Kwanini kuwa na mawaziri toka Zanzibar wakati wao hawana hata mmoja toka bara?

Acha unafiki wewe! Kuna tatizo gani kuwa na wa-TZ visiwani 4 kwenye baraza? na uzuri ni kwamba wanashika wizara ambazo ni za Muungano hivyo hakuna ubaya hapo. nani alikwambia kwamba uwaziri unatokana na mikoa? Mbona tunaleta porojo zisizokuwa na mshiko hapa!!!

Pia angalia vizuri hilo baraza mikoa yote uliyoitaja imetoa anagalu manaibu waziri: Mfano L. Nyalandu (naibu viwanda/biashara) anatoka Singida Kskzn, Mh. G. Teu (Fedha) anatoka Mpwapwa, Mh. C. Chizza (Kilimo) anatoka Buyungu - Kibondo, Kigoma. Tatizo lenu mmetawaliwa na sera za ukabila na upendeleo za CCM! Ingekuwa CDM mngepiga kelele sana ooh upendeleo sijui nini vile! Mbona Kilimanjaro imetoa wengi hamjapiga kelele (Maghembe, Matayo, Mwanri, Cyril, na ukipenda hata Lucy mweke huko)

Job K,

Baba_Enock sio mnafiki!

Soma Katiba ya JMT Ibara ya 55(2):

(2) Pamoja na Mawaziri waliotanjwa katika ibara ndogo ya (1), Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuwateua Naibu Mawaziri. Naibu Mawaziri wote hawatakuwa wajumbe wa Baraza la Mawaziri.
 
Katika Baraza "jipya" la Mawaziri (29) aliowateua JK kuna Mawaziri wanne kutoka Zanzibar wakati huhuo kuna Mikoa mitatu hakuna Waziri hata mmoja...

Kuna nini Zanzibar hadi kuwa na uwakilishi mkbwa kiasi hik katika Baraza la Mawaziri?


katavi-Pinda
Rukwa-?????????
 
Hivi wazanzibari ni watanzania kumbe?
Niliwahi kuwa ng'ambo wakati fulani, nikakutana na ndugu yangu wa visiwani, wakati tunajitambulisha, nikasema i am from tanzania. yeye akasema he is from Zanzibar tena kwa mbwembwe sana.

Au kwenye issue za kuchota ulaji Tanganyika wao ndio ghafla wanakuwa watanzania?
 
Dogo naona we una ubinafsi zaidi.Lazaro Nyalandu yeye si katoka singida??

kinachotakiwa ni wao kuchapa kazi hata wangekua wanatoka mkoa mmoja. Mi wangekuwepo kina magufuli hata 29 ndani ya nchi hii wanaotokea mkoa mmoja wangeweza wakapewa tu ili mladi wwatuhakikishie maendeleo.
 
Dogo naona we una ubinafsi zaidi.Lazaro Nyalandu yeye si katoka singida??

kinachotakiwa ni wao kuchapa kazi hata wangekua wanatoka mkoa mmoja. Mi wangekuwepo kina magufuli hata 29 ndani ya nchi hii wanaotokea mkoa mmoja wangeweza wakapewa tu ili mladi wwatuhakikishie maendeleo.

Soma Post #28:

Naibu Mawaziri wote hawatakuwa wajumbe wa Baraza la Mawaziri.
 
kikwete saaizi hafikirii kitu kingine zaidi ya dini yake y kiislamu kwa kuwalazimisha watz kuitii n kulipia kodi kitu ambacho hatuko tayari kusikia na wala kukiona..............

non sense, politics gat nothing to do with islam, ufisadi, uwizi ni kazi za shetani mungu hayupo hapo.!!! acha mawazo mgando mbona baraza limejaa wakristo wengi tu???
 
Mkuu kwa taarifa na ufahamu wako Zanzibar sio Mkoa, ndani ya Zanzibar kuna Mikoa 5 kati ya hiyo Mikoa 2 ipo Pemba na Mikoa 3 ipo Unguja.

