Kwanini kwenye kubadili Passport hakuna foleni kama NIDA licha ya kesho kuwa siku ya mwisho?

hapana mkuu.
hadi atimize miaka 18, ndio maana wale jamaa hawafungi ofisi zao
Kwahiyo chini ya miaka 18 anakuwa raia wa nchi gani? Chini ya miaka 18, haruhusiwi kumiliki laini ya simu..? Passport inataka kitambulisho cha uraia, inakuwaje hapo kwenye kupata passport ya mtoto wako aliye below 18?
 
mkuu maswali magumu hayo.
 
matunduizi, Uhamiaji wanadai ni Watanzania 200000 tu ndo wanapass za kielektroniki katika ya Watanzania zaidi ya M55 kwahiyo kupata pass ni anasa katika nchi yetu.

Sasa kama wanataka Watanzania wote tuwe na hizo Pasi za Kusafiria kwanini wasipunguze Gharama yake na pia waondoe Urasimu wake ambao upo na umekuwa ukilalamikiwa sana hapo Uhamiaji Mkuu? Je, ukitumia tu ' Logic ' ya kawaida hapo Kosa ni la hao Watanzania Milioni 55 au ni Wao wenyewe?
 
matunduizi, Uhamiaji wanadai ni Watanzania 200000 tu ndo wanapass za kielektroniki katika ya Watanzania zaidi ya M55 kwahiyo kupata pass ni anasa katika nchi yetu.
Unatakiwa uwe na uthibitisho wa uraia wa mzazi wako. Sisi wa miaka ya 47 wazazi wetu hawakuwa na vyeti vya kuzaliwa. Hivyo unamtafuta mzee wa miaka 90 aje kuthibitisha kuwa alikuwepo wakati baba yako anazaliwa na kuwa alijulishwa hivyo na babu yako ambaye ndiye baba mzazi wa baba yako
Hilo ni moja ya matatizo yanayotukabili huko. Lakini pia unatakiwa kuonesha sababu ya wewe kutaka hiyo pasipoti. Kama ni safari toa ushahidi wa hiyo safari vinginevyo hupewi pasipoti. Kwa hali hiyo basi, pasipoti ni anasa.
 
Sasa kama wanataka Watanzania wote tuwe na hizo Pasi za Kusafiria kwanini wasipunguze Gharama yake na pia waondoe Urasimu wake ambao upo na umekuwa ukilalamikiwa sana hapo Uhamiaji Mkuu? Je, ukitumia tu ' Logic ' ya kawaida hapo Kosa ni la hao Watanzania Milioni 55 au ni Wao wenyewe?

Uhamiaji hawajakaa kibiashara wanaisababishia serikali kutokkusanya maduhuli mengi katika pass za kusafiria
 
jamaa anasema hakuna hayo mambo, vishoka tu ndio walia watu fedha bure wakati taratibu ziko wazi.

Kama rushwa zipo hadi hapo, basi ndio maana hiyo kitu inafanywa kama kitu kikuubwa
Mkuu, juzi nimeenda kurasini vigezo vyote nilitimiza. Niliingia saa 4 asubuhi nikaitwa counter saa 7, nikaingia biometric saa 10. Saa 10:20 nikawa nimemaliza kila kitu nikaambiwa next week niende mambo ya ndani kuchukua.
Ikiwa uko na vigezo utakwama kwenye time tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_20200130-210548.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
matunduizi, Uhamiaji wanadai ni Watanzania 200000 tu ndo wanapass za kielektroniki katika ya Watanzania zaidi ya M55 kwahiyo kupata pass ni anasa katika nchi yetu.
Wanaikosesha serikali Mapato hao watu wa uhamiaji.chukulia ingetoa hata passport milioni moja tu kwa mwezi kila passport Ni laki moja na nusu .Serikali ingepata bilioni 150 chap chap ndani ya mwezi mmoja tu
 
Back
Top Bottom