Kwanini kuwa na mawaziri toka Zanzibar wakati wao hawana hata mmoja toka bara?

ndio watanganyika wanaufagilia huu Muungano... Ukiulaza wanasema eti Baba wa Taifa Blah blah...NCHI INAONGOZWA NA MAWAZO YA MWALIMU... KAMA VILE "SAINT "FULANI...

Kwa wakati ule ilikuwa sawa. Lakini kwa wakati sidhani tunawahitaji waje kutuamulia mambo bara kama wao wasivyotaka tushike nafasi kwao
 
Mwiba,
haya maswala ya Wazanzibar na Watanganyika unazitoa wapi mkuu wangu. Tanzania ni nchi moja, tukiendelea kupeana madaraka kwa fikra za Kibaguzi hatutafika popote. Kinachotakiwa kutazamwa ni uwezo wa watu hawa iwe Mzanzibar au Mtanganyika na tunaposahau uwezo na kufikiria zaidi tofauti zetu ndio maana tunalundika wanawake ili kuleta uuwiano bungeni, kesho Wakristu watadai ni zamu yao wanataka rais afuataye awe Mkristu na wanawake watadai, nasi Wakerewe tutakuja dai kupewa kiti hicho..

Tanzania kamwe haitaweza kuendelea kwa sababu ya vigezo kama hivi na nakuhakikishia kwa mtaji huu hatuna miaka mingi kuvunja hiyo amani na utulivu kwa sababu kila kiongozi kwa rangi yake huja ku represent kikundi cha watu wake na sii maendeleo ya Taifa. Hii ni hatari sana kwa vyama na uongozi wowote nchini na ndio maana CUF na Chadema hawataweza kuondokana na shutuma kwa sababu sisi wenyewe tunafikiria uongozi kwa tofauti ya makabila, dini na rangi za mhusika...

Mkuu Mkandara na Victahi hapo juu,
Nikufahamishe kuwa mambo ya ubaguzi hayakuwepo siku za nyuma.

Kuanzia awamu ya mwalimu Wazanzibar walikuwa wanafanya kazi bara bila maneno. Ushahidi upo, mitaani utasikia duka la mpemba na hakuna aliyehoji.
Utasikia shambani kwa mpemba wakimaanisha wazanzibar.

Chuki ya ubaguzi wameipanda Wazanzibar kwa matusi eti wabara ni wakoloni.

Ni hawa hawa wametaka wimbo wao wataifa, nembo yao ya taifa, Bank yao, shirika lao la bandari na bandari huru, huku wanataka kuwa na access na bara kama Watanganyika.

Kwamfano wanataka bandari huru waingize bidhaa zao halafu kodi iwe ya serikali yao lakini soko liwe la bara! Ni hao hao wana bunge lao na katiba yao lakini wanaingia bunge la Tanganyika tena kwa wingi na kuathiri hata maamuzi ya Watanganyika.

Wanapokwenda Dodoma posho na mishahara yao inalipwa na Wabara,hawajakataa kupokea. Wamepiga marufuku mahakimu na mawakili wa bara kwao, Lakini nenda wizara ya fedha, Afya, Elimu, Utumishi n.k wamejazana wanafanya kazi za bara na kuwaziba wabara riziki zao

Hili hawalisemi, wamejazana Dar wakifanya kazi na biashara wakisema bara ni wakoloni. Sasa kama hawataki ukoloni wanfanya nini bara?

Kama ni uwezo wa kazi kwanini tusiwaalike warundi, Waganda na Wakenya wenye uwezo huo kuwa mawaziri kama Wazenji kwa maana ya ni nchi ambazo zipo nje ya Tanganyika.

Sidhani bunge la Tanganyikaa limekosa wachapa kazi hadi kwenda kuwachukua watu hawa wenye chuki na sisi.Mbona mafuta walikimbilia kusema si la muungano, sasa mawaziri wa znz wanasimamia nini bara

Wazanzibar wakitaka kuondoka kwenye muungano Wabara hawana cha kupoteza, Mbara atapoteza nini. Kama yupo Mzenji akayethibitishia abara watapoteza atueleze tutapoteza nini.

Hulka ya wazanzibar ni '' Chako ni chetu, changu ni changu''.

Kwa mantiki hiyo najisikia dhalili sana kuwa na kiongozi mzanzibar si kwasababu nawachukia kama binadamau nachukia tabia zao za umimi.

Kwanza hata huko nje huwa hawajiiti watanzani wanajiita wazanzibar sasa kwanini tuwe na kiongozi asiyeipenda nchi anayotawala.?
 
Mkuu Nguruvi3 asante kwa ufafanuzi kuntu..

Nimefukua huu uzi wa siku nyingi na kukuta hiyo post yako hapo juu nikiwa najaribu kutafuta faida hata 1 tu ambayo Tanganyika inapata kutokana na huu muungano. Hakuna.

Anayejua faida ya muungano kwa Tanganyika naomba anitoe tongotongo tafadhali.

Naona Znz pekee ndo inapata manufaa lukuki kutokana na muungano
 
Mkuu hiyo post ni ya 2010 , yote tuliyosema yanatokea wazi

Leo wanalalamika muungano mbaya wa ukoloni, kesho wanataka access ya soko la sukari na bidhaa zao. Leo wanataka uhuru wa biashara za nje. Kesho wanataka soko la sukari kwa lazima

Mtanganyika hana cha kupoteza bali ametoa sana kwa znz. Kama hawataki,kila la kheri
 
Mkuu hiyo post ni ya 2010 , yote tuliyosema yanatokea wazi

Leo wanalalamika muungano mbaya wa ukoloni, kesho wanataka access ya soko la sukari na bidhaa zao. Leo wanataka uhuru wa biashara za nje. Kesho wanataka soko la sukari kwa lazima

Mtanganyika hana cha kupoteza bali ametoa sana kwa znz. Kama hawataki,kila la kheri
Kuna umuhimu gani kuendelea kuwakataza kuwa na mamlaka yao kamili (yaani tuvunje Muugano) maana wao ndio wanaotunyonya sisi Wabara?

