Kwanini kunakuwa na utofauti wa muda katika kipindi fulani cha mwaka?

Mwee

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
240
602
Nimeileta hili ili nisaidiwe kupata ufafanuzi zaidi maana najua hapa kuna wajuzi wa mambo kwa nyanja mbalimbali. Suala langu ni kuhusiana na utofauti wa saa kati ya eneo moja na lingine.

Naomba nitumie kati ya muda wa Afrika mashariki ambao upo katika longtudo nyuzi 45 mashariki mwa Greenwich.

Kuanzia mwezi Aprili hadi Oktoba kila mwaka tunakuwa na tofauti ya saa 2 kati yetu na GMT ambapo sisi tunakuwa mbele. Lakini kuanzia mwezi Oktoba hadi Machi tunakuwa mbele kwa saa 3.

Katika soma soma yangu ya somo la Jiografia tangu shule ya msingi hadi sekondari sijawahi kusoma kuhusu hiki zaidi ya kufundishwa tu namna ya kutafuta muda.

Sasa nauliza ni nini kinasababisha utofauti huu wa muda fulani tunakuwa mbele kwa saa 2 na mwingine kwa saa 3?
 
GMT iko pale pale, kinachobadilika ni local time kama za Uingereza na za time zone kama za Marekani.

Kwa mfano, sasa hivi Uingereza wanatumia British Summer Time - BTS/British Dailyght Time Zome (Daylight Saving Time) ambayo ni GMT+1, ingawa GMT iko based on Greenwhich, London na kwa GMT muda wa Uingereza ungetakiwa kuwa GMT kamili.

So, GMT iko palepale kwa sababu hiyo ndiyo dira ya saa zote za dunia (in terms of tunapoanza kuhesabia time zones) hatuwezi kuibadilibadili.

Kuna kitu kinaitwa Daylight Saving Time wanarudisha nyuma masaa au kupeleka mbele ili wapate siku yenye mwanga zaidi.

Kumbuka unavyokuwa karibu na Ikweta, urefu wa mchana na usiku haubadiliki sana, lakini unavyokaribia the poles, ndivyo urefu wa usiku au mchana unavyobadilika kulingana na msimu wa mwaka. Mpaka kuna wakati unapata siku yenye mchana ea saa 24, au usiku wa saa 24, at the poles.

So, ni nchi (au states kwa Marekani) wanaamua kuongeza au kupunguza saa moja ili giza lisiingie mapema.

Swali la kitoto ila kuuliza sio ujinga! Asubuhi mwanga wa jua sio mkali na jioni sio mkali, ni nini kinasababisha?
 
Back
Top Bottom