Katika maswala yetu ya umoja wa kusaidiana na kufarijiana katika kikundi chetu likaletwa wazo la kila mtu aje na mke wake siku ya sherehe ya kikundi chetu... lakini miongoni mwa wadau tulionao katika kikundi wamepinga vikali na kudai kwamba hakuna haja ya mtu kuja na mkewe hapa.. mmoja akadai yeye ndani ya miaka mitano hajawahi kuongozana na mkewe kwenda maeneo yoyote yale... jamani kwa nini iwe noma kuongozana na mkeo kwenye shughuli mbalimbali kama harusini, msibani hata kwenye nyumba za ibada...........