Kwanini kuna uwekezaji mdogo wa kampuni za bima katika soko la hisa DSE?

Agrey998

Member
Jul 8, 2019
88
125
Tofauti na nchi zilizoendelea ambapo uwekezaji wa makampuni ya bima katika masoko makubwa ya hisa ni mkubwa na hutazamwa zaidi na wawekezaji wengi duniani kwa Tanzania Sijawahi kuona kampuni yoyote ya bima ya Tanzania au ya nje ikawa listed katika soko la hisa Dar es salaam.

Lakini biashara ya bima hufanya vizuri hata katika swala zima la faida, kwa makampuni ya bima Tanzania au hata duniani ni mashahidi wazuri wa hilo.

Uwekezaji ungeanzia katika elimu juu ya watu kuhusu umuhimu wa bima na pia hata elimu ya uwekezaji ingetolewa kwa watu maana watu ndo wateja katika biashara ya bima.

Kwa niliyoona katika masoko makubwa ya hisa kama NYSE, NASDAQ, Shanghai stock exchange biashara ya bima imechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wake

Kwa maoni yangu makampuni ya bima yakiwa listed katika soko la hisa itakua hatua kubwa sana kiuchumi na katika biashara ya soko la hisa Tanzania , maana hata mitaji itakua katika soko la hisa la DSE na hata fursa za uwekezaji katika soko la hisa zitapanuka kwa kiasi kikubwa.

Mawasiliano hoja
 

Walec

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
940
1,000
Elimu ya haya mambo bongo bado sana...hata vyuoni haikidhi kabisa..DSE wana kazi kubwa sana
 

Agrey998

Member
Jul 8, 2019
88
125
Elimu ya haya mambo bongo bado sana...hata vyuoni haikidhi kabisa..DSE wana kazi kubwa sana
Ni kweli lakini pia hata taasisi zetu za serikali zimekuwa zikikwamisha haya mambo nakumbuka 2014 wakati kampuni ya swala imekua kampuni ya kwanza ya mafuta na gesi kuwa listed kwenye DSE nakumbuka walilalamika sana kuwa TPDC walikua wakiwahujumu , pengine hata katika bima huenda sio elimu pekee inakwamisha huenda kuna vingi
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
15,347
2,000
Waulize waliowanunua hisa za Vodacom mara ya mwisho walipata dividend ya shilingi ngapi? na bei ya hisa zao imepanda au kuporomoka?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom