa kama Ethiopia kiasi cha kuhitaji msaada ya chakula ktk nje basi Umoja wa mataifa wangeshasema hivyo, na kuhusu idadi ya Watu Ethiopia hiyo siyo sababu kwani wako milioni 70 na wana nchi kubwa sana tena sehemu kubwa ni nyanda za juu na rutuba ya kutosha wana Nile imepita na isitoshe population density ikilinganishwa na eneo lao siyo kubwa kabisa!

Hapa ni kwamba ni kipi muhimu kutumia mablioni ya fedha kujenga treni ya Umeme au kutumia hizo fedha kulisha watu wako kwanza? Jibu la hilo swali linatofautiana na binadamu na binadamu kwangu mimi ningesema kwanza chakula kwa watu cha kutosha halafu mambo mengine baadaye!
Hawa vijana wa ufipa ni wasaliti wa asili wa hili taifa kuanzia marreale alisaliti wapigania uhuru kwa ukibaraka wa wazungu...so ni laana inawafuata...mtei...kamrithisha mkwewe...so..wanatamani sana wazungu.
 
Tofautisha Baa la njaa na kushindwa kupata chakula bora, hivyo vitu viwili tofauti, njaa inayoongelewa nchini mwetu mara nyingi ukosefu wa Lishe lkn siyo kukosekana kwa kitu cha kula kwa 100% lkn Ethiopia na BAA la NJAA yaani watu hawana chochote cha kuweka mdomoni na Serikali haina uwezo wa kuwalisha mpaka inaomba msaada!

Ingawaje ni kweli kwamba kwetu huwa kunatokea matatizo ya uhaba wa chakula hasa kwa jamii zilizotengwa lkn mara nyingi Serikali huwapelekea chakula mara moja na hili hufanyika kwa maana chakula kipo maghala yetu yamejaa vyakula panapotokea dharura tunachukuwa ktk ghalani na kuwapelekea watu wetu wakati Ethiopia hakuna chakula na watu wanakufa ndiyo maana UN inaingilia na ukiangala hakuna sababu ya watu kufa njaa Ethiopia kwa maana sehemu kubwa iko kwenye Bonde la Ufa na rutuba ya kutosha Mto Nile unapita Ethiopia, Mbona Misri hakuna baa la Njaa?

Na sababu ya UN kuingilia ni kwamba Ethiopia hawana fedha ha kununua chalula kwa watu wake na ndiyo maana wanaomba msaada na ukisoma ripoti ya UN fedha ambazo zinahitajika ni kama milioni 200 US Dollars lkn hawana!

Ethiopia sio nchi ya kukosa dola milino 200
kuna zaidi ya hapo.... wananunua 'airbus dreamline' zaidi ya moja kwa shirika la ndege lao
wakati hiyo dolla milioni 200 ni kama ndege moja tu...

Kuna zaidi ya hapo.......ni sawa na sisi tunaposaidiwa kujenga vyoo na nchi wahisani
haina maana hatuna hela ya kujenga hivyo vyoo

Au unataka niambia Magufuli alipopewa msaada wa kujenga flyover ubungo na JICA
bilioni 100 ...ni kwamba hatuna kabisa uwezo wa kupata bilioni 100 tukajenga wenyewe?
 
Majibu mazuri sana. Mradi wa CDA Dodoma ambao sisi tunaudharau ndio uliotumika katika kulijenga jiji la Abuja Nigeria. Wanigeria waliangalia ni wapi wanaweza kupata mradi sahihi wa kujenga makao yao makuu mapya, wakaja kwetu Dodoma. Lakini mtanzania ambaye keshazoea kukiona cha kwake ni kibaya na kina matatizo wala hawezi kuumiza kichwa na kukubaliana na ukweli kwamba yapo mengi mazuri ambayo watu wa nje wanayapata kutoka kwetu.

Master Plan ya Abuja ilifanywa na kampuni tatu za Kimarekani kwa jina la International Planning Associates.

Mchoraji mashuhuri wa nyumba wa Japan, Kenzo Tange, pia alisaidia katika kuchora mji wa Abuja.

source:
por.habitats.org
en.m.wikipedia.org/wiki/Abuja
Archnet.org
Etsav.upc.se

Ningeomba kujua vipi CDA imesaidia kujenga Abuja kwa namna yoyote.

Unaweza kulinganisha Dodoma na Abuja?
Wizara zote za serikali ya Nigeria imehama Abuja pamoja na mabalozi wanaoiwakilisha nchi zao, Nigeria.
 
