Kwanini kuna wivu na hasira kubwa kwa watu wanaomiliki usafiri binafsi?

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
12,958
26,020
Huwa sielewi kwanini watu huwa wanakuwa na hasira na wivu na watu wenye magari, wakati kuna miongoni mwao wanatakiwa kuonewa huruma tu, mana wapo ambao gari zinawatesa.

Majuzi hapa kuna mtu alileta uzi kwamba katapikiwa na mrembo kwenye gari, basi raia kibao wakamshukia kama mwewe .

Huku mtaani ndio hatari maana wanaamini kila gari ni ya mkopo, utasikia gari yenyewe ya mkopo, unabaki unacheka tu.

Wengine wakiona mwanamke anadrive wanaamini kahongwa, kuna jamaa nimewahi kaa nae nyumba moja, alikuwa haamini kabisa kama mwanamke anaweza nunua gari kwa hela zake.

Hivi kwanini tunakuwa na mindset za namna hiyo, tena mpka humu JF wamejaa kibao, lisitajwe gari mahali utasikia "tushajua unamiliki gari".
 
Basi gongana na daladala uone raia kwenye basi watakavyoanza kukupigia kelele kwa hasira hata kama daladala ndo lina makosa .. yaani sijawaelewaga kabisa.
 
Umaskini na Chuki ni pete na kidole mzee
kwan umesahau sku ile kiduku alivokuwa na ile RANGE ROVER sport yake afu kwa bahat mbaya njian akagonga bata wa watu, raia wakamkazia kinoma.
Dah raia wanakuwaga na hasira sana..
 
  • Thanks
Reactions: _ID
No one has right to tell someone how to live his or her own life or what to own.

Floyd mayweather kwa kukomoa kaamua kununua Roll Royce 7 zinazofanana
img_1200x900$2019_02_06_12_56_54_139426.jpg
 
Gari kwa nchi kama Tanzania ni anasa ndo maana unaweza nunua gari toka Japani kwa milioni 4 au 5, ukaja kuliipishwa ushuru milioni 12,000,000 au zaidi
Huko mbona mbali kiongoz kuna gari ya hadi 1$ (we unalipia usafirishaji na bima tu) ila ukiileta hapa inakuwa nongwa. roho ya kimaskini mbaya sana.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom