Kwanini kuwa na mawaziri toka Zanzibar wakati wao hawana hata mmoja toka bara?

Bob_Dash

Member
Nov 1, 2010
90
13
Nimeona orodha ya mawaziri wapya pamoja na manaibu, kilichonishangaza ni kuona majina mengi ya watu toka Zanzibar, sasa kwanini kutawaliwa na watu toka Z'bar wakati wao hawana hata waziri ama naibu waziri toka bara?
 
Ile ni serikali ya zanzibar haiwahusu wabara, na hii ni ya Muungano, inawahusu wote wabara na zanzibar so wana haki ya kuwa hata wakuu wa mikoa au wilaya za huku bara. Kama inawezekana kuwa na rais Mzanji kwanini kwenye uwaziri isiwezekane?
 
Watanganyika mnasemaje kwa hili naona watu wasiotimia hata milioni moja wameweza kuchota sehemu kubwa kwa kuwemo katika Mawaziri na Manaibu ndani ya serikali ya Muungano ,kumbuka Tanganyika ina watu milioni zaidi ya arubaini.
Sasa hapa inakuwaje ? Je ni sawa au ni haki ? Kwa Zanzibar au Wazanzibar kupewa zaidi ya robo ya ngazi za uwaziri ?
 
Mkuu unashangaa mawaziri? Vipi kuhusu ghalib, rais mwinyi, waziri mkuu ahamed salim
 
Watanganyika mnasemaje kwa hili naona watu wasiotimia hata milioni moja wameweza kuchota sehemu kubwa kwa kuwemo katika Mawaziri na Manaibu ndani ya serikali ya Muungano ,kumbuka Tanganyika ina watu milioni zaidi ya arubaini.
Sasa hapa inakuwaje ? Je ni sawa au ni haki ? Kwa Zanzibar au Wazanzibar kupewa zaidi ya robo ya ngazi za uwaziri ?

...Hata miye nimeshtuka kidogo, ila, hii inaweza backfire kwa ccm, waki-underperfom, something which is very likely.

...Halafu, kunaweza tokea hoja ya ...hawa wanamachungu gani na maendeleo ya bara?...
 
Kwa sababu rahisi sana: Kila mzanzibar ni Mtanzania... lakini sio Kila Mtanzania ni Mzanzibar... in short Mtanzania bara sio Mzanzibar! delete the thread you have an answer.
 
that's why i simply hate muungano, cuase you have reps from znz in the parliament and some becoming ministers but with no passion whatsoever for the mainland. the only exception is wizara ya muungano but i hate the fact that we have them in other ministries.:angry:
 
Watanganyika mnasemaje kwa hili naona watu wasiotimia hata milioni moja wameweza kuchota sehemu kubwa kwa kuwemo katika Mawaziri na Manaibu ndani ya serikali ya Muungano ,kumbuka Tanganyika ina watu milioni zaidi ya arubaini.
Sasa hapa inakuwaje ? Je ni sawa au ni haki ? Kwa Zanzibar au Wazanzibar kupewa zaidi ya robo ya ngazi za uwaziri ?
Kwa maoni yako wewe unaonaje?
 
Hayo ndio makubaliano ya kuulinda Muungano!
1.Shamsi Vuai Nahodha.
2.Dr.Hussein Ali Mwinyi.
3.Mahadhi Juma mahadhi.
4.Prof.Makame Mnyaa Mbarawa.
5.Dr.Abdallah Juma Abdallah
 
Kwa sababu rahisi sana: Kila mzanzibar ni Mtanzania... lakini sio Kila Mtanzania ni Mzanzibar... in short Mtanzania bara sio Mzanzibar! delete the thread you have an answer.

Siyo kweli tungekuwa na serikali tatu ingewezekana zenji kuwa na mbara lkn siri kali hii ya kidikteta haiwezekani!
Refer hata mch.mtikila's speech.
 
niliwaambia kuwa kwenye CCM hakuna mtu anathubutu kumwambia Mwenyenyekiti wao kuwa kakosea! wanzanzibar wote wa nni kwenye Cabinet? au ndo kujipendekeza wasije wakadaI NCHI YAO?
 
Nimeona orodha ya mawaziri wapya pamoja na manaibu, kilichonishangaza ni kuona majina mengi ya watu toka Zanzibar, sasa kwanini kutawaliwa na watu toka Z'bar wakati wao hawana hata waziri ama naibu waziri toka bara?
kweli mimi nakuunga ,mkono-ndo mana tunasema swala la muungano linabidi kuangaliwa kwa upya-kama tumeunagana swala la mtu wa zanzibar kuwa na power huku isingekuwa tatizo kama pia,watu wa bara wangekuwa na power visiwani,yani watu wa bara pia wangekuwa mawarizi huko visiwani-ila mimi naona hapa kuna tatizo-ni mtindo wa CHANGU CHANGU-CHAKO CHANGU-mana wao huku bara tuna wanzibar wengi tu-kwenye vyeo mbalimbali-lakini wao kutoa vyeo kwa wa bara inakuwa ngumu kidogo-nashindwa kujua kwa nini CCM inakuwa na sera ya ajbu ya mtindo huu yenye kuwalea foreigners kwa kiasi hiki-kama ni kuungana-waache wimbo wao wa taifa,bendera yao na prezda wao-mbona kuna nchi zimeungana na kumekuwa na rais mmoja na mambo mengi yanaendaeshwa kiumoja?cha ajabu zaid sasa kuna makamu wa rais 2 huko zenji-inamana kukiwa na chama kingine chenye upinzani mkubwa kunaweza kuwa na makamu wa rais 3,ili ku-please raia wa zenji-NINACHOTAKA KUSEMA NI KWAMBA-KAMA WANZIBAR WANAWEZA KUWA NA VYEO HUKU BARA-BASI IWE VIVYO HIVYO KWA W-BARA KUCHAGULIWA KUWA VIONGOZI/MAWAZIRI HUKO ZANZIBAR-BEYOND HAPO BORA MUUNGANO UFE
 
Wajameni ishu si uzanzibari wao jamani.. Je wanaweza kupiga kazi!?. km wanaweza then sio ishu' si tunaka maendeleo na upige kazi ishu ya ulipotoka watajuana na wake zao!! Hatutafuti mke tunatafuta waziri' na Wazanzibari ni watanzania pia'
 
Mwiba,
haya maswala ya Wazanzibar na Watanganyika unazitoa wapi mkuu wangu. Tanzania ni nchi moja, tukiendelea kupeana madaraka kwa fikra za Kibaguzi hatutafika popote. Kinachotakiwa kutazamwa ni uwezo wa watu hawa iwe Mzanzibar au Mtanganyika na tunaposahau uwezo na kufikiria zaidi tofauti zetu ndio maana tunalundika wanawake ili kuleta uuwiano bungeni, kesho Wakristu watadai ni zamu yao wanataka rais afuataye awe Mkristu na wanawake watadai, nasi Wakerewe tutakuja dai kupewa kiti hicho..

Tanzania kamwe haitaweza kuendelea kwa sababu ya vigezo kama hivi na nakuhakikishia kwa mtaji huu hatuna miaka mingi kuvunja hiyo amani na utulivu kwa sababu kila kiongozi kwa rangi yake huja ku represent kikundi cha watu wake na sii maendeleo ya Taifa. Hii ni hatari sana kwa vyama na uongozi wowote nchini na ndio maana CUF na Chadema hawataweza kuondokana na shutuma kwa sababu sisi wenyewe tunafikiria uongozi kwa tofauti ya makabila, dini na rangi za mhusika...
 
Mimmi hii nchi kwakweli khasara kabisa!imenichosha sana!
Eti makamu wa rais wawili what crap is tht?kodi za wanachi kuzitumia vibaya tu!msssxzxzzzz
 
Back
Top Bottom