Zanzibar ni Nchi ambayo kabla ya Muungano ilikua ni Jamhuri ya watu wa Zanzibar, ni upotofu kufikiria Zanzibar kama ilivyo ni Mkoa haiko hivyo, haitakua wala haiwi Ng'o habari ndio hiyo

Naomba kuwasilisha kwa hatua zako.
 
Katika Baraza "jipya" la Mawaziri (29) aliowateua JK kuna Mawaziri wanne kutoka Zanzibar wakati huhuo kuna Mikoa mitatu hakuna Waziri hata mmoja...

Kuna nini Zanzibar hadi kuwa na uwakilishi mkbwa kiasi hik katika Baraza la Mawaziri?

chiza ni wa kigoma na nyalandu ni wa singida
 
Katika Baraza "jipya" la Mawaziri (29) aliowateua JK kuna Mawaziri wanne kutoka Zanzibar wakati huhuo kuna Mikoa mitatu hakuna Waziri hata mmoja...

Kuna nini Zanzibar hadi kuwa na uwakilishi mkbwa kiasi hik katika Baraza la Mawaziri?
Si mchezo Tatizo lenu nyinyi mnaifananisha zanzibar sawa na mkowa hajui ya kuwa zanzibar imeungana na tanganyika kama nchi kamili na dodoma ni part ya Tanganyika wakati huo na ilikuwa haina utawala wake. tatizo ni akili finyu mlizokuwa nazo na vile vile mara ya mwisho nilipoangalia Zanzibar ina mikoa 5 sasa kwa mahisabu yako hayo mkoa mmoja haujawakilishwa na kwa nini pia usijiulize mbona kilimanjaro ina mawaziri kama 5 na hiyo mikoa uliyoitaja hamna hata mmoja au kwa nini mawaziri wakatoliki ni wengi kuliko madhehebu mengine.lete maada nyengine tujadili na siyo huu upuuzi
 
katika baraza "jipya" la mawaziri (29) aliowateua jk kuna mawaziri wanne kutoka zanzibar wakati huhuo kuna mikoa mitatu hakuna waziri hata mmoja...

Kuna nini zanzibar hadi kuwa na uwakilishi mkbwa kiasi hik katika baraza la mawaziri?
nyie ndio akili zenu zinawaza udini,ukabila,umikoa achana na mambo hayo wote watanzania kijana badili fikra
 
Kwa hiyo unamaanisha zanzibar kuna wachapa kazi sana ukilinganisha na Tanzania bara? mbona kwenye baraza la mawaziri zanzibar hakuna mbra hata mmoja?



Zanzibar sio nchi hivyo hawawezi kuchagua waziri kutoka bara, wa zanzibar wamechaguliwa kwa sababu ya muungano ambao umeunda nchi moja inaitwa Tanzania.
 
Mbona uchaguzi wa mawaziri ulitakiwa usishirikishe kabisa Zanzibar. Walishavunja muungano zamaniiiii
 
nyie ndio akili zenu zinawaza udini,ukabila,umikoa achana na mambo hayo wote watanzania kijana badili fikra

Bado haujajibu swali langu la Msingi! Mimi naongelea uwakilishi wa Wa-Tanzania wala si u-mikoa wala u-dini! Sawa Joyce!
 
Note: Baraza la Mawaziri lazime liwawakilishe wa-Tanzania wote.

Mkuu, hii ni kwa sheria gani au kifungu gani cha katiba? Mimi naamini Rais anaweza kuwa na baraza la mawaziri lenye idadi ndogo kuliko idadi ya mikoa iliyopo. Kwa mfano, angeweza kuunda baraza lenye wizara kumi tu!
 
hivi ww kaka hujuwi hata ulise malo kumbuka serikali iliyoundwa ni ya Jamuhuri ya Muungano si Serikali ya Tanganyika kwa hakika hao wanne kwa upande wa zanzibar pia kidogo ila tu wanzanibar hawana uchu wa madaraka kumbuka kuwa serikali ya Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili na usifananishe kabisa kuwa zanzibar ni mkoa kama mikoa mingine zanzibar ni nchi yenye mamlaka yake ndani ya nchi yake sawa fikiri kabla ya kusema
 
...Kuna nini Zanzibar hadi kuwa na uwakilishi mkbwa kiasi hiki katika Baraza la Mawaziri?

