Kwanini kura za Mtulia zimepungua kwa zaidi ya 60%?

Hilo gazeti nafikiri wangeandika hivi UKAWA mgombea wao 2015 alipata kura elfu 70 safari hii mgombea wao wa UKAWA Salum Mwalimu kapata kura elfu 12 ambazo ni pungufu ya kura elfu 58 inamaanisha nini kwa UKAWA?
Nimekuelewa maana watu wanachagua chama siyo mtu, good!
 
Kwa kilichotokea Kinondoni sidhani kama Bushman ataendelea na biashara ya kununua wabunge na madiwani.
 
Ipo siku hawa wezi watajuta....ipo siku familia za hawa wezi zitalipa...ipo siku watalia...
 
Ipo siku hawa wezi watajuta....ipo siku familia za hawa wezi zitalipa...ipo siku watalia...
Sure watalipa.... Hsia nlizonazo moyoni juu ya hawa jamaa onl God knows, siku itafika na haki ya akina Mwangosi na Akwilina itapatikana hapa hapa duniani (Tanzania).. na watailipa kwa jinsi ile ile
 
Waliojiandikisha ktk daftari la mpiga kura jimbo la Kinondoni ni 264,055 jimboni humo na waliojitokeza kupiga kura ktk uchaguzi mdogo wa marudio tarehe 17 February 2018 ni watu 45,000. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar-es-Salaam.

Nini kilichofanya watu zaidi ya 220,000 kuamua kutotumia haki yao kikatiba kupiga kura ktk uchaguzi huu mdogo wa marudio ktk jimbo la Kinondoni?

WanaJamiiForums pamoja na wajuvi wa sayansi ya siasa / Political science, Philosophy and History fungukeni ili tupate kumbukumbu ya tukio hili lisilo la kawaida ktk siasa za Tanzania.
 
Kwa mujibu wa magazeti ya leo ni kwamba pamoja na Mtulia kushinda kwa kishindo kwa kupata kura 30,000 plus, lakini kura hizo ni pungufu kwa zaidi ya kura 40,000 plus ukilinganisha na kura alizopata mwaka 2015. Hii inamaanisha nini kwenye demokrasia?

Chanzo: Magazetini!
Jumla ya waliopiga kura 2015 walikuwa wangapi?
Huoni kwamba wapiga kura wamepungua?
Je kura za Cuf au Chadema au UKAWA hazijapungua?
 
Jumla ya waliopiga kura 2015 walikuwa wangapi?
Huoni kwamba wapiga kura wamepungua?
Je kura za Cuf au Chadema au UKAWA hazijapungua?
Kuna sehemu mtu kafanya analysis inayoonyesha kura zote zimepungua, hata zile za Idd " wetu " hazikufikiwa this time. Ila nimemuelewa mkuu Yehodava!
 
Back
Top Bottom