Kwanini kura zisihesabiwe vituoni moja kwa moja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini kura zisihesabiwe vituoni moja kwa moja?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Solomon David, Nov 1, 2010.

 1. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kulingana na mahojiano yanayoendelea live sasa hivi ITV kati ya Masako na Joshua Joel kutoka sumbawanga (Rukwa), kuna jambo nimelisikia ambalo limenitatiza sana. According to Joshua, matokeo hayajatangazwa kwa vile masanduku ya kura yamechelewa kuletwa kwenye kituo cha kuhesabia kura.

  Hii business ya kuhamisha masanduku toka sehemu moja kwenda nyingine kabla ya hesabu haijafanyika (kama ndivyo ilivyotokea) inatia wasiwasi wa usalama wa matokeo hayo. Nilivyoelewa mimi, kura zinatakiwa kuhesabiwa vituoni na kila kitu kinamalizika hapo kabla ya "kuhamishwa" kwenda sehemu nyingine.

  Ningependa kweli kujua kama kweli utaratibu umebadilishwa, na if yes, kwa nini kura zisihesabiwe moja kwa moja vituoni?
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu CCM wanajua watashindwa kuchakachua.
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ndungu yangu leo mimi nikuwa nasimamia masanduku yana hesabiwa na kubadikwa matokeo ya kila kituo pale pale kumbuka unaweza kuta kituo cha shule x lakini kina vituo vingine 60 sasa kinachoenda kufanywa kwenye kata ni majumlisho pamoja na kupitia malalamiko ya mawakala au ya wasimamizi na kuanza kujumlisha na kutoa certificate kwa madiwani ndipo wanapotoa matokeo ya kata baada ya matokeo ya kata yanapelewa kwenye jimbo napo wana pitia kama kuna tatizo wana jumlisha ndipo wanatoa matokeo sasa kuna tatizo la uelewa wa mawakana na wasimamizi kwenye kujaza form na kuhesabu na kujumlisha na kutoa maana kuna vihesabu na ukizubaa unaliwa au utafanya mamo kuwa magumu hupo kwenye kata vinginevyo wanaweza kuhesabu kula sehemu yoyote kama itatokea tishio la kiusalama kwa wasimamizi....
   
 4. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ndiyo inanitia wasiwasi
   
 5. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haaa, kwa hiyo kinachofanyika ni kujumlisha kura zilizokwishahesabiwa tayari kwenye vituo?
  Kwa jinsi nilivyomsikia huyo mtangazaji wa ITV, ilionekana kama kura hazijahesabiwa at all.... mpaka masanduku yaletwe somewhere kwenye kituo cha kuhesabu kura.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Namsikiliza huyu mtangazaji wa ITV akipewa taarifa (Masako?) akipewa matokeo ya udiwani na ubunge anaachia reporters waseme idadi, wakitaka kutaja kura za urais anawakataza na kuwaambia msitaje, kwa nini?

  Halafu anaongea kama kakabwa koo au amemeza dyck. Wanaboa kichizi.
   
 7. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha ha, huyo ni Masako (wale wale wanaotaka kupata U-DC toka kwa mkwere kama akifanikiwa kuiba hii election).

  CCM wameshalose hii election ... wanatafuta tu namna ya kuiba kura. Kwa nini wanazuia kura zisitangazwe?
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ni wapi ambapo nitaweza kupata matokeo yote ya kura zilizopigwa katika kila kituo tofauti na zile za nec? Nataka kuandika paper kuhusu uchaguzi wa 2010 na mustakabali wa kisiasa wa Tanzania kwa siku zijazo.
   
 9. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wasiliana na chadema makao makuu
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona ndo atakachowasilisha kesho Slaaaaaaaa
  Cheki na makao makuu yao
   
 11. lynxeffect22

  lynxeffect22 JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 625
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndugu wadau naomba kuwasilisha.
  Hivi kwa nini tume ya taifa ya uchaguzi isiwe wazi kuhusu mambo ya kura. Mimi nafikiri utaratibu mzuri ni ule wa kura zote kupigwa vituoni, zihesabiwe papo hapo, matokeo ya kituo yatangazwe na kila wakala apewe copy yake na wananchi wabandikiwe kwenye ukuta wa matangazo nje ya kituo. Hii itasaidia kila chama kujumlisha kura zake makao makuu ya uchaguzi bila kutegemea kusubiri msimamizi wa uchaguzi ambaye anaweza kuja kuconfirm na kuyatangaza rasmi tu.

  N.B: Nilikua nafikiri masanduku ya kura yawe 'transparent' ili mwanzo wa zoezi kila wakala aone hakuna kitu ndani. Na wale wanaokuja mara kwa mara kwenye vituo vya kura wakati zoezi likiendelea wasiruhusuiwe kuwa karibu na masanduku ya kura.

  ELIMU YA URAIA NI MUHIMU SANA ILI KUENDELEA KUONGEZA MWAMKO WA MABADILIKO KWA TANZANIA YETU
   
 12. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono ndugu yangu!
   
 13. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Kaka no research no right to speak!! Hii mbona ndo inafanyika katika vituo vyote? Mbona chaguzi zote ndo zilivyo? Mbona Mabox ni transparent?

  Halafu ukiwa mwananchama wa JF unauliza maswali ya kijinga hivi unaonyesha wazi wewe si mwenzetu na wala huna nia na mabadiliko ya nchi hii. (Mtanisamehe kama nimekuwa mkali ila nachukia sana maswali ya hivi tena kutoka kwa kijana.)
   
 14. m

  makumvi Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Niwazo zuri, nadhani litafaa kwakuwa ni rahisi hata wananchi kufahamu matokeo mapema
   
Loading...