Kuna sovereignty.

Wanzanzibari wanatuhurumia na tushukuru. Kinadharia wangeweza kudai, na wangekuwa na hoja, wakisema katika baraza la watu 29 wawakilishwe na mawaziri 14 unusu. Kama Wanzanzibari 5 kwenye cabinet ni wengi, mbona sisi tuna 24?

Tulivyokubaliana nao 1964 , Zanzibar ni sovereign entity ndani ya Muungano. Tuliamua kuungana na kakisiwa ka watu laki moja ushee sisi tukiwa milioni nane wakati huo kutengeneza pande zenye hadhi sawa.

Sovereignty maana yake haijalishi wana watu wangapi, au ukubwa gani, au uchumi kiasi gani, wao ni kitu kamili kisichotawaliwa. Kiongozi wa Tanzania Bara akikataa kuhudhuria ghafla ya Rais analaaniwa kwa kutikisa nchi, lakini Karume anakuja kusikiliza hotuba za Kikwete uwanja wa Taifa anapojisikia. Kwa nini, wao ni sov ereign entity.

Ndivyo tulivyokubaliana nao wenyewe. Na wajanja huwezi kuwala, inakula kwetu kwa sababu sisi ndio wajinga tunaokataa kuangalia upya Muungano kwa vile mawazo yetu ni mgando wa mtindi. Milioni takriban 40 na millioni moja mtaunganaje muwe na hadhi sawa? Wako wachache kiasi kwamba ukiwa na Masters degree we waziri! Na Mtanganyika ukitaka kupanda haraka pitia Zanzibar (Rais Mwinyi). Kanchi kama wilaya, Unguja na Pemba zinaingia Newala na Masasi mara tano! Lakini tumewakubalia sovereignty.

Mawazo mgando kwa sababu hakuna anaeweza kuutetea Muungano kwa kutuambia faida zake. “Adui ataweka himaya visiwani na itatishia usalama wetu.” Ndio historia tuliyofundishwa. Nchi masikini ya makapuku hii itazuia aduni gani hii? Kwamba Mmarekani akitaka kukutungua itabidi kwanza apate viwanja vya kupaki vifaru visiwani? Na North Korea akitaka kumtungua Mmarekani itabidi kwanza achukue Jamaica kuhifadhi vifaru, au? Historia. Kikwete akizindua Bunge la kumi ametoa sababu kwa nini tuendelee na Muungano: ”Tunalo jukumu la kihistoria la kuhakikisha kuwa Muungano wetu unadumu na unazidi kuimarika.”

Muungano wetu ni historia tu, zaidi ya hapo ni mzigo wa hasara kwa Watanzania Bara. Tulikosea.
 
hivi ww kaka hujuwi hata ulise malo kumbuka serikali iliyoundwa ni ya Jamuhuri ya Muungano si Serikali ya Tanganyika kwa hakika hao wanne kwa upande wa zanzibar pia kidogo ila tu wanzanibar hawana uchu wa madaraka kumbuka kuwa serikali ya Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili na usifananishe kabisa kuwa zanzibar ni mkoa kama mikoa mingine zanzibar ni nchi yenye mamlaka yake ndani ya nchi yake sawa fikiri kabla ya kusema

Sasa naomba uvute subira ili uwezo kutoa hoja vizuri baada ya utendaji wao wa kazi na si kulaumu kuwa zbr inamawazir 4, 5 1 iyo si hoja ya kutilia manani

lakini hata hivo inaonekana kaka kidogo mwalimu wa history na civcs huku chini ulimkimbia nadarasani ila lamsingi tu elimu haina mwishi bado muda unao jiendeleze utaweza kwa nini usiweze hao waloweza wananini. rudia shule au soma magazetu sikiliza habar na kesho kutwa kutakuwa kuna sistoria nyingi juu ya Tanganyika
 
Back
Top Bottom