Wanatunyonya halafu tunawakatalia wao kujitenga jinsi wanavyodai, tunachoking'ang'ania kwao ni nini?

Muungano hauna faida, uvunjwe
 
Kuna umuhimu gani kuendelea kuwakataza kuwa na mamlaka yao kamili (yaani tuvunje Muugano) maana wao ndio wanaotunyonya sisi Wabara?

Wanatunyonya halafu tunawakatalia wao kujitenga jinsi wanavyodai, tunachoking'ang'ania kwao ni nini?

Muungano hauna faida, uvunjwe
Tusiwaze kuuvunja kwanza, tujaribu kuwaza namna ya kuufanya uwe na faida hizo tunazozani hazipo kwa sasa.
 
Kuna umuhimu gani kuendelea kuwakataza kuwa na mamlaka yao kamili (yaani tuvunje Muugano) maana wao ndio wanaotunyonya sisi Wabara?

Wanatunyonya halafu tunawakatalia wao kujitenga jinsi wanavyodai, tunachoking'ang'ania kwao ni nini?

Muungano hauna faida, uvunjwe
Sidhani kama wanawakataliwa
Kwanza, ilikuwepo tume ya Warioba ikikusanya maoni ya wananchi kuhusu muungano

Hakuna, narudia hakuna Mzanzibar hata mmoja aliyesimama na kusema hataki muungano
Tulisikia wakitoa maoni ya Serikali 2, serikali 3 na muungano wa mkataba

Serikali 2 na 3 ziliweza kujadilika. Muungano wa mkataba haukuweza hata kujadiliwa

Muungano wa mkataba ni njia ya kujitoa katika muungano lakini wabakishe masuala yenye masilahi kwao kama umiliki wa ardhi, soko la ajira, soko la bidhaa, ulinzi na usalama.

Hata siku moja hutasikia wazanzibar wakilalamikia mambo hayo kuwa ya muungano
Muungano wa mkataba hauna faida wala maana kwa Tanganyika, hoja ikafa mapema mno

Kwa mantiki wasioutaka muungano bado waliamini kuna mambo wanayataka katika mahusiano ya ambazo zingekuwa nchi mbili tofauti.Ni kwa ukweli kuwa ndani au nje ya muungao Znz ipo katika kivuli cha Tanganyika, ndivyo maumbile ya dunia yalivyo

Serikali 2 ilitakiwa na Waunguja ambao kwa sababu za kihistoria walihisi tatizo la usalama wao
Utakubuka Mbunge wa Unguja aliyesema 'muungano ukifa wapemba hamtakanyaga Unguja''

Serikali mbili ndiyo iliyozaa ' Wazanzibar wa Mkuranga na Machotara'

Tume ya Warioba ikapitia maoni na kuona mambo 7 tu ya muungano, wakataka uwepo wa Tanganyika na Zanzibar na kushirikiana kwa mambo hayo.

Hili lilikuwa na maana moja kwa wazanzibar, kwamba, uwepo wa Tanganyika utatoa fursa kamili kwa Watanganyika kuwa na sheria zao kama walivyo Wazanzibar.

Hoja ikatia hofu wznz kuwa ule mteremko wa kupitia muungano utafikia kikomo.
Tanganyika itaweka sheria zake ambazo zitawaathiri wazanzibar

Waliokataa serikali 3 si Watanganyika, ni Wazanzibar ambao ndani ya Bunge la katiba walikuwa na fursa kama mshirika mwenza, walishindwa kuafikiana yakajitokeza makundi ya uchama ya ''kutoaminiana''

Laiti wangekubali serikali 3 leo wasingekuwa na malalamiko kwasababu uwezo wao ungekuwa mkubwa katika kuamua hatma yao.

Ni ngumu kuwalaumu Watanganyika kwasababu wao hawana chombo tofauti
Wenye uwezo ni Wazanzibar kupitia BLW na SMZ.

Nakuhakikishia hakuna hata siku moja kumekuwepo na jaribio la kukataa muungano.
Hata wale wanaokuja Dodoma bado hakuna anayesimama na kutaka kitu tofauti

Kwa maana nyingine wazanzibar wameshindwa kutumia SMZ, BLW na kupitia Wabunge wao Dodoma kueleza kitu tofauti, hawajashikiliwa , mazingira yaliyopo wanaona ni afadhali kuliko tofauti.

Kwa upande wa Tanganyika, Znz ni sehemu tu kama nyingine. Hakuna malalamiko ya kutunyonya kwa mantiki hiyo. Kinachotokea ni majibu kuwa muungano una faida kwao

Katika kufanya hivyo ndipo yanaanishwa mambo ya wazi jinsi wanavyonufaika na muungano.
Hii ni kufutiaupotoshaji unaonezwa. Kwa mfano, eti Tanganyika inaionya znz kiuchumi

Hisia za kunyonya zinapata nguvu pale ambapo ZNZ inakuwa 'treated' kuliko maeneo mengine.

Kwa mfano, nini mchango wa znz katika kuendesha muungano ukilinganisha na maeneo ya bara?

Kwanini wadai hata kisicho chao kama haki,wakatae vyao visiwe vya muungano?

Kwa Watanganyika uwepo wao au kutokuwepo kwao hakuna athari kama ilivyo kwao
 
Back
Top Bottom