Sio kweli kwamba wamarekani ndio wameuchora mji wa Abuja. CDA ya dodoma ndio iliyowapa ramani Nigeria wakaenda kuitumia kwa kujenga Abuja. Siwezi kulinganisha Dodoma na Abuja, siwezi kulinganisha Lagos na Dar. Siwezi kumlinganisha mtanzania na mnigeria.
 
Ingawaje uko nje ya Mada labda ni kosa langu nimeshindwa kuiweka mada jinsi ambavyo nilitegemea ieleweke lkn pia siyo mbaya nikikujibu kuhusu mifano yenu ya Ethiopia na kosa kubwa ambalo wengi wenu mnalifanya ni kujaribu kulinganisha mambo juu juu tu bila kwenda ndani zaidi nitakupa mfano wewe umeisifu Ethiopia kwamba wametuzidi kwa sababu wamejenga treni ya Umeme lkn pia hivi tunavyoandika nchi ya Ethiopia kimetangaza baa la njaa na Umoja wa Mataifa tayari umeanza kujipanga ili kuepusha balaa kama ya mwaka 84' mpaka ukatungwa wimbo wa We are the world sasa ni kwa nini wasiwekeze kwenye chakula cha uhakika kwanza badala ya kujenga treni ya Umeme? Na kama wao wako mbali kiasi hicho ni kwanini wanategemea chakula cha msaada ktk UN? lkn sisi ingawaje pia kuna watu wetu hawapati chakula bora hatuna baa la njaa!

Hiyo treni ya Umeme ya Ethiopia unayoiongela mimi kuna Muethiopia nimekutana Dar ambaye ni Dr.(PhD) Chuo Kikuu huko kwao na akaniambia kwamba anasifu sana mradi wa Dar wa Dart na akasema kwamba anatamani nchi yake ingeanza na mradi kama huu wa kwetu, anasema hizo treni za Umeme kwanza umeme wa uhakika hakuna unakatika katika kama Dar sasa utaziendesha vipi? Na akasema mradi wetu wa Dart uko realistic zaidi kwa nchi yenye maendeleo ya chini kama TanZania na kama tukiusimamia vizuri unatosha kabisa kupunguza kama siyo kuondoa kero ya usafiri hapa Dar!

Kuhusu Kenya sitaki kwenda huko kwa maana nitajaza kurasa hapa!
Mimi nashangaa sana nchi inayosifiwa kwamba ina maendeleo ukiachilia mbali janga la njaa kila siku wanakamatwa wahamiaji haramu.
Na kama kungekuwa na maendeleo makubwa kama inavyelezwa tusingeona wanachi wao wakihama kila siku na wangine wakifa kwa njaa.

Na ukiangalia makundi hayo yote ni ya vijana ambao ndiyo nguvu kazi.
Ila ninachokiona baadhi wachangiaji ni jazba za vyama kuchangia bila kuangalia hali halisi.
Na kwa hapa kwetu sijaona makundi ya watu wahamiaji kama ilivyo kwenye nchi nyingine.
 
Ethiopia sio nchi ya kukosa dola milino 200
kuna zaidi ya hapo.... wananunua 'airbus dreamline' zaidi ya moja kwa shirika la ndege lao
wakati hiyo dolla milioni 200 ni kama ndege moja tu...

Kuna zaidi ya hapo.......ni sawa na sisi tunaposaidiwa kujenga vyoo na nchi wahisani
haina maana hatuna hela ya kujenga hivyo vyoo

Au unataka niambia Magufuli alipopewa msaada wa kujenga flyover ubungo na JICA
bilioni 100 ...ni kwamba hatuna kabisa uwezo wa kupata bilioni 100 tukajenga wenyewe?

Serikali inaomba mpaka gari la wagonjwa kutoka Japan.

Sijui ni kukosa aibu, ujinga au uvivu wa kufikiri kuomba kijigari wakati Waziri anatembea na Land Cruiser VX.
 
Sio kweli kwamba wamarekani ndio wameuchora mji wa Abuja. CDA ya dodoma ndio iliyowapa ramani Nigeria wakaenda kuitumia kwa kujenga Abuja. Siwezi kulinganisha Dodoma na Abuja, siwezi kulinganisha Lagos na Dar. Siwezi kumlinganisha mtanzania na mnigeria.

Naomba source au itakuwa habari ya vijiweni.

Mimi nimekupa source NNE (4) kuonyesha kuwa Wamarekani walikuwa planners na Mjapani ndiyo architect.
 
Back
Top Bottom