Kwanini kuna wabunge wapo kwenye kamati zaidi ya moja?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
KWANINI WABUNGE WENGINE WAPO KWENYE KAMATI ZAIDI YA MOJA?

Na Elius Ndabila
0768239284

Sawa! Swali lako ni la msingi. Labda kwa faida ya wengine nianze kwa kusema hivi:-

Utaratibu unaongoza kupata kamati hizi za Bunge ni kwa mjibu wa Kanuni za kudumu za Bunge. Kifungu cha 135 cha kanuni za kudumu za Bunge kinampa nguvu Spika namna ya kuunda hizi kamati. Lakini swali lako linasema kwanini Mh Hasunga na Mh Gwajima wameonekana katika kamati zaidi ya moja?

Majibu yake ni haya:-
Sheria zinatoa mwanya kwa baadhi ya wajumbe kutoka kwenye kamati fulani kuwa wanaweza kuwa pia wajumbe wa kamati nyingine. Kifungu cha 135(4) kimeeleza hivi, "Wajumbe walioteuliwa kwenye kamati ya kanuni za Bunge, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Kamati ya masuala ya UKIMWI au kamati nyingine kwa kadiri Spika atakavyoona inafaa wanaweza pia kuteuliwa kuwa Wajumbe wa kamati nyingine".

Kwa mkutadha huu bila shaka Wabunge uliowaona kwenye kamati zingine basi wameangukia kwenye kamati hizo ambazo zimetajwa kikanuni kuwa wajumbe wake wanaweza kuwa kwenye kamati zaidi ya moja.
 
Hata hivyo hatufuatilii hilo bunge kibogoyo la wezi wa kura, hivyo pangeni mtakavyo Lakini hatuna muda nalo.
 
Back
Top Bottom