Kwanini kusini mwa Jangwa la Sahara kuna.................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini kusini mwa Jangwa la Sahara kuna..................

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WomanOfSubstance, Sep 1, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Umaskini uliokithiri....na matokeo yake kuna...
  Maambukizi ya kutisha ya HIV na Ugonjwa wa UKIMWI.....MALARIA, magonjwa mengineya tropiki, utapiamlo.....elimu duni.....na mengineyo.Tukiangalia kwa undani tunapata kwamba nchi nyingi kusini mwa jangwa hili zina utajiri wa kutisha wa maliasili - ardhi yenye rutuba, hali nzuri ya hewa, madini ya kila aina, misitu , wanyama na ndege wa kila aina, maji ( mito, maziwa,bahari),mvua za kutosha.......na mengineyo mengi!
  TATIZO NI NINI??????
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  africa inaitwa the last frontier........

  time yetu bado.......
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,052
  Trophy Points: 280
  Huku ndiko kwenye neema zote za dunia hii.
  Wazungu wanataka kutumaliza kisha waje kurithi nchi
   
 4. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni uongozi - Good Governance

  Viongozi wetu hawajaamua kuwa wazalendo wa kweli. Ila siku wakiamua kila kitu kitabadilika.
  Bado tuna stand chances za kuondokana na huu umasikini uliokithiri kama viongozi wetu wataamua kufuata njia sahihi ya utawala bora.

  Believe me, wanajua wanatakiwa wafanye nini ila hawataki kufanya kwa makusudi kwasababu ya maslahi binafsi. Wanaiba mpaka vitu vingine wanasahau kama ni vyao kwao na bado wanahitaji na vingine...

  Ni ulafi uliopitiliza.

  Mungu awasaidie siku moja wauone Mwanga na wajirudi kusaidia jamaa zao.
   
 5. S

  SIPENDI Member

  #5
  Sep 2, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Among other things, people out there aren't smart compared to other people from the rest of the world... let us keep on watching the dynamic world
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hahahahaaa....tatizo ni nini? Tatizo hatuna akili. Wewe angalia Afrika Kusini ilivyoendelea. Au Afrika Kusini haipo kusini mwa jangwa la Sahara?

  Licha ya utawala dhalimu dhidi ya weusi kwa miaka mingi, yale mazungu yameijenga ile nchi bana. Kuna atakayebisha kuwa kusingekuwa na wazungu Afrika Kusini ingekuwa hapo ilipo?

  Ukweli wa mambo, mkubali au mkatae, Miafrika Ndivyo Tulivyo. Najua mtanipinga sana tena sana tu, lakini mtaishia kunipinga kwa maneno tu. Na tayari tunajua maneno matupu hayaleti maendeleo wala kubadilisha hali tuliyonayo.

  Ni mpaka hapo tutakapoanza kuvumbua vitu na mambo ndio tutakapoendelea. Na mpaka sasa huo uwezo hatuna.
   
Loading...